Mke wangu hanisikii

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,524
863
nimeoa mwanamke aliyeisha olewa zamani na akaachika, maelewano na masikilizano ndani ya nyumba mwanzo yalikuwa mazuri, ukorofi ukaanza ghafla, akashika mimba akaenda itoa kisha akadai imetoka yenyewe, safari za kwenda kwao zikawa haziishi , na vitu vyake alivyokuja navyo kwangu akawa anahamisha kidogo kidogo kila nnapokuwa sipo.

Nilipomuuliza akadai yeye kuna mtu amemuazima pesa na ili akasome ndio kaamua na yeye amuazime vitu vyake kisha akimaliza kusoma ataenda kuvigomboa, nikamuuliza mbona mimi hukunishirikisha ktk hilo japo vitu ni vyako, basi kuanzia hapo ni makeke tu na hivi niongeapo yuko kwa dada yake yapata wiki na zaidi hakuna ugomvi zaidi ya hilo suala, jana ananiambia uko kimya hali ya kuwa unajua nahitaji kwenda kusoma huku sina hela nikueleweje, NIMEMWAMBIA KAMA UNAJUA MIMI NI MUMEO NAWAJIBIKA KWA HILO NI VIPI UKAE KWA DADA YAKO ...?

NIMEKATA MAWASILIANO NA YEYE KAKAA KIMYA ..........
 
Yale yale... ndugu mwanaJF mwenzangu.... dalili ya mvua ni mawingu.... sasa unasubiri nini tena mwenyezi mungu akuoneshe ndio utambue huyo mke kimeo?????:twitch:
 
ndugu kwa hiyo hatua aliyofikia hapo huna chako, kaa chini tafakari, chukua hatua...
kwani umemuoa lini? yaani ndoa yenu inamuda gani???
 
Uwezekano mkubwa ni kwamba pole pole wanarejeana na mumewe wa mwanzo, na ndiyo maana hataki hata kupata mtoto na wewe.

Nilishawahi kukumbana na kesi kama mbili hivi wanawake wameolewa na waume wengine wana uhusiano na waume zao wa mwanzo.
 
Huna mke hapo, ndo ameshakupa taarifa kuwa una mwenzio hapa kwako nachuma tu kukamilisha malengo yangu.
 
Pole sana,hongera yataka moyo kuoa mwanamke aliyeisha achika kwa mumewe kwanza.......

Nakushauri tulia na jipange vizuri kukabiliana naye.....huo ni mwanzo tu,kama alimuacha wa kwanza akakupata wewe then anajua aweza mpata/kama si anaye mwingine.......

Muombe Mungu akulinde na aondoke salama,huna mke,una mwanamke unayeishi nae chini ya dari moja.......let her go....forgive....move on!!!!

Na kama yuko kwa dada yake na dada yake haoni tatizo,then hata ndugu zake hawana busara au labda hawakutaki......kama unampenda sana mpe muda uone,mshirikishe Mungu na wazazi na ndugu zako pia,watakushauri.
 
Dah!
Vioja vya ndoa haviishi.
Mmh wengine naona hatutasogeza pua zetu huko.
 
Pole sana..mara ya mwisho we na mkeo mlienda kanisani au msikitini ilikuwa lini?

Hizi ndoa bila mungu ni ngumu sana...
 
Moja ya vitu vigumu ni kumshauri mtu kuhusu mwenza wake, hakuna anayejua ni jinsi gani unampenda.

Humu ndani utapata ushauri mbali mbali lakini situation nzima ni wewe unaijua, nakushauri tafuta mtu mzima unayemuamini mueleze in and out, ukiweza fanya kwa watu kama watatu hivi sikia comments zao then chukua hatua.

Vinginevyo u got the wrong couple but u deserve to be happy with ur mariage, so chukua hatua
 
Labda na wewe ni wale wanaume wenye gubu, hawapendi maendeleo na wenye visa nyumbani-dada wa watu kaona ameingia sipo hivyo anajinasua taratibu:twitch::twitch:,...........

Ongea na huyo dada yake aongee naye aseme tatizo ni nini mpk mnashindwa kuwasiliana,kwa nini alishindwa kukuambia anataka kujiunga na shule? Aliogopa hutam-support au nini tatizo?

Duh, ila POLE SANA.
 
Moja ya vitu vigumu ni kumshauri mtu kuhusu mwenza wake, hakuna anayejua ni jinsi gani unampenda.

Humu ndani utapata ushauri mbali mbali lakini situation nzima ni wewe unaijua, nakushauri tafuta mtu mzima unayemuamini mueleze in and out, ukiweza fanya kwa watu kama watatu hivi sikia comments zao then chukua hatua.

Vinginevyo u got the wrong couple but u deserve to be happy with ur mariage, so chukua hatua
Mkuu kumbe nyanja hizi pia upo fit?
 
ila siriazz kama ni kweli una uhakika aliitoa mimba yako......then that should be a warning sign,haoni future na wewe!..tunatoa mimba za maboyfriend tu sio waume zetu...mnh????:twitch::twitch::twitch::sick:
 
Achana naye huyo,atakuua bure!mwenzio nilishaweka nadhiri ya kutokuoa aliyeachika ama aliyekwishazaa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom