Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

The MaskmaN

JF-Expert Member
Sep 28, 2017
350
753
Habari wana JF

Mimi ndugu yenu nina makubwa ambayo yamenifika na sijui nitayatatua vipi?

Nina mke wangu nilimuoa mwaka 2015, baada ya kuishi nae miaka kama 7 sasa kuna siku juzi nipo kazini nikapokea simu kutoka kwa mdada wa kazi pale nyumbani akinitaka nirudi haraka nyumbani, bila kusita nikafanya hivyo baada ya kama lisaa nikawa nishafika nyumbani, nikamkuta mke wangu kakaa chini sebuleni kama analia afu mdada wa kazi kasimama. Nikamuuliza mdada kuna nini hapa akaniambia naona kama dada kapandisha mashetani!! Ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona mtu au mke wangu kapandisha mashetani, yakawa yanalia kwa sauti kubwa mnoo huku anajipiga piga chini.

Baada ya dakika 4 za kulia yakanitaka tuanze mazungumzo ila kwa sharti yule mdada wa kazi ama mie nimshike sikio mke wangu "kiti" kwa lugha yao. Kupitia mdomo wa mke wangu yale majini/mashetani yakasema kuwa yamekuwa yakipambana na MCHAWI kwa takribani mwaka sasa ila leo yameona vita inataka kuwashinda hivyo kiti "mke" anaweza akazidiwa na kupoteza maisha.

Nikawauliza huyo mchawi wamemuona wapi au anatokea wapi? Yule jini akaniambia je unatuamini? Au hautuamini? Kulingana na shauku ya kutaka kujua hilo tatizo linalotaka kuchukua maisha ya mke wangu ikanibidi niombe kutajiwa kwa kujibu "ndio nawaamini" Basi yule jini aliyepo kwa mkewe wangu akaniambia bila hata kupepesa macho kuwa "Mchawi ni bi fulani" ambaye ni mama yangu mzazi kabisaaa. Nilishtuka sana kiasi kwamba nilitamani hata kuchapa fimbo wote waliokuwepo palee ila nikajikaza na kuacha lipite. Basi hiyo siku ikapita.

Baada ya siku kama 3 nikapokea simu kutoka nyumbani kwa wazazi wangu, nikaenda bila kusita kufika tu baada ya mama kuniona akaangua kilio na kunikumbatia kwa huzuni. Ikabidi nimuulize mama kulikoni? Kuna tatizo? Au kuna msiba? Akasema hapana kuna jambo nimekuwa namuhadithia baba yako kila siku hivyo na wewe yakupasa kulijua leo. Nikamwambia sawa mama niambie...basi akaanza kusema "ujue mwanangu mie mama yako huwa nina karama kama sio bahati fulani kichwani mwangu toka nikiwa binti mdogo tu, nina uwezo wa kuona na kuzungumza na vitu/viumbe ambavyo wewe kwa jicho lako hilo la nyama huwezi kuona"....baada ya maelezo mengi tu ya historia na nguvu zake hizo ndipo mama bila kusita akasema "Mwanangu mkeo ni MCHAWI" kama utakubali sema nikupe dawa ambayo itakusaidia kumuona bila yeye kujua ili ikusaidie kusadiki haya ninayo yasema na badae uchukue hatua...

Basi nikarudi nyumbani nikiwa na mawazo mengi nisijue nini kinaendelea hapa katikati. Nikafika nyumbani ile kuingia tu mke akaanza kupiga kelele kama jogoo huku akinifuata kwa hasira na kuniomba nimpe nilichopewa na huko nilipotoka. Nikashtuka mnoo!!

Ikabidi niitoe ile dawa na kumkabidhi mke wangu, baada ya dakika 3 akaniambia sasa achana na hii dawa ngoja nikupe ya kwangu ili ushuhudie mama yako anachotufanyia usiku.

Nikamwambia kwa sasa hapana ngoja nifikirie then nitakuambia unipe...

Ndugu zangu nipo hapa Sea clif napata upepo nikitafakari nini kinaendelea kwenye familia yangu haswaa kwa watu ninaowapenda mnoo. Je yupi ni yupi?

Nipeni ufumbuzi.
 
Kama stori yako ni ya kweli, hapo wote wachawi hao...

Mama yako kakiri kuwa na 'karama ya kuona' watu wabaya, halafu kakupa nawe dawa ili uweze ona mauzazuza ya mkeo, kuwa na karama haina maana unakuwa na uwezo wa kutengeneza dawa...kama anatengeneza dawa huyo ni fundi tayari

Pia kwa mkeo ni wale wale tu, ana uchawi wa maruhani, na kitendo cha yeye kukupa dawa ina maana na yeye ni fundi...

Nina swali moja, kama mama yako ana karama ya kuona mauzauza, iweje hakuona kabla mwanamke uliyenaye hajawa mkeo?
 
Habari wana JF

Mimi ndugu yenu nina makubwa ambayo yamenifika na sijui nitayatatua vipi?

Nina mke wangu nilimuoa mwaka 2015,baada ya kuishi nae miaka kama mi 7 sasa kuna siku juzi nipo kazini nikapokea simu kutoka kwa mdada wa kazi pale nyumbani akinitaka nirudi haraka nyumbani, bila kusita nikafanya hivyo baada ya kama lisaa nikawa nishafika nyumbani,nikamkuta mke wangu kakaa chini sebuleni kama analia afu mdada wa kazi kasimama...nikamuuliza mdada kuna nini hapa akaniambia naona kama dada kapandisha
Waite wote wawili nyumbani kwako, sokota fimbo ya ufito mwembamba, chapa wote hadi waombe poo!
Hayo madudu bai bai!
 
Habari wana JF

Mimi ndugu yenu nina makubwa ambayo yamenifika na sijui nitayatatua vipi?

Nina mke wangu nilimuoa mwaka 2015,baada ya kuishi nae miaka kama mi 7 sasa kuna siku juzi nipo kazini nikapokea simu kutoka kwa mdada wa kazi pale nyumbani akinitaka nirudi haraka nyumbani, bila kusita nikafanya hivyo baada ya kama lisaa nikawa nishafika nyumbani,nikamkuta mke wangu
MKEO NI MCHAWI.
Hata kama mama ni mchawi hana madhara kwako, tangu upo tumboni hadi. leo hii, angetaka kukuua mbona angekumaliza mapema sana?

mwisho kabisa,
Ingia kwenye maombi na ukitaka msaada wa maombezi karibu PM yangu. Bure kabisaa
 
Hii kitaalamu tunaita Double Chance.

Kiboko wakutanishe wazipige tu
 
MKEO NI MCHAWI.
Hata kama mama ni mchawi hana madhara kwako, tangu upo tumboni hadi. leo hii, angetaka kukuua mbona angekumaliza mapema sana?

mwisho kabisa,
Ingia kwenye maombi na ukitaka msaada wa maombezi karibu PM yangu. Bure kabisaa
Ndio mama hana madhara kwangu ila mke ananiambia kuwa anataka kuchukua uhai wake hivi karibuni!..
 
Kama stori yako ni ya kweli, hapo wote wachawi hapo...

Mama yako kakiri kuwa na 'karama ya kuona' watu wabaya, halafu kakupa nawe dawa ili uweze ona mauzazuza ya mkeo, kuwa na karama haina maana unakuwa na uwezo wa kutengeneza dawa...kama anatengeneza dawa huyo ni fundi tayari

Pia kwa mkeo ni wale wale tu, ana uchawi wa maruhani, na kitendo cha yeye kukupa dawa ina maana na yeye ni fundi...

Nina swali moja, kama mama yako ana karama ya kuona mauzauza, iweje hakuona kabla mwanamke uliyenaye hajawa mkeo?
Asante mkuu, ila yeye hakusema kama anaweza kuona ya mbeleni bali ana uwezo wa kuona mauza uza ndivyo nilivyo muelewa
 
Habari wana JF

Mimi ndugu yenu nina makubwa ambayo yamenifika na sijui nitayatatua vipi?

Nina mke wangu nilimuoa mwaka 2015,baada ya kuishi nae miaka kama mi 7 sasa kuna siku juzi nipo kazini nikapokea simu kutoka kwa mdada wa kazi pale nyumbani akinitaka nirudi haraka nyumbani, bila kusita nikafanya hivyo baada ya kama lisaa nikawa nishafika nyumbani,nikamkuta mke wangu kakaa
Itakua wamejuana kwa muda mrefu katika tasnia ya kuwanga sema sasa kuna mmoja ni mzoefu/mjuzi kuliko mwenzake sasa wana kitu kama maslahi hivi wanapigania usijetolewa kafara wewe..ila mama yako nae ni noma aisehhhh
 
weee achana nao kaka sema wapende wote tu na uchaw wao ila kwa navyskia majin ayapendan na wachawi ... tengeneza mazingira ya kuish nao ivo ivo
Sasa mchawi nani na mwenye jini ni nani?..pia kumeisha ingia viapo vya kutaka kutoana uhai
 
Back
Top Bottom