Mkesha Mwaka Mpya: Polisi yasema kukaa ufukweni mwisho saa 12 jioni

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kuelekea mkesha wa mwaka mpya, Jeshi la Polisi Nchini limewataka Wananchi watakaokusanyika katika fukwe za Bahari na Maziwa kurejea nyumbani ifikapo saa 12 jioni.

Vilevile uchomaji wa Matairi umepigwa marufuku na kwakuwa unasababisha uharibifu wa miundombinu mingi ambayo imejengwa kwa gharama, pia ni kero kwa raia wema.

Aidha, Polisi wamepiga marufuku Disko Toto Nchini kote na Watoto wametakiwa kusherehekea chini ya uangalizi wa Wazazi au Walezi.


390EE962-72B9-43DF-BA61-CF630FDAE0CB.jpeg

2F2841BA-6A6E-48B7-B595-E8D906A48B1E.jpeg
 
Jeshi la polisi nchini limesema kwa siku ya leo katika shamrashamra za kuukaribisha mwaka 2021 wanaopenda kwenda kwenye fukwe za bahari na maziwa ( beach) mwisho wa kuwepo maeneo hayo ni saa 12 kamili jioni.

Nawatakia mwaka mpya 2021 wenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wapo sawa Sana maana Kuna wengine wanatumia Giza kwenye mikusanyiko kufanya Uhalifu
 
Kwenye kuchoma matairi naunga mkono. Unatoka zako huko huna hili wala lile unakuta matairi yamechomwa barabarani unashindwa kupita
 
Back
Top Bottom