Mke wangu hapendi ndugu zangu.

Mke wangu hapendi ndugu zangu.

Wazazi wako ni wazazi wako na hakuna wa kukutenga nao. Walikuelekeza jinsi ya kuishi hadi ukawa kijana morani na ukaja kuoa. Weka issue za familia yako mbali na issues za wazazi wako. Timiza wajibu wako nyumbani, na wajibu wako kwa wazazi.

Wa kulaumiwa ni wewe. Unashindwa jinsi ya kuwasiliana na wote. Hivi kuna siku ulishasema home 'jane yule receptionist, kaniambia friji za zec ndo nzuri kwa hiyo nitanunua' ? Kuwa muangalifu na taarifa unazopeleka kati yao. Namaanisha kuwa mwanaume. Jipange.

Asante kwa hayo
 
Tambua mipaka iliyopo kati ya wazazi na wewe na mke wako, vile vile kati ya mkeo na wazazi!
 
isije ikawa yeye, mwanaume, ndiye anayetakiwa kurudishwa kwao akafunzwe jinsi ya kuishi na mke.. ni ngumu ku-judge kutokana na jinsi alivyoileta sory yenyewe, haijakamilika.
isije kuwa ni yule mwanaume anayemwambia mkewe "mama kasema tusinunue gari tununue shamba, mama kasema mtoto asiende shule hii aende ile, mama kasema bla bla bla...". atueleze vizuri

Kwa hiyo mume akifanya hayo ndio mke anaruhusiwa kuwachukia wakwe zake???
 
tatizo huwa tunajidanganya kwamba atabadilika akifika ndani ya ndoa..... yani ni bora kuamni mlima kilimanjaro kuna siku utaamia dar es salaam.... kuliko kuamnini tabia ya mtu itabadilika hasa katika maswala nyeti kama ya ndoa.... pole mkuu hiyo ni chuki ambayo ni personal kama una imani jaribu kumwomba Mungu atakusaidia lakini kwa akili za kibinadamu sidhani kama utaweza...!!!!!!!!
 
Huyo mkeo inaonesha unamuendekeza sanaaaa...we miaka tisa yote unapandwa kichwani tu!!!

Rudisha kwa wazazi wake huko wakamfunze namna ya kuheshimu mume na wazaa chema asilete umajinuni...

Sidhani kama inafaa kutoa hukumu hiyo wewe Watu8 just kwa kusikia story from one side. Haya matatizo huwa magumu sana kuyatolea hukumu pasipo kujua chanzo cha tatizo. Kwa nini awachukie wazazi? Yaani from nowhere tu awachukie! There is a strong reason my dear.
 
Kwa hiyo mume akifanya hayo ndio mke anaruhusiwa kuwachukia wakwe zake???

sisemi kama awachukie wakweze. ila mwanaume ukiambiwa huwezi amua kwenye family yako, kila kitu unafanyiwa maamuzi na wazazi wako, hiyo ni serious issue na unatakiwa ujitazame mara mbili.
huyo jamaa naye alitakiwa atuambie kwa nini mkewe anadai anafanyiwa maamuzi na ndugu zake.
atueleze pia je anaishi na mkewe kwa wazazi wake au? maana mkiishi kwa wazazi wote wawili mnapoteza nafasi ya kuwa baba/ mama mwenye nyumba.
 
Sidhani kama inafaa kutoa hukumu hiyo wewe Watu8 just kwa kusikia story from one side. Haya matatizo huwa magumu sana kuyatolea hukumu pasipo kujua chanzo cha tatizo. Kwa nini awachukie wazazi? Yaani from nowhere tu awachukie! There is a strong reason my dear.

Mimi ni muhanga wa tabia kama hiyo ya wanawake, wengi wao wala huwa hawana sababu yoyote ya msingi bali huwa wamejaa CHOYO, UBINAFSI n.k.

Na kumrudisha mke kwa wakwe akajifunze adabu hiyo wala sio hukumu bali ni utaratibu wa kimila za kibantu...unless uniambie hufahamu vizuri mila za Kitanzania.
 
Rafiki yangu hata kama ukielezwa hayo ya upande wa pili, bado hayafuti makosa ya huyu bi dada...

sisemi kama awachukie wakweze. ila mwanaume ukiambiwa huwezi amua kwenye family yako, kila kitu unafanyiwa maamuzi na wazazi wako, hiyo ni serious issue na unatakiwa ujitazame mara mbili.
huyo jamaa naye alitakiwa atuambie kwa nini mkewe anadai anafanyiwa maamuzi na ndugu zake.
atueleze pia je anaishi na mkewe kwa wazazi wake au? maana mkiishi kwa wazazi wote wawili mnapoteza nafasi ya kuwa baba/ mama mwenye nyumba.
 
Kumbuka mwanaume ni kichwa cha familia sasa kichwa kikilegalega mambo huwa hayaendi. Inawezekana na wewe kwa kiasi flani unachangia hali kuwa hivi hata kama ni kwa 0.00009% bado inaweza kuleta matata kwenye familia so jichunguze halafu simama nafasi yako kumbuka kichwa ndicho chenye maamuzi kikiamua leo safari ni kkoo basi na miguu lazima ielekee huko . Lkn kichwa kikiwa hakijielewi bwana waweza jikuta unaingia jalalani ooohoooo.
 
unajua sheria haifuati demokrasia? KIFUPI, kila mmoja anapaswa kuheshimu nafasi ya mwenzake.

BIBLIA INASEMA "ASIYEWATUNZA WA KWAKE HASA MKE NA WATOTO AMEIKANA IMANI TENA NI KAMA MCHAWI" hivyo mwelekeze shemeji kwa misingi ya imani kuwa unawajibika kuwatunza na huwajibiki kuamuliwa kila kitu mke awe mshauri ni si sauti ya mwusho na huo ndo uongozi, VILEVILE
"WAHESHIMU BABA YAKO NA MAMA YAKO SIKU ZAKO ZIPATE KUWA NYINGI KATIKA NCHI UPEWAYO NA BWANA MUNGU WAKO" hivyo heshima ni kuwatendea wema ndio maana yake na si kuwatenda jeuri HATA HIVYO
"ENYI WAZAZI MSIWACHOKOZE WATOTO WENU BALI WALEENI KATIKA MAONYO YA YEHOVA" hivyo angalia penye udhaifu rekebishA na endelea na maisha
 
Mimi ni mwanamke lakini nakubaliana na wewe 100%...sisi ndio chanzo cha maugomvi kwenye familia za watu...usiombe familia iwe na upendo afu mmoja abugi step aoe mwanamke asiyejua kubwa na dogo...mtasambaratishwa kama M23...
Mimi ni muhanga wa tabia kama hiyo ya wanawake, wengi wao wala huwa hawana sababu yoyote ya msingi bali huwa wamejaa CHOYO, UBINAFSI n.k.

Na kumrudisha mke kwa wakwe akajifunze adabu hiyo wala sio hukumu bali ni utaratibu wa kimila za kibantu...unless uniambie hufahamu vizuri mila za Kitanzania.
 
Pole sana ndugu. mwelewwshe mkeo umuhimu wake na wa wazazi wako katika maisha yako. asilete ujinga amejisahau huyo hajui kuwaheshimu wazazi huleta baraka
 
It is 100% your fault. Wewe kama mwanaume umeshindwa kusimama katika nafasi!
 
Wewe ndo ulitakiwa ku'define mipaka katika ndoa yako. Ndugu wa pande zote ni muhimu lakini maamuzi katika ndoa yako ni wewe na mkeo. I don't see how, hao ndugu wa pande mbili wameingia kwenye mgogoro mpaka hawasalimiani? Definitely kuna maneno yalikua yanapelekwa to both sides, maybe in the form of 'malalamiko' kwamba mwenzangu kanifanya hivi, ndugu zake wamesema vile, etc, etc... then hiyo ikazaa chuki kwa kila upande kuona ndugu yao anaonewa. I don't see how mkeo anaweza kuwachukia ndugu zako kama kila decision katika ndoa yenu mnakubaliana na kufanya as a team. Inaonekana kuna sehemu umekosea big time.
 
Kwa ushauri, huyo sio wa kumuacha au kumrudisha kwao (usidhani ukimuacha ndo unamkomoa, life goes on anaweza hata akaolewa tena and find happiness huko! Plus utawapa shida watoto). Kaeni wewe na mkeo kwanza muongee, try to figure out where you two went wrong. Also do some soul searching. Determine if you still love her and want to continue with the marriage. If you get positive results from this, present that to both families. Waambieni mmesameheana na mnawaomba wao kama ndugu wafanye hivo pia. Set boundaries in your marriage and ask both families to respect that. Remember, mkeo na watoto ni wakwako. Ukikosea, unaharibu familia yako mwenyewe na wakulaumiwa ni wewe mwenyewe kama baba kwa kushindwa kuiongoza. Best of luck and I wish you resolve this soon because problems in marriage really affect children. You might not notice it now, but its true.
 
Jamani wana JF naomba ushauri wenu,niko ndani ya ndoa zaidi ya miaka kumi tuna watoto 3,kinachofanya niombe ushauri ni kwamba baada ya kufunga ndoa ndani ya mwaka 1 familia yangu ilianza kuwa na migogoro isiyoisha,tatizo mke wangu hapendi ndugu zangu hasa wazazi wangu,imefikia ndugu wa pande zote mbili wazazi wa mke na wazazi wangu hawasalimiani,kisa anadai mie nafanyiwa maamuzi na wazazi wangu,imefikia mahala sasa hataki kuwasalimia hata wazazi wangu,nifanyeje?

Pole sana mkuu. Maisha ndivyo yalivyo, yana misukosuko mingi mno. Na wakati mwingine mambo ambayo hukuwahi kufikilia kutokea ndo hutokea.

Kwangu mimi, happy life ndio kitu cha kwanza katika maisha. Hivo chochote kile kinachotokea kutaka kunipokonya furaha naachana nacho haraka sana iwezekanavyo.

Wazazi wangu na ndugu zangu ni watu mhimu sana. Hii ni kutokana na ukweli kuwa baba na mama na ndugu siwezi kuwapata mahali popote pale. Lakini mke, wakati wowote na mahali popote anapatikana.

Kwa utamaduni wa Afrika,familia nyingi ni extended families. Hakuna namna yoyote ile niwezavyo kujitenga na baba, mama na ndugu zangu. Ikiwa ni hivo basi mke wangu kama hawataki basi hanitaki hata mimi. Na kwanini niendelee kuishi nae!

Kibaya zaidi migogoro ya namna hiyo ikishaanza ndani ya familia ni kama kidonda ndugu. Haiishi mpaka kufa. Mtaisuruhisha kwa kila namna lakini kinyongo hakiishi ndani ya moyo wa mlalamikaji.

Wengine wanasema ni majaribu katika ndoa hivo unatakiwa kuvumilia na kumvumilia mwenzako. Lakini kwangu there is no point of living if I can't feel happy in my life.

Hivyo jiulize nikitu gani cha msingi unachohitaji katika maisha yako. Ukilijua hilo, utapata ufumbuzi wa tatizo hilo kwani utaona njia ya kufuata.
 
Lazima yalianzia mbali na wewe kiunganishi cha hizi pande mbili ulizembea sehemu!

Wewe na mkeo wote ni watoto kwa wazazi wako na wake,hebu jishusheni na mjifunze kunyenyekea hata kama hamuwategemei kwa chochote. Ongea na mkeo asahau yaliyopita,kawaombeni radhi wazazi maisha yaendelee kila mmoja akiwa kwake,mkikutana msalimiane ikipita 2weeks na zaidi watoto pigeni simu kuwajulia hali basi.

Usikubali kuwa katika nafasi ya kuchagua kati ya wazazi na mkeo na watoto maana kila kundi lina nafasi yake kwako na hakuna kundi rahisi wewe kulitelekeza hapo.

Mwambie mkeo Sikio Halizidi Kichwa!


mbona wewe ni sikio la punda kabisa!!!!
 
Back
Top Bottom