Mke wangu kaniletea shoga yake nitembee naye!

Mke wangu kaniletea shoga yake nitembee naye!

hapa mwanaume ana kosa gani jamani?

mwanaume unakubalije mkeo anakuletea upuuzi wa aina hii nyumbani kwako!
eti nakuletea shogangu akuhudumie wewe na familia!na we dume zima unakubali tu!unapikiwa unamkuta mtu kwenye sebule yako unachekelea tu!
mkeo anafanya ujinga ujinga usoeleweka unanyamaza tu!ah! mi sipendi hii aina ya mwanaume bana!
mimi nikiwa poyoyo hivi si unitreat accordingly ,KIUME!sio unanichekea tu!
 
Nimejikuta tu na'like' thread aisee..kwani wewe huoni hapo jamaa hana makosa..we men we're WEAK..

eti we men are weak!
ndo naruhusu wake wanawaendesha namna hii!
mi sitaki mwanaume wa kunichekea kiasi hiki!lol!
nafanyaje huu ujinga na shem wako achekelee tu eti namletea msaidizi!
kwani mi nimekuwa yesu!kumbaf!
 
Biblia inasema aziniye na mwanamke hana akili kabisa. Ndugu yangu nawe wataka kuwa mmojawapo wasiokuwa na akili? Naomba usome Mithali 5 yote,natamani kuongeza kitu lakini nakuomba uisome between line itakusaidia sana. Pili taka kiuhalisia kujua hiyo NGO ya mke wako siku anakuaga mwambie leo nataka nikupeleke ukiona anakuwa mkali m'mbane zaidi kwann hataki ujue.Zungumza na mkeo onesha hisia zako jins gani anavyokupa wakati mgumu na ikibidi mueleze ukweli, ukweli utakuweka huru na utakusaidia sana kuachana na huyo shogaake kama kweli unataka kuiacha dhambi hii. Tubu dhambi yako anza kwa upya 2013 na muilinde ndoa yenu until death, baba ulipoapa kwa shida na raha,ktk huzuni ama furaha,uzima ama ugonjwa sasa shida zenyewe,huzun na ugonjwa ndo hizi unatakiwa uzishinde,unakumbuka pia ulisema nitawaepuka wengine wote nitaambatana na ww tu!
 
Kama kweli kama umetunga leta nichangie wanawake bwana wapo very smart huyo mkeo anajua analolifanya na huyo rafiki ye lao moja hapo mjinga wewe.
Huyo rafiki wa mkeo ndo kuwadi wa mke wako na mke wako anatembea na jiboss limoja sasa kukuzuga inabidi shost atembee na wewe.
Muhimu hapo we mjaze mimba rafiki ya mke wako baaaaaas.
Maana wewe utakuwa umewapiku.
Mchana mwema
 
MM kwa upande wangu , NAKUOMBA SIKU ATAKAYOKWAMBIA ANASAFIRI MFUATILIE WEWE MWENYEWE AU MPE MTU KAZI YA KUMFUATILIA ILI AKULETEE MAJIBU YALIYO SAWIA, KWA SABABU SISI WANAWAKE TUNA WIVU SANA , HAIWEZEKANI AMTUME SHOGAYE KWAKO , IHALI ANAJUA KILA KITU KINACHOWEZA TOKEA.
 
eti we men are weak!
ndo naruhusu wake wanawaendesha namna hii!
mi sitaki mwanaume wa kunichekea kiasi hiki!lol!
nafanyaje huu ujinga na shem wako achekelee tu eti namletea msaidizi!
kwani mi nimekuwa yesu!kumbaf!

Huyu ni kilaza...in and out
 
mkeo analiwa!
Kisha kakuletea shosti wake umle!

Dawa muoe shosti awe mke mdogo,maana mkeo kesharidhia
 
Kwa kweli dunia hadaa!Sitaki kumuhisi mkeo vibaya lakini huenda na wewe ni kiwembe akaamua kuliko ugegede huku na huko afadhali umgegede rafiki yake.
Tafakari, dushelele for your wife unaigawa kwa shosti!vibaya hivyo.
 
Mke wangu amejiunga na VICOBA na pia NGO moja ya mambo ya kuwawezesha wanawake kibisahara. Amekuwa akisafiri mara kwa mara kwenda mikoani kwenye semina za hiyo NGO yao. Nimekuwa nikilalamika sana kuhusu hiyo tabia yake mpaka tukapelekana kwa wazazi na akaahidi hatosafiri tena.

Miezi miwili iliyopita amenijulisha kwamba amepewa cheo kwenye NGO yao na atalazimika kusafiri sana hivyo kuna shoga yake ndiye atakuja kunipikia na kulala hapo nyumbani kila akisafiri ili kunihudumia mimi na watoto. Nilipinga sana wazo lake lakini akasema hawezi kuacha kusafiri kwa sababu anapata marupurupu kwa ustawi wa familia jambo ambalo si kweli maana tangu ajiunge na hiyo NGO sijaona lolote la maana zaidi ya mavazi ya gharama anayojinunulia.

Tatizo hataki hata siku moja nitembelee NGO yao wala nisafiri naye, mie ni mtumishi serikalini, lakini siwezi kunyimwa hata ruhusa ya wiki moja ili nisafiri naye.
Mabishano yetu hayakupata muafaka na matokeo yake siku aliposafiri, shoga yake akaja pale nyumbani na kufanya shughuli zote zipaswazo kufanyw ana mke na niliporudi usiku nilimkuta sebuleni akinisubiri. Aliniandalia maji ya kuoga na kisha chakula na wakati nakula alikuwa amekaa pale sebuleni akiangalia TV huku tukizungumza.

Tuliishi hivyo kwa wiki nzima hadi mke wangu akarudi na yule shoga yake aliondoka na kurudi kwake. (Huyu dada hajaolewa ila amezaa na jamaa flani huko kwao Songea na mtoto yuko kwa wazazi wake. Hapa mjini anaishi peke yake akijishughulisha na biashara ya kukopesha nguo za kike). Mke wangu aliniuliza kama shoga yake hakumuangusha, yaani alikuwa anaihudumia familia vizuri, nikamjibu kwamba hakuwa na tatizo.

Wiki mbili baadaye mke wangu akaaga anasafiri tena kwenda Dodoma kwenye semina na atakaa kule kwa wiki mbili, hivyo shoga yake atakuja tena kukaa pale nyumbani hadi atakaporudi. Sasa wiki moja tangu mke wangu aondoke tuliishi vizuri tu, lakini wiki ya pili huyu bibie kaanza kunitega na kama mjuavyo wanawake wako smart sana, nilijitahidi sana kukwepa mitego, lakini sikufua dafu, akanidaka tena ilikuwa sebuleni watoto wote walikuwa wamelala.

Naomba nikiri kwamba huyu mwanamke alikuwa ni hodari kweli kweli maana nadhani alikuwa anajua ninachokikosa kwa mke wangu. Tangu siku hiyo alikuwa analala chumbani kwangu mpaka alfajiri ndio anarudi chumbani kwake.
Mke wangu aliporudi nilisikitika sana, maana nilitamani asafiri tena, kutokana na kunogewa na penzi la shoga yake. Hivi sasa tumeendea kukutana mara kwa mara maeneo ya mbali na huyu shoga wa mke wangu na kwa kweli ameniteka kabisa yaani namuwaza wakati wote na nimejikuta nikiwa simtamani mke wangu kabisa.

Lakini cha kushangaza mke wangu wala hajanishitukia na amekuwa akimuamini sana shoga yake kupita kiasi na siku hizi huwa anasafiri mara kwa mara tena huwa anakaa wiki mbili kila akisafiri na huyo shoga yake ndio kawa kama mke wangu, yaani kama dini yangu ingekuwa inaniruhusu ningemuoa awe mke wa pili.

Hebu wana JF niambieni, hivi mke wangu akijua atanilaumu kweli?

Mmebadilishana , umepewa wa kumla naye analiwa huko safarini
 
Mkuu kwa kuwa umepata Kandarasi endelea lakini ujue Mkeo nae kama unavyofanya nae wajanja wanampuliza.Kama umejua hiyo Ngo haina msaada mbona akirudi unampokea vema . Wote ninyi ni wajanja wajanja mmechokana kila mmoja anatafuta sababu kwa mwenzake. Mmefungua mwaka vzr kumbukeni kinga maana ukimwi upo.
 
Tegelezeni umznye aho wadantwa mbwawe!!!! Yaani ni simple trick wala haihitaji msuli kujua nini kinaendelea. Kwa ufupi mkeo ana bwana mwingine ambaye ndiye anayetanua naye. Kama angekuwa mkweli asingekukataza wewe kusafiri naye. Kuhusu huyo shoga yake ni kwamba wamepanga wao wenyewe na siyo kama bahati mbaya. Hivyo mkeo akijua wala hatakuwa na noma maana yeye kaanza muda mrefu ila kakuonea huruma unaumia bure ngoja akuletee shosti wake uwe unajipooza.
 
Last edited by a moderator:
sasa dini yako imekuruhusu kufanya hilo
ulifanyalo na huyo bibie imeshindwa vipi
kukuruhusu kumfanya mkeo wa pili?

Hiyo dini yako mbona ina makengeza...........
 
Eroo mkeo anagegedwa huko safarini, na huyo shoga wake anajua mchongo mzima ndomaana kapata ujasiri wa kukutegega na kukunasa kama broiler.
Ushauri chunguza udhaifu wa shoga yake kwenye mapenzi na umtege nao atakupa mkanda mzima wa mkeo, hakika ukimkamata vizuri atakumwagia yote....nb wakati unamuoji onja chumvi kama imekolea mtoni,,
Na inavyooneka wife wako kakukamata masikio kinoma!! yaani hata kwenye hiyo NGO anayofanya kazi ataki ufike? je umeolewa au umeoa???
 
Back
Top Bottom