Mkeo ni kivuli chako. Chochote utakachofanya au unachotaka afanye atafanya. Akikusumbua ujue wewe ndio msumbufu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,894
MKEO NI KIVULI CHAKO. CHOCHOTE UTAKACHOFANYA AU UNACHOTAKA AFANYE ATAFANYA. AKIKUSUMBUA UJUE WEWE NDIO MSUMBUFU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mkeo ukimuona hana akili ujue wewe ndio huna akili. Ukimuona anadharau ujue wewe ndio unadharau. Ukimuona anakasoro yoyote ile ujue kasoro hiyo imeanzia kwako.

Hata hivyo matatizo ya mkeo utaanza kuyaona mara tuu ukishindwa kumdhibiti. Wanaume waliofanikiwa kudhibiti wake zao hawajui wala kuziona kasoro za Wake zao.

Hakuna kiumbe rahisi kukidhibiti kama Mwanamke. Mwanamke ni rahisi kumdhibiti kwa sababu ni kiumbe kinachohitaji Kupendwa "Upendo" mtu yeyote anayehitaji upendo ni rahisi kumdhibiti. Hii ni tofauti na mtu anayehitaji kuheshimiwa "Heshima" . Ni ngumu kumdhibiti mtu anayehitaji kuheshimiwa. Kwa sababu heshima inahitaji Akili (Ubongo)wakati upendo unahitaji Hisia(Moyo).

Unapoishi na mwanamke jaribu kuishi naye kwa kujua yeye sio mwanaume. Usiishi na mwanamke kwa kumchukulia yeye yupo kama wewe. Huo ndio mwanzo wa kushindwa kumdhibiti.

Mwanamke hufanya mambo kwa kukuiga wewe. Elewa kuwa chochote utakachomfanyia Mwanamke jua naye atakufanyia tuu.
Mwanamke ni kama mtoto mdogo anayejifunza kuongea. Ukisema "leta" naye atasema "eta" ukisema "Maji" naye atasema "Mma" akishajua kuzungumza kama wewe hapo ndio utapiga mayowe.

Unapomfanyia mwanamke jambo mfanyie kwa upendo ili yeye akufanyie kwa heshima.
Ni kosa la jinai kumfanyia jambo mkeo kwa heshima kwani ataanza kupata hisia kuwa unamuogopa na hiyo kwake itaanza kumfanya ajihisi hayupo safe kwako.

Kumfanyia Mwanamke jambo kwa heshima ni ile hali ya kujaribu kum-please, kumpa jambo fulani ili asikuache au asiende kwa mwingine. Na ile hali ya kujitesa kwaajili yake. Unafikiri yeye atakulipa nini? Huo sio upendo ambao wanawake wanautaka.

Elewa kuwa Mwanamke hawezi kumuacha mwanaume anayempenda. Atamvumilia kwa kila jambo. Lakini Mwanamke ni rahisi kukuacha ukiwa unamheshimu.

Ili mkeo awe na akili lazoma ajifunze kutoka kwako. Ili mkeo awe na imani lazima ajifunze kutoka kwako. Huwezi taka jambo la kihisia au kiakili au kiroho ambalo wewe mwenyewe hauna.

Mwanamke ni kama mtoto. Ili awe na furaha lazima mwanaume uwe na akili yenye furaha.

Vijana wanahangaika kutafuta pesa wakidhani ndio zitawafanya wawe na Ndoa zenye furaha lakini wanashindwa kuelewa kuwa Kitu pekee Mwanamke ambaye anakitaka kwa mwanaume ni kile ambacho hana uwezo wa kukipata ambacho ni uanaume. Unapozungumzia Uanaume unazungumzia NGUVU. Yaani Nguvu ya kiakili, kiroho, kihisia na kimwili.

Pesa hata wanawake wanaweza kuzitafuta. Tena wapo wanawake wenye pesa kuliko ukoo wenu wote. Lakini Mwanamke hata afanye nini hawezi kupata nguvu ya uanaume.

Elewa kuwa ndani ya Mwanaume kuna Mwanamke. Hiyo hata kisayansi ipo hivyo. Kwamba mwanaume ana gamate X(like) na Y(kiume) Wakati Mwanamke ana gamates X (kike) tuu. Ndio maana Mwanamke hana uwezo wa kuamua kuzaa mtoto wa kiume ila mwanaume ndiye anajua uwezo.

Ukiona Mwanamke hakuheshimu wala hakutii basi elewa kuwa wewe ndio Umeshindwa kumdhibiti Mkeo.

Elewa kuwa wakati unawaza kutafuta pesa ili umfurahishe huyo mkeo. Kuna wenzako hawana pesa na wanaishi maisha ya furaha na wake zao. Tena Wake wa zuri wa sura na maumbile.

Usije ukajitesa kutafuta pesa ukadhani ndio utaheshimika na mkeo. Thubutu! Heshima yako, heshima ya mwanaume ipo ndani yake na sio nje.
Pesa ni nzuri kwa mahitaji ya familia lakini kamwe haiwezi kumfanya mkeo akuheshimu au akupende.

Huwezi mpa mkeo mtaji wa biashara wakati wewe mwenyewe biashara huwezi kufanya. Ni rahisi sana mkeo kushindwa kitu ambacho wewe kimekushinda.
Kama wewe ni mfanyabiashara ni rahisi sana mkeo kufanya vizuri kwenye biashara kwa sababu ataiga kutoka kwako na wewe ndio utakuwa kocha wake.

Ikiwa wewe ni muajiriwa na unataka kumfungulia mkeo biashara basi itakupasa ushirikiane naye kwa kufanya biashara kwa kuanzia na mtaji mdogo mdogo huku wote mkijifunza na kupata uzoefu.

Sio mke hana uzoefu wa biashara na wewe hujawahi kufanya biashara alafu anakuomba mtaji wa milioni tano au kumi na wewe unachukua mkopo unaanzisha biashara ya milioni tano au kumi wakati hauna uzoefu.
Mpe mtaji angalu wa laki tano au milioni moja kisha fanyeni biashara huku mkisoma mchezo. Kadiri mnavyopata uzoefu ongezeni mtaji, milioni mbili, milioni tatu na nusu. Milioni tano hivyohivyo.

Elewa kuwa Mwanamke ni mtu anayependa mambo makubwa na yatokee kwa haraka au mara moja hivyo utakuwa na kazi ya kumuelewesha jinsi mambo yalivyo kiuhalisia. Kumbuka wanawake wengi wanatumia hisia kuliko uhalisia (ukweli au akili).

Hivyo usimlaumu kuwa ni mbishi. Sio ubishi bali wao ndivyo waonavyo mambo kwa kutumia hisia. Hapo ni kuifuta akili yao ifanye kazi na waone mambo kwa jicho la akili. Lazima watakuelewa.
Na sio kujibizana kama mtu usiye na Akili. Mtaishia kuvunja nyumba.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Me bandia (Wavulana): "Naoa Ke Mfanyakazi wa kusaidiana naye maisha"

Ke: "Nikiwa na kazi yangu kamwe sibabaishwi na Me yeyote kimahusiano"

Wazazi wa Ke: Someni sana Mabinti zetu ili mpate kazi msinyanyaswe na Me zenu katika ndoa"

Me halisi: "Nasimamia majukumu yote kifedha ni wajibu wangu kula kwa jasho ila Ke anizalie na kunilelea Watoto tu".

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Me halisi: " Nasimamia majukumu yote kifedha ni wajibu wangu kula kwa jasho ila Ke anizalie na kunilelea Watoto tu".

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Mparaganyiko🤣😅😭

DEFINITION OF MPARAGANYO​

Swahili definitions powered by Oxford Languages
mparaganyo/mparagaɲɔ/nominoWord forms: miparaganyo (plural)

Ngeli za nomino: u-, i-hali ya kuvurugika kwa mambo, vitu kuwa mchafukoge
 
Tunahangaika sana kufikiria kuhusu wanawake, wakati kuna mambo mengi ya msingi ya kufikiria.
 
True, uko sawa.

Ingawa Si Kila mume ameoa mke sahihi.

Ubavu, ndo kivuli ulichozungumzia, ukioa asie ubavu wako, KAZI unayo.
 
MKEO NI KIVULI CHAKO. CHOCHOTE UTAKACHOFANYA AU UNACHOTAKA AFANYE ATAFANYA. AKIKUSUMBUA UJUE WEWE NDIO MSUMBUFU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mkeo ukimuona hana akili ujue wewe ndio huna akili. Ukimuona anadharau ujue wewe ndio unadharau. Ukimuona anakasoro yoyote ile ujue kasoro hiyo imeanzia kwako.

Hata hivyo matatizo ya mkeo utaanza kuyaona mara tuu ukishindwa kumdhibiti. Wanaume waliofanikiwa kudhibiti wake zao hawajui wala kuziona kasoro za Wake zao.

Hakuna kiumbe rahisi kukidhibiti kama Mwanamke. Mwanamke ni rahisi kumdhibiti kwa sababu ni kiumbe kinachohitaji Kupendwa "Upendo" mtu yeyote anayehitaji upendo ni rahisi kumdhibiti. Hii ni tofauti na mtu anayehitaji kuheshimiwa "Heshima" . Ni ngumu kumdhibiti mtu anayehitaji kuheshimiwa. Kwa sababu heshima inahitaji Akili (Ubongo)wakati upendo unahitaji Hisia(Moyo).

Unapoishi na mwanamke jaribu kuishi naye kwa kujua yeye sio mwanaume. Usiishi na mwanamke kwa kumchukulia yeye yupo kama wewe. Huo ndio mwanzo wa kushindwa kumdhibiti.

Mwanamke hufanya mambo kwa kukuiga wewe. Elewa kuwa chochote utakachomfanyia Mwanamke jua naye atakufanyia tuu.
Mwanamke ni kama mtoto mdogo anayejifunza kuongea. Ukisema "leta" naye atasema "eta" ukisema "Maji" naye atasema "Mma" akishajua kuzungumza kama wewe hapo ndio utapiga mayowe.

Unapomfanyia mwanamke jambo mfanyie kwa upendo ili yeye akufanyie kwa heshima.
Ni kosa la jinai kumfanyia jambo mkeo kwa heshima kwani ataanza kupata hisia kuwa unamuogopa na hiyo kwake itaanza kumfanya ajihisi hayupo safe kwako.

Kumfanyia Mwanamke jambo kwa heshima ni ile hali ya kujaribu kum-please, kumpa jambo fulani ili asikuache au asiende kwa mwingine. Na ile hali ya kujitesa kwaajili yake. Unafikiri yeye atakulipa nini? Huo sio upendo ambao wanawake wanautaka.

Elewa kuwa Mwanamke hawezi kumuacha mwanaume anayempenda. Atamvumilia kwa kila jambo. Lakini Mwanamke ni rahisi kukuacha ukiwa unamheshimu.

Ili mkeo awe na akili lazoma ajifunze kutoka kwako. Ili mkeo awe na imani lazima ajifunze kutoka kwako. Huwezi taka jambo la kihisia au kiakili au kiroho ambalo wewe mwenyewe hauna.

Mwanamke ni kama mtoto. Ili awe na furaha lazima mwanaume uwe na akili yenye furaha.

Vijana wanahangaika kutafuta pesa wakidhani ndio zitawafanya wawe na Ndoa zenye furaha lakini wanashindwa kuelewa kuwa Kitu pekee Mwanamke ambaye anakitaka kwa mwanaume ni kile ambacho hana uwezo wa kukipata ambacho ni uanaume. Unapozungumzia Uanaume unazungumzia NGUVU. Yaani Nguvu ya kiakili, kiroho, kihisia na kimwili.

Pesa hata wanawake wanaweza kuzitafuta. Tena wapo wanawake wenye pesa kuliko ukoo wenu wote. Lakini Mwanamke hata afanye nini hawezi kupata nguvu ya uanaume.

Elewa kuwa ndani ya Mwanaume kuna Mwanamke. Hiyo hata kisayansi ipo hivyo. Kwamba mwanaume ana gamate X(like) na Y(kiume) Wakati Mwanamke ana gamates X (kike) tuu. Ndio maana Mwanamke hana uwezo wa kuamua kuzaa mtoto wa kiume ila mwanaume ndiye anajua uwezo.

Ukiona Mwanamke hakuheshimu wala hakutii basi elewa kuwa wewe ndio Umeshindwa kumdhibiti Mkeo.

Elewa kuwa wakati unawaza kutafuta pesa ili umfurahishe huyo mkeo. Kuna wenzako hawana pesa na wanaishi maisha ya furaha na wake zao. Tena Wake wa zuri wa sura na maumbile.

Usije ukajitesa kutafuta pesa ukadhani ndio utaheshimika na mkeo. Thubutu! Heshima yako, heshima ya mwanaume ipo ndani yake na sio nje.
Pesa ni nzuri kwa mahitaji ya familia lakini kamwe haiwezi kumfanya mkeo akuheshimu au akupende.

Huwezi mpa mkeo mtaji wa biashara wakati wewe mwenyewe biashara huwezi kufanya. Ni rahisi sana mkeo kushindwa kitu ambacho wewe kimekushinda.
Kama wewe ni mfanyabiashara ni rahisi sana mkeo kufanya vizuri kwenye biashara kwa sababu ataiga kutoka kwako na wewe ndio utakuwa kocha wake.

Ikiwa wewe ni muajiriwa na unataka kumfungulia mkeo biashara basi itakupasa ushirikiane naye kwa kufanya biashara kwa kuanzia na mtaji mdogo mdogo huku wote mkijifunza na kupata uzoefu.

Sio mke hana uzoefu wa biashara na wewe hujawahi kufanya biashara alafu anakuomba mtaji wa milioni tano au kumi na wewe unachukua mkopo unaanzisha biashara ya milioni tano au kumi wakati hauna uzoefu.
Mpe mtaji angalu wa laki tano au milioni moja kisha fanyeni biashara huku mkisoma mchezo. Kadiri mnavyopata uzoefu ongezeni mtaji, milioni mbili, milioni tatu na nusu. Milioni tano hivyohivyo.

Elewa kuwa Mwanamke ni mtu anayependa mambo makubwa na yatokee kwa haraka au mara moja hivyo utakuwa na kazi ya kumuelewesha jinsi mambo yalivyo kiuhalisia. Kumbuka wanawake wengi wanatumia hisia kuliko uhalisia (ukweli au akili).

Hivyo usimlaumu kuwa ni mbishi. Sio ubishi bali wao ndivyo waonavyo mambo kwa kutumia hisia. Hapo ni kuifuta akili yao ifanye kazi na waone mambo kwa jicho la akili. Lazima watakuelewa.
Na sio kujibizana kama mtu usiye na Akili. Mtaishia kuvunja nyumba.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
naam swadakta
 
Me bandia (Wavulana): "Naoa Ke Mfanyakazi wa kusaidiana naye maisha"

Ke: "Nikiwa na kazi yangu kamwe sibabaishwi na Me yeyote kimahusiano"

Wazazi wa Ke: Someni sana Mabinti zetu ili mpate kazi msinyanyaswe na Me zenu katika ndoa"

Me halisi: "Nasimamia majukumu yote kifedha ni wajibu wangu kula kwa jasho ila Ke anizalie na kunilelea Watoto tu".

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
sasa vimarioo vya Tandika kama haka Robert Heriel Mtibeli kanakesha hapa jf kuhubiri "maisha kusaidiana" ati wanaume waoe wanawake wenye ajira ili wasaidiwe maisha !!

mwanaume mwenye hii mindset ni dhaifu na wengi wamelelewa na masingle mother (which am whole heartlly haka ka Hariel kamelelewa na single mom kwa hakika)
 
Back
Top Bottom