Mke wangu kachachamaa anataka tuachane!

Mke wangu kachachamaa anataka tuachane!

Ni nani kakwambia kwamba kaka yangu kafa kwa ukimwi?
Nishasema kafa kwa ajali mwezi uliopita
i realy dought about your personality !!!!!kweli na kupita pita kwako unaweza kubali hilo pale pale ungewaambia nitawasaidia watoto lakini BUJUGWA LA MKEWE MIE SIGUSI WACHA LILIWE NA NYENYERE!!!SAIDIA HAO WATOTO ITS ENOUGH ACHA ULAFI UTAKUFA .NA INAWEZEKANA WEE NDIO ULIMUONDOA KWA AJALI ILI URITHI MKEWE KAMA SIO BASI WACHA MKEWE
 
Hivi mpaka sasa kwenye dunia hii kuna watu wenye akili hizi?tena mtu mwenye kujua even kuingia kwa mitandao ya Internet?
I wonder TAMAA zinakusumbua tu wewe!!
Sasa mtandao na mila vinaingiliana vipi?
Kusoma haimzuii mtu kufuata mila na desturi za kwao
Mimi ni mmatumbi halisi hata kama nimesoma mpaka PHD niaenzi mila za kwetu
 
Mpe talaka yake aende zake kwa amani na MUNGU amjalie huko aendako afanikiwe wala asikukumbuke tena ubaki na mjane wako, unataka kumuua mwenzio na virus. Bado watu badala ya kutafuta hela mnakaa vikao vya uzinzi.

Umejuaje kama huyo mke wa kaka yako anakupenda? Unahisi watoto wake watajisikiaje wakikuona unalala kitanda cha baba yao? Ingekuwa ni mama yako anatembea na baba yako mdogo ungejisikiaje?

Inaelekea ulikuwa unamtamani toka kaka yako akiwa hai!
Wewe ndio hujui, nani kasema kaka yangu kafa kwa ukimwi?
Acheni uzushi wenu hapa
 
Aaaaaaaaaaahhhhh!Kwa mfano wewe ndiyo ungekuwa mwanamke, halafu mumeo anataka kurithi mke wa kaka yako ungekubali?
Hapa mie naona unaendekeza njaa.Hizi mila zingine bwana, kwanini usichukue tu jukumu la kusaidia kui-support hiyo familia bila kumuoa huyo mwanamke?
Kwani mungu alipomchukua hakujua kama damu yake itapotea.
wewe sema tu ulimtamani shemeji yako tangu siku nyingi na ulikuwa unasubiri wakati muafaka.
ila kama umedhamiria, bora umpe mkeo talaka akaanze maisha mapya salama kabla haujamletea maradhi kutoka huko unakoenda kurithi.

Bora akuache maana hujastarabika hata kidogo!
 
sasa mtandao na mila vinaingiliana vipi?
Kusoma haimzuii mtu kufuata mila na desturi za kwao
mimi ni mmatumbi halisi hata kama nimesoma mpaka phd niaenzi mila za kwetu
to hell sasa ushauri unaomba wa nini hapa jf umeileta mada wakati ushaweka conclusion nashawishika wewe ndio umemuua kaka yako ili ubaki na mkewe potelea mbali
 
Hata angekuwa dada yangu lazima ningemwambia abofye kidude cha undo kwenye hiyo ndoa. Maana ukifa wewe, yeye na huyo mwingine watarithiwa na ndugu yenu mwingine!!!! Bofa ajiondokee zake
 
i realy dought about your personality !!!!!kweli na kupita pita kwako unaweza kubali hilo pale pale ungewaambia nitawasaidia watoto lakini BUJUGWA LA MKEWE MIE SIGUSI WACHA LILIWE NA NYENYERE!!!SAIDIA HAO WATOTO ITS ENOUGH ACHA ULAFI UTAKUFA .NA INAWEZEKANA WEE NDIO ULIMUONDOA KWA AJALI ILI URITHI MKEWE KAMA SIO BASI WACHA MKEWE
Mila hazitaki hivyo ukikubali lazima uendeleze ukoo, kama usipofanya utaleta mikosi kwenye ukoo
 
to hell sasa ushauri unaomba wa nini hapa jf umeileta mada wakati ushaweka conclusion nashawishika wewe ndio umemuua kaka yako ili ubaki na mkewe potelea mbali
Nimetaka watu wa JF wanaishauri namna ya kumsihi mke wangu arudishe moyo nyuma tulee watoto..
haya ni mambo ya mila huwa hayakwepeki
 
Kwa vyoyote utakuwa unatoka huko lushoto, ndiyo kuna kabila linafanana na kabila lingine la huko Moshi ndiyo wana hii mila.
Hizi mila ziko Tanzania nzima sema tu siku hizi wengine wanazikana na ndio maana wanapata mikosi katika ukoo na wanakufa kufa hovyo
 
Kuna kabila moja huku kwenye visiwa vya ziwa victoria, wana tabia ya "KUWATAKASA WAJANE".eti kila mwanamke anayefiwa na mumewe, ili aweze kuolewa na mwanamme mwingine lazima "ATAKASWE", kwa maana kwamba kuna mwanaume(MTAKASAJI) ameteuliwa kwa kazi hii ya kuwatakasa(KUWAGEGEDA) wajane kabla hawajaolewa tena ili wasipate mikosi kwenye ndoa zao.
Sijajua kama huyu mtakasaji ameoa, na kama ameoa, mkewe anajisikiaje wanapoletwa wajane pale kwake kwa ajili ya kutakaswa?

Duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu hi dunia imekwisha kwa kweli
 
Hata angekuwa dada yangu lazima ningemwambia abofye kidude cha undo kwenye hiyo ndoa. Maana ukifa wewe, yeye na huyo mwingine watarithiwa na ndugu yenu mwingine!!!! Bofa ajiondokee zake
Alinipenda mwenyewe, na alikuwa anajua kuhusu mila zetu, ni vile tu ana wivu sana na wasiwasi kuhusu kupanda kwa gharama za maisha, lakini mimi ni mwanaume maisha hayatanishinda nitahakikisha familia haitetereki
 
Sasa mtandao na mila vinaingiliana vipi?
Kusoma haimzuii mtu kufuata mila na desturi za kwao
Mimi ni mmatumbi halisi hata kama nimesoma mpaka PHD niaenzi mila za kwetu
Tangu lini wamatumbi wakarithi wajane?
Isitoshe, Wamatumbi wako kilwa na sio Tanga.hata kwenu haupajui.umekariri hii mila ya kurithi wajane ndiyo unayoipenda na kuizingatia.
 
Mkubwa si umpe hiyo talaka ili kila mmoja ashike "mila" yake tu
 
to hell sasa ushauri unaomba wa nini hapa jf umeileta mada wakati ushaweka conclusion nashawishika wewe ndio umemuua kaka yako ili ubaki na mkewe potelea mbali

Umeona ehhhhh.......usije mruhusu pacha wako FP aolewe na hili kabila.
 
mpe mkeo talaka, oa huyo mke wa kaka ako, . .
Sometimes advice is what we know but just ask for justification.
 
Alinipenda mwenyewe, na alikuwa anajua kuhusu mila zetu, ni vile tu ana wivu sana na wasiwasi kuhusu kupanda kwa gharama za maisha, lakini mimi ni mwanaume maisha hayatanishinda nitahakikisha familia haitetereki
Kwaiyo ukifa wewe itakuwaje?
 
Tangu lini wamatumbi wakarithi wajane?
Isitoshe, Wamatumbi wako kilwa na sio Tanga.hata kwenu haupajui.umekariri hii mila ya kurithi wajane ndiyo unayoipenda na kuizingatia.
Hukunielewa.
Mmatumbi inasimama kama muafrika halisi, ndio nilikuwa namaanisha..
Lakini pia Tanga mbona wapo sana wamatumbi, wayao, wanyamwezi, wawemba, waha warundi, wanyarwanda na wasukuma
We nenda pale Kwa Lukonge utawakuta wengi tu
 
Back
Top Bottom