MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,562
naogopa ku mwambia umwache yasije nitokea yaliyonikuta huko nyuma. mwaka juzi mdogo wangu alioa mke kutoka mikoani, sasa alipomuowa yule mke akawa na vitimbi vya ajabu ajabu na mara anadai huyo mme siyo chaguo lake, ndani pakawa hapakaliki na mimi mwenyewe nikaona kweli ndani hakuna maelewano. siku moja mdogo wangu akawapigia wazazi wa yule mke wake akawaelezea kila kitu. wale wazazi walipompigia mtoto wao (mke wa dogo), mwanao akawajibu hivi...kwani baba we ndio umeolewa huku? msinilazimishe kuishi na mtu ambaye mm simtaki. hapo na mm nilikuwa naskia na naona hiyo movie...hapohapo nikachukua uamuzi wa kumshauri dogo amuache. sikujua kuwa dogo alikuwa anaomba ushauri wa kumfukuza mke wake ili hali bado anampenda, wakienda kitandani wanabembelezana. baade dogo kanambia..aah, nimeamua nimsamehe amesema atajirekebisha, ngoja tuone itakuwaje hapo baadae.
then wakaanza kuishi wote na mimi niliyetoa ushauri wa kuachana nikaanza kuona aibu. pamoja na kuwa wanaishi lakini wanaishi maisha ya bora liende..mwanamke ni mchungu kama pilipili, namuonea sana huruma dogo maana ile siyo ndoa ni ndoano.
ndio maana nasema msimshauri amwache huenda anampenda sana na nyie atawashangaa kwa ushauri wenu maamuzi ya mwisho anayo yeye...maana ndiye anayefinywa...
Katika washauri wa makmbo ya ndoa wewe unastahili...TEAMO huwa ana msimamo kama wako.
HATUJUI ANACHOMPENDEA- SO HATUWEZIMSHAURI AMUACHE.
On second thought............mtoa mada ameomba tumshauri namna ya kumwacha mkewe au amelalamika tu kuwa mke hamsikilizi???
Kaa chini ongea na mkeo, mweleze usiyoyapenda na yeye akueleze anayoyataka, muya-table na kupanga namna ya kuyatekeleza. Mawasiliano ni muhimu MUME na MKE COMMUNICATION ni muhimu sana.