Mke wangu kachachamaa anataka tuachane!

Mke wangu kachachamaa anataka tuachane!

Eti ni kwa sababu kikao cha ukoo kilichokaa juzi kimeamua nimrithi mke wa marehemu kaka yangu aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Kwa mila na desturi zetu inaruhusu mdogo mtu au kaka mtu kumrithi mke wa ndugu yake pale anapofariki. Sasa namshangaa mke wangu kanuna wiki sasa anataka talaka yake aondoke.

Hivi hapa nimechanganyikiwa sijui nifanye nini maana mke wangu nampenda lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee. Lazima mila iheshimiwe...

Mkuu kwa dunia ya leo bado una haya mawazo jaman!
 
eti umekuja kuomba ushauri.hebu nihamie kwingine.
Kila la kheri kaka.Tekeleza mila kaka.Bahati nzuri umeoa mke ambaye haujui haki zake.
Wewe ni mkataa kwenu.
Umazitupa mila na desturi zenu na ndio maana unatokwa na povu kwa mila za wengine ambazo hazikuhusu
 
marehemu kaka yako alipima???????swali lingine...hivi huko kwenu tarehe mnazotumia zimeshafika ANGALAU 1900?swali la mwisho tafadhali......unaishi misitu ya kongo au tanzania hii hii?

Hahahaha well said mkuu
 
Eti ni kwa sababu kikao cha ukoo kilichokaa juzi kimeamua nimrithi mke wa marehemu kaka yangu aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Kwa mila na desturi zetu inaruhusu mdogo mtu au kaka mtu kumrithi mke wa ndugu yake pale anapofariki. Sasa namshangaa mke wangu kanuna wiki sasa anataka talaka yake aondoke.

Hivi hapa nimechanganyikiwa sijui nifanye nini maana mke wangu nampenda lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee. Lazima mila iheshimiwe...

Kama hataki kukubaliana na mila zenu, achana naye. Wewe endelea na huyo mke wa marehemu ili udumishe mila. Utapata mke mwingine. haina shida.
 
Ni nani kakwambia kwamba kaka yangu kafa kwa ukimwi?
Nishasema kafa kwa ajali mwezi uliopita

kwani aliyekufa kwa ajali hawezi kuwa alikuwa nao kabla we una hakika gani na afya yake? Mila nyingine inabidi zifutwe tu hali ya sasa au we mwenzetu unaishi nchi gani, mana nashangaa eti mpaka leo hii bado hizo mila na desturi........tafakari na chukua hatua!!!!!! Achana na mambo ya kizamani
 
eti umekuja kuomba ushauri.hebu nihamie kwingine.
Kila la kheri kaka.Tekeleza mila kaka.Bahati nzuri umeoa mke ambaye haujui haki zake.[/QUOTE]
Kuna watu tunao karne hii lakini ilibidi waishi enzi za kurithiana wake.... yaani mtu anajieleza eti 'mke wangu analeta kauzibe'. Hawa nahisi walikuwa wangegedana hata kabla kaka yake hajafa.... ila kwa sasa anatafuta namna ya kuiweka iwe 'official' tu..
 
Basi isiwe nongwa tutapima huo ukimwi ili yaishe
 
eti umekuja kuomba ushauri.hebu nihamie kwingine.
Kila la kheri kaka.Tekeleza mila kaka.Bahati nzuri umeoa mke ambaye haujui haki zake.[/QUOTE]
Kuna watu tunao karne hii lakini ilibidi waishi enzi za kurithiana wake.... yaani mtu anajieleza eti 'mke wangu analeta kauzibe'. Hawa nahisi walikuwa wangegedana hata kabla kaka yake hajafa.... ila kwa sasa anatafuta namna ya kuiweka iwe 'official' tu..
Naomba ujifunze h=kuheshimi mila za wenzako mkuu. Mimi sijaja hapa kuomba kutukanwa bali kuomba ushauri namna ya kumsihi mke wangu arudishe moyo wake nyuma ili tulee watoto
 
Hakuna tusi hapo kaka, ila unapewa LIVE tu... Kama vipi niwekee matusi niliyokutukana hapa... Kuhusu kuheshimu mila kuna ambazo hata ufanyeje siwezi, kwa mfano kukeketa, kurithi mke/mume.... Hayo siwezi kuyaunga mkono kisa 'h=kuheshimu mila za wengine'... BIG NOOO

Ni nani kakwambia kwamba kaka yangu kafa kwa ukimwi?
Nishasema kafa kwa ajali mwezi uliopita

Kwa hiyo umetamani mabaki ya hilo gari na mali nyingine ndio maana unajifanya umeshikilia mila!! loooo hebu uwe na haya kidume wewe! Unaonekana wazi huna upendo zaidi ya kutamani vya kaka yako, nyie ndio mnaowatamanigi shemeji zenu!

Acha bana, endelea kumtunza mke wa marehemu na watoto wake na umuheshimu kama shemeji; USIMRITHI na kumfanya mkeo.
 
Eti ni kwa sababu kikao cha ukoo kilichokaa juzi kimeamua nimrithi mke wa marehemu kaka yangu aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Kwa mila na desturi zetu inaruhusu mdogo mtu au kaka mtu kumrithi mke wa ndugu yake pale anapofariki. Sasa namshangaa mke wangu kanuna wiki sasa anataka talaka yake aondoke.

Hivi hapa nimechanganyikiwa sijui nifanye nini maana mke wangu nampenda lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee. Lazima mila iheshimiwe...

Watu watakuja na yao, cha msingi ni kuzingatia mila na nafsi maana kwa mfano kama wewe ni Muislam sijaona shida kuoa mke wa kaka, kama mkristo mke ni mmoja tu. Namkubali Zuma kwa africa nzima maana yeye ndio pekee amekataa kuwa mzungu kwa kudumisha mila mke kadhaa.
 
siku hizi nimeokoka na kuacha matusi otherwise ungenikoma
 
Eti ni kwa sababu kikao cha ukoo kilichokaa juzi kimeamua nimrithi mke wa marehemu kaka yangu aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Kwa mila na desturi zetu inaruhusu mdogo mtu au kaka mtu kumrithi mke wa ndugu yake pale anapofariki. Sasa namshangaa mke wangu kanuna wiki sasa anataka talaka yake aondoke.

Hivi hapa nimechanganyikiwa sijui nifanye nini maana mke wangu nampenda lakini pia nisingependa damu ya kaka yangu ipotee. Lazima mila iheshimiwe...

Buluu hapo mh! mwe! wonders shall never cease
 
Cheeeee!!!Yaani izo mila potofu bado ipo!! Ebu acha ujinga wewe. Mpeni huyo mwanamke uhuru wa kuamua aolewe na nani na ivi hujui kuwa ni matusi kumuoa mke wa kakao?Na vipi kuhusu magonjwa!!! Lol!!Ebu badilikeni bwana
 
Naomba ujifunze h=kuheshimi mila za wenzako mkuu. Mimi sijaja hapa kuomba kutukanwa bali kuomba ushauri namna ya kumsihi mke wangu arudishe moyo wake nyuma ili tulee watoto
Ngoja nikupe mbinu sasa; Ukishazima computer yako, nenda ukampigie magoti, halafu uanze kulia kama umepata msiba mwingine, wakati anakubembeleza jaribu kumsihi kwamba unahisi siku zako za kuishi zimebaki kidogo, hivyo muombe arudishe moyo wake nyuma ili aje mlee watoto, Basi hapo kwa huruma atakubali kuendelea kuishi na mumewe " Haambiliki Tegelezeni
 
Kuna kijana namfahamu yeye alimlea Mke wa marehemu rafiki yake ambae alikuwa mjamzito, alijifungua na jamaa akalea mtoto na mama yake na akamsomesha mtoto hadi leo hii jamaa ana mke wake na huyo mke wa mareheu rafiki yake alishaolewa kitambo na amini usiamini jamaa hakuwahi tembea na huyo dada hata siku mojs!Kumbuka alikuwa mke wa rafiki tu, sasa wewe kaka yako!!!!!!!!!!!!Ebu acha uhuni bwana
 
Ngoja nikupe mbinu sasa; Ukishazima computer yako, nenda ukampigie magoti, halafu kama umepata msiba mwingine, wakati nakubembeleza jaribu kumsihi kwamba unahisi siku zako za kuishi zimebaki kidogo, hivyo muombe arudishe moyo wake nyuma ili mlee watoto, nasi hapo kwa huruma atakubali kuendelea kuishi na mumewe " Haambiliki Tegelezeni
Yaani anakuja kuomba ushauri wakati tayari ana majibu ya anachoulizia na ana msimamo wa kutobadirika...

Back
Top Bottom