Mkoba wa uchawi unavyomtesa mume wangu

Mkoba wa uchawi unavyomtesa mume wangu

Khaa ndugu yangu Bujibuji, mkasa wa mtu huo. Huwa nafanya ushauri kwenye mahusiano na uandishi wa makala za mahusiano. Huo nimeuleta nipate na mawazo yenu wadau. Dunia kila mtu ana lake jambo.
Mahusiano yana siri nzito sana.
Ungetuambia kuwa ni kisa cha mtu mwingine yuko huko kaskazini mashariki mwa uwanja wa mapambano
 
huyu ni paka mwongo huyo mbona harudi kujibu anasoma comment
Mmh leo ndugu Wakurochi sikuwez, tulia bhana unapokuwa mshauri katika masuala ya mahusiano na unakutana na changamoto zingine, napaswa kuziweka mezani ni rahisi kupata na mawazo mengine.
 
Nikiwa na umri wa miaka 19 nilikabithiwa na bibi mzaa mama mkoba wa uchawi. Bila kuukataa niliupokea kwa kuaminishwa ungenisaidia ningeweza kufaulu na kufanya vyema kielimu, kwani ilikuwa ni kiu yangu kubwa pale kijijini.
Kweli nilipoupokea baada ya muda niliona matokeo mazuri katika elimu na kweli hatimye nilifika hadi chuo na kupata Ajira taasisi kubwa nchini.
Nikiwa ofisini na tena mjini maisha mazuri,baada ya mwaka nilipata mwanaume akaniona na nikamzalia watoto wawili. Lakini hivi navyozungumza nimeshaacha kazi yangu kwa kufuata maelekezo ya mkoba.
Kwangu hainiumi bali kwa mume wangu ndio inaniuma, kila siku ziendazo anazidi kufirisika, anazidi kudhoofu afya yake na hata kazi ameshasimamishwa na ndugu zake wamemtenga, wakiamini yeye ameendekeza mapenzi kwangu haambiliki pasipo wao kujua, sio akili yake bali ni mkoba wangu.
Sharti ni yeye na mimi tuwe wote waganga, mimi nilikubali na kuacha kazi yangu niliyoajiriwa ila mume wangu hayupo tayari kuwa saidia wangu.
Imefika kipindi hata nguvu za kiume ni tatizo, pesa imekuwa ngumu na watoto shule za gharama tumeshindwa kuwalipia.
Natamani kumuokoa mume wangu na watoto wangu, ila sharti la suluhu ni mimi labda kufa. Natamani kwenda kujikabithi kwa Mola ila naogopa kuumbuka kwa heshima yangu jamii itanionaje.
Na mmmuhumba
0624 440 454
Tiktok mmmmuhumba
Tangazo limekaa utamu sana
 
Ungetuambia kuwa ni kisa cha mtu mwingine yuko huko kaskazini mashariki mwa uwanja wa mapambano
Uko sahihi. Ila kubwa ni binadamu tuna mikasa mingi, napokutana na mtu au mtu anapiga simu na kueleza jambo kama hili ni zito na jepesi kumshauri kwa kufuata imani. Ila linagharimu maisha ya mtu, mambo mengine yanatisha.
 
Ila hakuna watu wa ajabu kama washirikina. Unakuta mtu alienda kwa mganga miaka hiyo, akatoa kafara ya mnyama. Madhara yanayokuja kutokea baadae ni kwamba watoto wa kizazi chake hawazai. Hivi tatizo huwa ni nini? Kwanini mtu anahatarisha maisha ya ukoo usio na hatia kwa tamaa zake. Ushirikina huwa unawasaidia nini?? Mwenye kujua anijuze.
 
Tatizo linapompata mtu yeyote, kila mmoja huwa ana waza kwa namna yake kulitatua na mawazo ya kwanza huwa ni yeye kujifikiria namna ya kutoka katika lile shimo, kwahiyo uamuzi wowote anao ona unamtoa yeye ndio ataouchukua kwa haraka.
Matokeo huwa ni majuto ila kwanza ni yeye anatokaje ( self centred in decision and deontology) hii sio tu ushirikina hata nje ya ushirikina utokea.
 
Huo mkoba unatesa sana katika jamii ila watu ni kimyakinya tu. Utasikia namuachia Mungu!! Pambana, angamiza huo mkoba kwa gharama yoyote ili watu waishi kwa amani. Ogopa nguvu isiyoonekana.
 
Tatizo linapompata mtu yeyote, kila mmoja huwa ana waza kwa namna yake kulitatua na mawazo ya kwanza huwa ni yeye kujifikiria namna ya kutoka katika lile shimo, kwahiyo uamuzi wowote anao ona unamtoa yeye ndio ataouchukua kwa haraka.
Matokeo huwa ni majuto ila kwanza ni yeye anatokaje ( self centred in decision and deontology) hii sio tu ushirikina hata nje ya ushirikina utokea.
Yaani wameingiza koo katika matatizo makubwa sana. Haswa vibibi
 
Nikiwa na umri wa miaka 19 nilikabithiwa na bibi mzaa mama mkoba wa uchawi. Bila kuukataa niliupokea kwa kuaminishwa ungenisaidia ningeweza kufaulu na kufanya vyema kielimu, kwani ilikuwa ni kiu yangu kubwa pale kijijini.
Kweli nilipoupokea baada ya muda niliona matokeo mazuri
Chukueni mkoba wenu muupeleke Kawe madhabauni kwa Bwana kwa mtumishi wa Mungu Mtume Mwamposa atauteketeza kwa upako na kuchomwa moto. Wakati huo huo Nanyi (familia) mtaombewa na mtafunguliwa na kuwekwa huru kutoka falme hizo feki za mikoba ya uganga.
 
Nenda Kwa kuhanimusa akuombee na ukabidhi mkoba
 
Back
Top Bottom