Mke wangu ni mgumu sana kujishusha

Mke wangu ni mgumu sana kujishusha

Kaka umechapia umesema Shula tu badala ya shuka tula. Unatuchanganya sie wapare Shula tu maana yake Jamba tu[emoji23][emoji23]

Pamoja na kuwa na Baba na Mama mpare nachojua ni erehoa tu, Mlamua, na mcheku.
 
📌📌📌📌📌📌📌📌

Huwa hawataki ujinga ujinga. Yaani ni bandika bandua kampa kampa kama huna kifua utakimbia au utapata presha ni ego tu kwa kwenda mbele. Ku-deal nao sawasawa ni lazima kujitoa ufahamu na wewe uwe mtu usiyejali vinginevyo presha ya kupanda inakuhusu 😁😁😁
😂😂😂😂 kumbe unawajua vyedi mkuu!. Hivyo hivyooooo
 
Wakuu nawasalimu kwa jina la muungano.

Niende moja kwa moja kwenye mada kuu, nimekua kwenye ndoa na huyu mke wangu yapata miaka nane sasa, tulioana wote tukiwa vijana na ni binti ambae tulisoma nae kuanzia primary tukaja kukutana chuo, kwahiyo namfahamu vizuri tu. Nikiri tu kwenye mambo mengine ya kifamilia yupo vizuri sana, ila tatizo linaanza ni kujishusha na kuomba msamaha pale tunapotibuana.

Hii hali inanikwaza sana sababu bila kujishusha mimi tunaeza kukaa hadi mwezi hatuongei eti ameninunia. Mara nyingi huwa inanilazimu mimi kujishusha baada ya kubanwa na upwiru sana. Kwa ninavofahamu kupishana kauli kwenye ndoa kupo na ni jukumu la wanandoa wote kuipambania ndoa kwa kujishusha na kuyaongea, ila mwanamke ndio anatakiwa awe mstari wa mbele kujishusha ili mambo yaende, ila kwa huyu mke wangu imekua tofauti.

Kwa sasa tuna watoto watatu ila hii hali inanifanya nihisi kama nalazimisha mapenzi hivi hadi nimeanza kupata mawazo ya kuivunja hii ndoa. Nakwazika sana.

Naombeni ushauri wenu wakuu.
Jishushe wewe ndio uwe Mke wake 😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom