Nimekataa ndugu wa mke wangu kwenye biashara zangu, sitaki ujinga!

Mkulungwa01

JF-Expert Member
Jul 14, 2021
3,979
5,295
Jumatatu njema kwenu nyote!

Huwa nafikiria mengi mno, na hawa kaka zake ni kutoka mkoa ule karibu na Tanga, wilaya ile inayoanza na herufi M na kuishia na herufi E.

Hapo kabla kulizuka maneno maneno mengi mno kwenye familia yangu hasa kutoka kwa kaka zake mke wangu. Maneno hayo yalihusu mimi kuwatenga na kutowakumbatia kaka zake hasa wakubwa, pamoja na wadogo zake kwenye miradi yangu ya kiuchumi.

Sikufanya haya kwa bahati mbaya, hii ilitokana na ukweli kwamba ndugu zake mapema mno walianza kuingilia familia yangu kiuchumi, from nowhere nampa mke wangu 500000 aniwekee tu ili nimpime, unakuta katoa yote kampa kaka yake na kabaki na 50000 tu. Namuuliza samahani na kujiliza kunakuwa kwingi mno.

Hapo nilikuwa najifunza kitu. Sasa timefungua mradi mkubwa sana mpya, nimeajiri watu tofauti kabisa na yeye alipendekeza wawe kaka zake 'atleast' watatu 'on top of management', hili nililikataa.

Mke alinielewa sasa tangu hapo nasikia maneno maneno ya kunisema mno, na sijui shida hasa ni ipi. Kama ni fedha huwa nawasaidia wakikwama tena kwa roho safi kabisa, siyo pesa tu, ni pesa nyingi sana.

Shida ni kwamba wanasema nawatenga, kwa sababu siwahusishi na biashara zangu. Najiuliza nawatenga kivipi? Mbona wakati wa matatizo nawajibika bega kwa bega pamoja nao? Kwa nini wanafikia kunichukia kwa kunisema vibaya?

Nilishawahi kumkopesha mmoja wa kaka zake 20M baada ya kuniomba, na nikamuambia anirejeshee 5M tu, tena mambo yake yakikaa vizuri, mpaka leo hajanipa hata mia na alisha 'solve' suala lake. Hela hii alinikopa ili aende akagomboe vitu vyake ikiwemo 'assets' mara baada ya kushikiliwa kutokana na uzembe wake 'I can call it that', sasa maneno yanatoka wapi?

Kwa sababu ya haya na mengine mengi, nimefikia hatua ya kupitisha rasmi sasa ndugu wa mke wangu kutojihusisha kwa chochote kwenye biashara zangu.

Kama najitoa kwao likitokea tatizo sasa kwa nini wasiwe na shukrani? Wanafikiri wana 'deserve' sana mimi kuwapiga 'tough'?

Uamuzi wangu nilifikiri uwe ni huo. Nakaribisha ushauri kutoka kwenu pia kwenye masuala haya.

NB: maneno ndani ya funga semi ni ya lugha ya kiingereza.
 
Hakuna ulazima wa kuwaingiza kwenye maisha yako
Tena sio hata lazima uwasiliane nao
Waheshimu na kuwasaidia wazazi tu (kama uko nao karibu)

Wasikuangushe na kukurudisha nyuma kwa uzembe wao, fanya maamuzi magumu na waambie ukweli wakikuuliza msaada
Ahsante sana, ni ngumu ila nitaichambua hii nayo.
 
Nakutakia kila la kheri
Kuna wakati lazima uangalia maisha yako tu na familia yako kwani wao wanakutegemea wewe I mean watoto na future yao
Waandalie chao maana hao wanaotaka chako, wanaandaa wa kwao pia tena kwa mgongo wako

Ukifeli watakucheka ndio binadamu walivyo na ukifilisika watakukimbia hata huyo mke ambae unampa hela badala aweke Bank anawapa ndugu zake.
Huyo nae atakukimbia believe me
 
Nimekuelewa sana. Penye wengi hakiharibiki kitu.
 
Jumatatu njema kwenu nyote!.

Hapo kabla kulizuka maneno maneno mengi mno kwenye familia yangu hasa kutoka kwa kaka zake mke wangu. Maneno hayo yalihusu mimi kuwatenga na kutowakumbatia kaka zake hasa wakubwa, pamoja na wadogo zake kwenye miradi yangu ya kiuchumi.

Sikufanya haya kwa bahati mbaya, hii ilitokana na ukweli kwamba ndugu zake mapema mno walianza kuingilia familia yangu kiuchumi, from nowhere nampa mke wangu 500000 aniwekee tu ili nimpime, unakuta katoa yote kampa kaka yake na kabaki na 50000 tu. Namuuliza samahani na kujiliza kunakuwa kwingi mno.

Hapo nilikuwa najifunza kitu. Sasa timefungua mradi mkubwa sana mpya, nimeajiri watu tofauti kabisa na yeye alipendekeza wawe kaka zake 'atleast' watatu 'on top of management', hili nililikataa.

Mke alinielewa sasa tangu hapo nasikia maneno maneno ya kunisema mno, na sijui shida hasa ni ipi. Kama ni fedha huwa nawasaidia wakikwama tena kwa roho safi kabisa, siyo pesa tu, ni pesa nyingi sana.

Shida ni kwamba wanasema nawatenga, kwa sababu siwahusishi na biashara zangu. Najiuliza nawatenga kivipi? Mbona wakati wa matatizo nawajibika bega kwa bega pamoja nao? Kwa nini wanafikia kunichukia kwa kunisema vibaya?

Nilishawahi kumkopesha mmoja wa kaka zake 20M baada ya kuniomba, na nikamuambia anirejeshee 5M tu, tena mambo yake yakikaa vizuri, mpaka leo hajanipa hata mia na alisha 'solve' suala lake. Hela hii alinikopa ili aende akagomboe vitu vyake ikiwemo 'assets' mara baada ya kushikiliwa kutokana na uzembe wake 'I can call it that', sasa maneno yanatoka wapi?

Kwa sababu ya haya na mengine mengi, nimefikia hatua ya kupitisha rasmi sasa ndugu wa mke wangu kutojihusisha kwa chochote kwenye biashara zangu.

Kama najitoa kwao likitokea tatizo sasa kwa nini wasiwe na shukrani? Wanafikiri wana 'deserve' sana mimi kuwapiga 'tough'?

Uamuzi wangu nilifikiri uwe ni huo. Nakaribisha ushauri kutoka kwenu pia kwenye masuala haya.

NB: maneno ndani ya funga semi ni ya lugha ya kiingereza. Huwa nafikiria mengi mno, na hawa kaka zake ni kutoka mkoa ule karibu na Tanga, wilaya ile inayoanza na herufi M na kuishia na herufi E.
Piga chini ushemeji wa kiwaki...
Waambie kama ni vyepesi watafute na zao kama ni rahisi....
😊😊😊😊
 
Kama ndoa ilivyopoteza thamani hata yale mahusiano yanayotakana na ndoa hizi yamekosa mashiko.

Zamani ilikuwa mkwe/shemeji aliyeoa binti wa familia anaheshimika kupita maelezo. Nyumbani kwa mtoto wa kike hata wazazi wake hawapazoei kizembe achilia mbali kumzoea mume wake. Lakini sasa hivi si ajabu kukuta mama mkwe anahamia kwa mtoto wa kike na kushinda na kitenge kimoja huku mume wa mwanawe akiwa hapo hapo.

Kwa wepesi kabisa mipumbavu iliyokosa dira ya maisha inaona ni halali kuwa sehemu ya mali ya mtu ambae nasaba pekee waliyokuwa nayo kwake ni kuwa ameoa dada yao. Hawa ndio design ya watu mwanaume akikata moto tu wanakuja kufukuza watoto wote na kudai mali ni zao.

Ukweni kwako ni washenzi, kaa nao mbali kabisa. Wanaweza hata kukuua sababu ya mali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom