Mke wangu hanisikii

Huyo pengine si ubavu wako, na ukorofi na roho ya kimaskini na ubinafsi inayomsumbua pengine pia ndo ilomtoa kwa mume wa kwanza. Muombe mungu, pia sikiliza sauti ya moyo wako inasema nini, kwani hata ukipata ushauri mwisho wa yote ni moyo wako unataka nini.

Mke wako yupo tu, usijitwike msalaba usio wako kaka huyo dada hatabadilika.
 
Pole sana kwa hayo yanayokukuta. Hapa kuna maswali najiuliza:-

>> Wewe mwanaume una umri gani sasa?
>> Kwanini uoe mwanamke aliyeachika, Je, ulizifahamu sababu za kuachika kwake?
>> Mlioana kwa namna gani, mlifunga ndoa au mlichukuana kienyeji kienyeji?

Nafikiri maswali haya yakijibiwa vizuri pamoja mengine wanayojiuliza wengine utapata jibu.
 
Huyo amepata Mwingine,apo una jinsi achana nae,na ata ikitokea one day anataka rudi kwako KIMBIZA ni kimeo cha Nguvu.Najua unaweza kuwa UNAMPENDA but piga Moyo Konde usiangalie Nyuma(nnajua ipo siku atakutafuta) wewe mpotezeee mlupo huyo.MALAYA NI MALAYA AFAI KUWA MKE
 
ingawa wengi wanamyooshea kidole huyu mama,mie nahisi ndoa yake iliyopita ilimuathiri amejikuta anakaa kimachale machale.:twitch:
Apana huyu Mwanamke anaonekana Mapepe tu, na wapo wengi sana now days!wanababaika na vitu vidogo tu then wanakuja kukumbuka shuka asubuhi wakati Mbu wamemg`ata usiku kucha,
Kweli NO WOMAN NO CRY
 
Pole sana kwa hayo yanayokukuta. Hapa kuna maswali najiuliza:-

>> Wewe mwanaume una umri gani sasa?
>> Kwanini uoe mwanamke aliyeachika, Je, ulizifahamu sababu za kuachika kwake?
>> Mlioana kwa namna gani, mlifunga ndoa au mlichukuana kienyeji kienyeji?

Nafikiri maswali haya yakijibiwa vizuri pamoja mengine wanayojiuliza wengine utapata jibu.
Mkuu hivi wanawake walio achika hawana haki ya kuolewa tena?
 
nimeoa mwanamke aliyeisha olewa zamani na akaachika, maelewano na masikilizano ndani ya nyumba mwanzo yalikuwa mazuri, ukorofi ukaanza ghafla, akashika mimba akaenda itoa kisha akadai imetoka yenyewe, safari za kwenda kwao zikawa haziishi , na vitu vyake alivyokuja navyo kwangu akawa anahamisha kidogo kidogo kila nnapokuwa sipo.

Nilipomuuliza akadai yeye kuna mtu amemuazima pesa na ili akasome ndio kaamua na yeye amuazime vitu vyake kisha akimaliza kusoma ataenda kuvigomboa, nikamuuliza mbona mimi hukunishirikisha ktk hilo japo vitu ni vyako, basi kuanzia hapo ni makeke tu na hivi niongeapo yuko kwa dada yake yapata wiki na zaidi hakuna ugomvi zaidi ya hilo suala, jana ananiambia uko kimya hali ya kuwa unajua nahitaji kwenda kusoma huku sina hela nikueleweje, NIMEMWAMBIA KAMA UNAJUA MIMI NI MUMEO NAWAJIBIKA KWA HILO NI VIPI UKAE KWA DADA YAKO ...?

NIMEKATA MAWASILIANO NA YEYE KAKAA KIMYA ..........
Nakushauri uwaite wazazi wako na wazazi wake, uwaeleze tatizo lenu na yeye hakiwepo.
 
mi nilishashuhudia kimara mke aliolewa akiwa anafanya kazi na alikuwa na fenicha kiasi, migogoro ilipoanza wakatengana vyumba mke akawa anagomga kwa nguvu mlango wa mumewe usiku hadi majirani tunaamka eti anataka mume amtolee dressing table yake aliyokuja nayo na kuwa haimuhusu alikuja nayo. aibu zilipozidi, mume alianza mchakato wa talaka ndo akili ya mke ikafunguliwa akauona uovu wake na kutambua kuwa sasa anaachwa! ndo akaomba msamaha na hadi leo kama miaka ninne hvi wanaishi kwa amani.

sasa case yako umeonyesha moyo mkuu wa uvumlivu. mkeo yuko katika mchakato wa kujitammbua. yaani licha ya kuvunja ndoa yake ya kwanza inaelekea bado hajajitambua. sasa nakushauru mvumilie na usiweke akilini mwako vitu vyake muache avihamishe kadiri atakavyo hata kama atamaliza vyote. watu wengine ni wabinafsi sana na kila siku huhesabu kila walichotaaabikia na roho huwauma kuona wengine wakinufaika na jasho lao.

ila wewe mtegemee Mungu kutafuta vitu vya familia yako. matumizi usimvyime kama uwezo unao. wema wako ndio utakaomfanya amuogope Mungu na kuuona uovu wake. ila kama hatimaye ataondoka mwenyewe, wewe utakuwa umejitenga na dhambi yake na usimzuie muache aende kwa amani kwani Mungu ametuita katika amani.

pole sana kaka yangu, Mungu aijaze nyumba yako kwa faraja na upendo wake hata kama mwenzio atakuacha
 
Mimi nadhani mliingia kwenye mahusiano kabla ya kujuana vyema,

Wapo wengi walioachika na wakaolewa na wanaendelea, kuna tabia moja mbaya hiyo ya 'kuazimana' fedha..I hate the wording and that behaviour

Nadhani mkuu unajibu la yote japo umeileta jamvini ili ui'confirm' tu, kwa ushauri kwakweli yambidi awe muwazi sana kwako,

Ndoa ni nzuri lakini pasipo uwazi watu 'wanaazimana' hela na mengineyo
 
....Dawa yake huyo ni kumchunia usipige simu wala kwenda huko,uone atareact vipi.
 
jamani w.ke wengi wakiachika,wakija kuolewa tena hutulia katika ndoa zao.There are 2 sides to every story.maybe huyo dada ni mkosaji au maybe huyu kaka nae ana mapungufu yake,pengine huyo dada kipo kilichomkimbiza.The best way,mfate huyo mke wako,muulize vizuri tatizo lipo wapi na awe mkweli,na kama kuna sehemu ya kujirekebisha wote wawili,basi mjirekebishe,lakini kama hakutaki tena,using'ang'anie,amini huyo sio riziki yako
 
nimeoa mwanamke aliyeisha olewa zamani na akaachika, maelewano na masikilizano ndani ya nyumba mwanzo yalikuwa mazuri, ukorofi ukaanza ghafla, akashika mimba akaenda itoa kisha akadai imetoka yenyewe, safari za kwenda kwao zikawa haziishi , na vitu vyake alivyokuja navyo kwangu akawa anahamisha kidogo kidogo kila nnapokuwa sipo. Nilipomuuliza akadai yeye kuna mtu amemuazima pesa na ili akasome ndio kaamua na yeye amuazime vitu vyake kisha akimaliza kusoma ataenda kuvigomboa, nikamuuliza mbona mimi hukunishirikisha ktk hilo japo vitu ni vyako, basi kuanzia hapo ni makeke tu na hivi niongeapo yuko kwa dada yake yapata wiki na zaidi hakuna ugomvi zaidi ya hilo suala, jana ananiambia uko kimya hali ya kuwa unajua nahitaji kwenda kusoma huku sina hela nikueleweje, NIMEMWAMBIA KAMA UNAJUA MIMI NI MUMEO NAWAJIBIKA KWA HILO NI VIPI UKAE KWA DADA YAKO ...? NIMEKATA MAWASILIANO NA YEYE KAKAA KIMYA ..........
Endelea kukauka na kama unaweza kusafiri japo kwa mwezi.
 
Jamani ukisikia kuna wanawake wana bahati ndo kama huyu.
Haaa unamfanyia mwanaume mambo kama haya bado yuko na wewe??
Hapa ndo kitchen Party/Unyago nk vinahitajika mwanaume anatakiwa kuheshimiwa na si kumfanyia mchezo wa kijinga kama hivi.
HAJAFUNDWA HUYU NA SI MTZ NAHISI KAMA VILE MKENYA!!!Hana adabu kabisa.
Pole sana my brother ila uvumilivu tu ndo unatakiwa ila mie kama mimi mpe displine kwakweli anatuabisha wanawake wenzake
 
Achana naye huyo,atakuua bure!mwenzio nilishaweka nadhiri ya kutokuoa aliyeachika ama aliyekwishazaa!

Kuachika wala kuzaa co tatizo, nafikiri hapa kati lipo tatizo na anayejua nje ndani ni yeye na mke wake! Nashauri awashirikishe wazazi au watu wazima wenye busara zao watawasaidia.
Mi nimeoa mke aliyeachika na ana mtoto mmoja, ninampenda ila ananipenda zaidi za sn, am proud of that na ninakiri kwa mwenyez mungu we love each other, so litafutwe tatizo.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom