Mke wangu kachachamaa anataka tuachane!

Mke wangu kachachamaa anataka tuachane!

Kwa hiyo umetamani mabaki ya hilo gari na mali nyingine ndio maana unajifanya umeshikilia mila!! loooo hebu uwe na haya kidume wewe! Unaonekana wazi huna upendo zaidi ya kutamani vya kaka yako, nyie ndio mnaowatamanigi shemeji zenu!

Acha bana, endelea kumtunza mke wa marehemu na watoto wake na umuheshimu kama shemeji; USIMRITHI na kumfanya mkeo.
Mkuu kama ni hali nzuri kiuchumi mimi ninao zaidi ya huyo kaka yangu ambaye alikuwa ameajiriwa tu na hakuwahi kumiliki gari.
Mke wa marehemu mwenyewe ndio amenichagua nimrithi sasa tatizo liko wapi?
 
Kuna kijana namfahamu yeye alimlea Mke wa marehemu rafiki yake ambae alikuwa mjamzito, alijifungua na jamaa akalea mtoto na mama yake na akamsomesha mtoto hadi leo hii jamaa ana mke wake na huyo mke wa mareheu rafiki yake alishaolewa kitambo na amini usiamini jamaa hakuwahi tembea na huyo dada hata siku mojs!Kumbuka alikuwa mke wa rafiki tu, sasa wewe kaka yako!!!!!!!!!!!!Ebu acha uhuni bwana
Sasa si ushasema alikuwa ni ke wa rafiki yake
Hiyo ni kesi tofauti ukifananisha na ya kwangu ni kama vile unanionea, mila zetu hazisemi tuwarithi wake wa marafiki zetu bali wake wa kaka au wadogo zetu tumbo moja.
Je huoni tofauti hapo?
 
Cheeeee!!!Yaani izo mila potofu bado ipo!! Ebu acha ujinga wewe. Mpeni huyo mwanamke uhuru wa kuamua aolewe na nani na ivi hujui kuwa ni matusi kumuoa mke wa kakao?Na vipi kuhusu magonjwa!!! Lol!!Ebu badilikeni bwana
Huyo mke wa kaka yangu kanichagua mwenyewe kwa hiyari yake bila shuruti kuwa mimi nimrithi awe mke wangu.
tatizo ni mke wangu hataki kuwa na mwenzie.
 
Eti ni kwa sababu kikao cha ukoo kilichokaa juzi kimeamua nimrithi mke wa marehemu kaka yangu aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Kwa mila na desturi zetu inaruhusu mdogo mtu au kaka mtu kumrithi mke wa ndugu yake pale anapofariki. Sasa namshangaa mke wangu kanuna wiki sasa anataka talaka yake aondoke.

Hivi hapa nimechanganyikiwa sijui nifanye nini maana mke wangu nampenda lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee. Lazima mila iheshimiwe...

Yaani kweli hizi mila potofu bado ziko kwa makabila!! Piga marufuku mila za kurithi wajane na Nyumba Ntobo!! Huku ndiko kusambaza VVU? Hata ningekuwa mimi kwa hali ya maisha ilivyo na mtandao wa VVU nisingekubali. Wanawake wanaonewa sana. Huyo mjane ana haki ya kumua kuolewa na mwanaume amtakaye na mke wako anapaswa kuishi kwa maadili ya ndoa mliyo kubaliana.
 
Huyo mke wa kaka yangu kanichagua mwenyewe kwa hiyari yake bila shuruti kuwa mimi nimrithi awe mke wangu.
tatizo ni mke wangu hataki kuwa na mwenzie.

Kwa hiyo kwa vile kakuchagua mwenyewe wewe huna uwezo wa kukataa?For the sake of your wife as you say u nampenda, TUPA KULE HUYO SHEMEJI YAO NA UKIMKUBALI TUNAAPIGIA MSTARI ULISHAANZA KUMGEGEDA HATA KABLA KAKA YAKO HAJAFARIKI!Period!!
 
Mkuu kama ni hali nzuri kiuchumi mimi ninao zaidi ya huyo kaka yangu ambaye alikuwa ameajiriwa tu na hakuwahi kumiliki gari.
Mke wa marehemu mwenyewe ndio amenichagua nimrithi sasa tatizo liko wapi?

Amekuchagua kwa sababu una mali! Kumbe hapo ni tamaa zenu tu, mila kisingizio. Mkeo ana kila sababu ya kuomba talaka, Mkuu kuna jambo limejificha hapo kati yako na huyo shemeji tena isiwe ikawa ndio sababu ya ajali ya marehemu!
 
Sasa si ushasema alikuwa ni ke wa rafiki yake
Hiyo ni kesi tofauti ukifananisha na ya kwangu ni kama vile unanionea, mila zetu hazisemi tuwarithi wake wa marafiki zetu bali wake wa kaka au wadogo zetu tumbo moja.
Je huoni tofauti hapo?

Sitaki kuona matusi aisee, yani aliponanihii kaka yako na wewe ukananihii pale plae, lol!!!
 
hicho kikao cha familia na wewe uliyeridhia hovyoooooo

au mnataka mali za marehemu? Maana kama mna nia ya dhati mnaweza kumsaidia shemeji yako bila kumridhi... Tena kamati nzima ya ukoo mmeshindwa kuja na njia endelevu ya kusaidia zaidi ya hiyo?

Na huyo mwanamke kakubali umridhi? Au mlikuwa mnatamaniana kabla mumewe hajafa?

Anyway najiuliza tu

Hata mm nashangaa!!!
 
Amekuchagua kwa sababu una mali! Kumbe hapo ni tamaa zenu tu, mila kisingizio. Mkeo ana kila sababu ya kuomba talaka, Mkuu kuna jambo limejificha hapo kati yako na huyo shemeji tena isiwe ikawa ndio sababu ya ajali ya marehemu!
Temea chini rafiki yangu, hayo si mambo mazuri kusema hapa JF, mimi siwezi kumuua kaka yangu kwa sababu ya mkewe, mbona wanawake wapo wengi tu, tunachofanya ni kufuata matakwa ya mila zetu.
 
Mila za hivo Kama mie rafiki yako nauvunja urafiki!! Yaani mke wa kaka yako unataka umrithi!! Je Kama alikua na ukimwi si mnaangamia?! Kuficha ajali sio kusema hawezi Kua Hana virusi!! Kwanza ni uchafu tu huo!
 
Hizi ni tamthiliya tu hakuna mtu aliyesoma anaweza kuomba ushauri kwa mambo ya kipuuzi ambayo ni obvious. Kama ukiomba ushauri kwa mambo rahisi kama haya akili yako itakuwa inafanya kazi gani? Unless utuambie huna ubongo kabisa ndo tunaweza kukusaidia kwani hakuna mahali panapoonyesha kwamba ukikataa kumrithi utauawa!!
 
Back
Top Bottom