Mkenya kaniuliza swali!

Mkenya kaniuliza swali!

Msiwe waoga kusikia neno Mkenya tu mnaanz akuseme maneno mengi bila kujiuliza maswali ya msingi kuwa mtoa hoja na alikutana na Mkenya wa kada (level) ipi ya maisha,yeye alichojali ni Ukenya tu, inawezekana alikutana na Menya ambaye ni tingo wa gari la mizigo toka Nyawahita ama Katito alikuwa mtu wa mtaani tu ila kama zali kapata nafasi katika kampuni ya Trans East Africa so ukimuuliza kuhusu mambo ya dunia nadhani ni rahis yeye kutojua.
Sasa jiulize kama huyo Mkenya kama anayajua haya;
1.Wakati unatuma hii Thread yako rais wa Mwai Kibaki alikuwa hapa nchini ziara ya siku mbili,Je Mkenya analijua hilo?
2.Mwaka 2007 wakati wa uchaguzi mkuu wa Kenya,Kibaki alionekana dhahiri kupoteza nafasi yake ya urais aliyokuwa anaantetea hivyo kuwa na mgogoro kati yake yeye KIBAKI NA ODINGA,sawa je,huyo Mkenya anawakumbuka walioenda KUSULUHISHA mgogoro huo,na walienda kwa sifa zipi.
NISEME MACHACHE,MAANA SIJUI HATA KAMA AKIWA MFUATILIAJI WA HABARI KUPITIA VYOMBO VYA HABARI KAMA BBC-SWAHILI ANAWEZA KUELEMIKA ZAIDI,HATA HUYU MWANDISHI WA HII THREAD PIA
 
nilichokielewa mimi kiukweli wenzetu wapo bize na vyakwao na sio kufuatilia vya wenzao na ndio maana nchi yao inaendelea maana wapo bize kuijenga nchi yao na sio kuwa wambea na msitari wa mbele kufuatilia ya wengine kama Tanzania. mfano angalia rais wetu atavyokuwa wakwanza kutoa pongez au pole kwa nchi nyingine unaweza kukuta hata mawaziri wa nchi hiyo taarifa walikuwa hawajapata vizuri. sisi watanzania ni wajinja sana kiukweli yetu yanatushinda kazi kuangalia vya wenzenu na sio tunajifunza kupitia wao hapana isipokuwa tunapenda kuwa vimbele mbele waache wakenya watushangae tunavyojua kuusiana na wao na ndio maana uchumi wao unakwenda juu maana wapo bize kufanya yao sisi tupo bize kuwaangalia wao na sio kuiga
 
Nilikuwa naongea na jamaa mmoja Mkenya, kama kawaida mambo ya siasa yakaanza na Uchaguzi, jamaa akaniuliza ''It seems you people you know alot about Kenyan politics, how come i dont know anything about Tanzanian politics?'' nikakosa jibu, sijui wewe ungemjibu vipi yule jamaa?
safi sana

inaonekana ulikua na kimbelembele sana kujifanya unajua mambo ya kenya kuliko ya kwenu
 
Nilikuwa naongea na jamaa mmoja Mkenya, kama kawaida mambo ya siasa yakaanza na Uchaguzi, jamaa akaniuliza ''It seems you people you know alot about Kenyan politics, how come i dont know anything about Tanzanian politics?'' nikakosa jibu, sijui wewe ungemjibu vipi yule jamaa?

Ulishawahi ona au sikia mfano the Citizen tv wanakipengele cha za EA kwenye taarifa zao za habri?

Cha ajabu tv zote za tz zinakipengele hicho, sijui ni kukosa ubunifu au kujipendekeza
Citizentv walirusha habari moja tu ya tz tokea kuanzishwa, nayo ni ile ya babu wa Loliondo.
Hata hii ya mauwaji ya padre, hawajui,.
 
Jibu liko papa hapa, asilimia sabini na tano ya waliojibu hapa wana hiki au kile kuhusu uchaguzi uliopita wa 2007, so much for being progressive.
Mimi hufuatilia sana yanayojiri nchini tz ukinilinganisha na wakenya wenzangu wala ila kujua kuna ccm na chadema Tanzania hayo mengine siyafahamu maana hayanihusu,zeluzelu akinyofolewa mkono humo huwa nasikitika kama nyinyi lakini sina ufuatilizi wa hilo jambo maana halinihusu na niko na imani mtalitatua kiungwana.
Basically there is a tendency of trying to hold Kenyans down on whatever they do amongst you that you fast and pray that Kenya fcks up big-time thats why you will see so much unwarranted advice on how we should shun tribalism in our politics yet we know you guys face an equal task of religious intolerance but its not in our lingo to dwell on it.
 
Kijakazi, yaani ulishindwa hata kumwambia kuwa "SISI RAISI WETU NI HANDSOME BOY, anaendaga ulaya kila siku, anapiga picha na masupa staa, na Obama anamshobokea"?

Au angemjibu kisiasa tu kwamba Tanzania hatuna kesi The Hague ndio maana hawezi kutusikia sana ila juhudi ziko mbioni na kwa kuanzia tu , tumeipa barabara ya old bagamoyo jina jipya la kibaki ili kueneza siasa za Tz kenya. Hutakiwi kukosa jibu la kisiasa bwana....
 
safi sana

inaonekana ulikua na kimbelembele sana kujifanya unajua mambo ya kenya kuliko ya kwenu

Kweli kabisa ni kimbelembele tu, lakini utakiepuka vpi kama kila bar unayoingia hukuti wanaonyesha ITV bali ni Citizen ya Kenya, tembelea nyumba nyingi TZ utakuta watu wanaangalia TV za Kenya, wakati ukiwa Kenya hakuna mtu hata mmoja anayewaza, achilia mbali kujua tu hata jina la kituo chochote cha TV cha Tanzania!
Achana na hayo Nairobi kuna Nyerere road, mimi naijua, lkn ni ndogo sana na wala sio muhimu hata ukiwauliza Wakenya wengi kama hawaishi huo mtaa hawaijui, angalia sisi nani asiyeijua Kenyata drive, na sasa Mwai kibaki Road inakwenda zaidi ya km 10, Nyerere rd Nairobi haifiki hata km 3! Kwa hiyo uko sawa ni kimbelembele lkn ndio hivyo!
 
Nilikuwa naongea na jamaa mmoja Mkenya, kama kawaida mambo ya siasa yakaanza na Uchaguzi, jamaa akaniuliza ''It seems you people you know alot about Kenyan politics, how come i dont know anything about Tanzanian politics?'' nikakosa jibu, sijui wewe ungemjibu vipi yule jamaa?

Manyang.au hao achana nao
 
Back
Top Bottom