Anatishia kunywa sumu au vidonge

Choosen85

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
563
1,364
Wakuu hamjambo....

Sasa Kuna jambo limetokea nyumbani kwangu ninaishi na mwanamke ambaye sijafunga naye ndoa lakini pia yupo Mdogo wake wa kike ambaye amekuja kujiendeleza mambo ya ushonaji.

Sasa ninapotoka asubuhi kwenda kazini Huwa ninatoka na Mdogo mtu ambaye Huwa anaelekea huko kwenye ushonaji maana tunaelekea uelekeo mmoja.

Kumbe jambo Hilo linamkwaza sana dada mtu ingawa hasemi yaani ninamaanisha dada mtu hataki niongozane na Mdogo wake.

Matokeo yake dada mtu amekuwa akipiga simu kwao kisirisiri akiongea mambo ya uwongo kuhusu Mdogo wake pamoja na Mimi lengo likiwa Mdogo wake apigiwe simu kwao kwamba aondoke hapa arudi nyumbani huko kwao kwenyewe mambo ni magumu maana ni kijijini hata dada mtu mwenyewe tu hataki kupasikia.

Niwe mkweli ninaishi nyumba ya kupanga na ndo mwaka wa 3 Toka nimeanza maisha Nina chumba na sebule Sasa Mdogo mtu alipofika sikutaka mambo mengi niliruhusu vitu vyake vyote kuwekwa chumbani na akitaka kujiandaa aingie chumbani ajiandae kasoro kulala tu. Imekuwa hivyo Toka amekuja hapa hata mwezi haujaisha.

Cha ajabu juzi dada mtu ananitumia sms anasema hataki kumuona Mdogo wake anaingia chumbani aisee nilikataa kbs nikamwambia Hilo zoezi halitafanyika maana Toka amefika hapa chumbani amekuwa akiingia mara Kwa mara na hakuna tatzo halafu Leo ghafla tu tumwambie usiingie chumbani unadhan atahisi nn pili sebuleni kumejaa hata godoro lenyewe kumtandikia tunamtandikia Kwa kujibana je vitu vyake tuvihamishie sebuleni vikae wapi nikasema hapana.

Akalalamika sana mi nikabaki na msimamo wangu. Sasa ameanzsha tabia ya kumpeleleza Mdogo wake Kila akirudi huko kwenye ushonaji kujua kama Kuna nn tumeongea na Mdogo wake au huko kwenye ushonaji mambo Yako sawa ila lengo lake anataka asikie mambo hayako sawa ili apige simu kwao kusema kwamba huyu dogo huku hakuna anachokifanya arudi home tu.

Nilipoligundua Hilo nilimpa angalizo mdogo mtu maana nimeshangaa sana huyu mwanamke mpaka simu yake ameweka password mpya ghafla wakati alikuwa hawekagi nikagundua Kuna jambo linaendelea hapa.

Jana wakati naondoka na mdogo mtu nikamwambia anipe simu yake aliponipa nilikuta sms nyingi sn za dada ake akimuhoji kama SI kumpeleleza akinizungumzia Mimi niliumia sn mbaya zaidi sms zngn zimeandikwa usku na Mimi nikiwemo ndani yaani amemchatisha Mdogo mtu sms usiku wakinizungumzia Mimi.

Nilipogundua haya yote mi nimechukua hatua za kunyamaza kimya tu siongei na mtu sjibu mtu Wala siulizi chochote Kwa mtu humu ndani na Wala sili humu ndani Wala siitikii salamu ya mtu nipo busy na mambo yangu tu.

Usiku dada mtu analia eti ye ikibidi atakunywa hata sumu au vidonge mimi skujibu.

Line za simu alizokuwa anatumia nilimsajilia Mimi nazo nimechukua maana SI ndio hizo anatumia kunizungumzia Mimi.

Na nimetoa msimamo akiondoka Mdogo mtu kisa visa vya dada ake basi nitaamini pia huyu mwanamke hawezi kuishi na ndugu yangu Wala kuishi na Mimi kama ameshindwa kuishi na Mdogo wake wa damu kwaiyo na yeye ataondoka so achague Moja.

Sasa wakuu nimekosea wapi hapo kosa langu ni lipi?
 
Saa 11 alfajiri mtu anapost magumu ya kuishi na mwenzake A.K.A ndoa.
Mkiambiwa msioe "Mnakuja na essay humu za kutuita mashoga na LGBT (sijui ndio inaandikwa hivyo)"" na wengine wanakwambia eti ""Tumelelewa na single mazas""

Ila, mtajuana wenyewe na hizo ndoa zenu za sogea tuishi mi nachojua ""Nitafute hela ili nisipange kwenye nyumba na chumba na sebule, bali nikapange upande mzima Makumbusho au Sinza""

#YNWA
 
Nikuulize swali kaka, mdogo mtu unamla?

Kama unamla endelea ila itaku cost na kama humli basi wewe ni chizi kaka. Yaani unagombana na mkeo sababu ya kumkingia kifua mdogo wake? Asee we sio mzima.

We unaona Sawa binti mkubwa kushea chumba na nyie? Yaani michupi Yake kuweka humo akitoka kuoga kuvalia humo dah! Ingekuwa Kuna limwanaume linafanya hivyo ungeridhika?

Mtu aliyezaliwa nae tumbo moja hamtaki ila wewe baki unamng'ang'ania
 
Mwanangu huna akili yaani umpishe shemeji avalie chumbani.

Ungemwachia sebule ilimtosha, anakoogea avalie huko huko

Yanini kubeba majukumu mengi huku pesa za kupanga hata vyumba vitatu hauna?

Kwani huko kwao ameshindwa kusoma hiyo cherehani?

Huyo mkeo akomae vinginevyo hana ndoa, nina experience.
 
1. Kuhusu kuzuia mdogo wake asiingie chumbani, huna sababu ya kukataa. Mwambie amwambie yeye mwenyewe. Wewe usihusike.

2. Acha kuongozana na mdogo wake. Kila mtu aondoke kivyake. Hilo pia linakushinda?

3. Acha mawasiliano ya karibu na mdogo wake. Kushika shika simu ya mdogo wake ya nini? Kufuatilia mazungumzo yao ya nini? Kua mwanaume, fanya yako.

4. Wanawake ni territorial na hawamuamini mwanamke mwingine yoyote kua karibu na mume wake na wanajua kwamba wanaume ni washenzi hawachukui muda kuwatafuna hao wanawake. Hivyo ana haki ya kujilinda dhidi ya mdogo wake.

5. Muombee mdogo wa mke wako sehemu ya kulala, kama unaishi na majirani vizuri huwezi kukosa jirani ambae ana nyumba yenye nafasi ukamuombea dogo mahala pa kulala mkapunguza misuguano.

6. Unaonekana uko interested na dogo, basi mpangie mtaa mwingine ili umchakate bila kipingamizi.

7. Endelea kupambana mkuu, one day utamiliki nyumba kubwa, yenye nafasi na utakaribisha wageni zaidi nyumbani kwako. Unaonekana una roho nzuri ya kibinadamu.
 
Kuna uwezekano mkubwa kama mwanaume akioa binti wa kwanza kwenye familia yenye mabinti wengi basi uwezekano wa kuwapitia wadogo zake wote unakuwa mkubwa pia kama mwanaume hatakuwa na mipaka na kumheshimu mke wake.

Mara nyingi mabinti wanavutiwa sana na mume wa dada yao na wanatamani waone ana nini cha ziada mpaka akaoa dada yao. Nafikiri mke wa jamaa analijua hili
 
Nawasi wasi na umri wako bro, utakuwa bado una umri mdogo hivyo una upeo mdogo wa kuelewa mambo.

Huyo mwanmke yupo sahihi kabisa, anajaribu kulinda mauhusiano yenu kuepuaha usilete mambo ya aibu ya kutembea na mtu na dada yake.

Angeweza hata akawaambia kwao kuwa unatembea nay mdogo wake wakamrudisha nyumbani tu ila amekustili sababu anakupenda.
 
Katika vitu ambavyo inatakiwa uepuke ni kuruhusu watu kuingia katika chumba chenu unacholala na mke/ mume wako. Si mashemeji wala mama, baba hata watoto wako kuna umri wakifika hawatakiwi kuingia huko. Kaa chini na mkeo muangalie namna ya kufanya.
 
Saa 11 alfajiri mtu anapost magumu ya kuishi na mwenzake A.K.A ndoa.
Mkiambiwa msioe "Mnakuja na essay humu za kutuita mashoga na LGBT (sijui ndio inaandikwa hivyo)"" na wengine wanakwambia eti ""Tumelelewa na single mazas""

Ila, mtajuana wenyewe na hizo ndoa zenu za sogea tuishi mi nachojua ""Nitafute hela ili nisipange kwenye nyumba na chumba na sebule, bali nikapange upande mzima Makumbusho au Sinza""

#YNWA
"Hivi umesoma huko juu aliposema sijafunga nae ndoa"
 
1. Rudisha line zake.

2. Mwanaune ni msimamo sio kununa.

3. Kama hakuna ulazima msiongozane.

4. Mpe heshima mke wako hata kama huna dhambi.

5. Jua mke ana nafasi yake hata kama ana uzaifu.

6. Achana na umbea wa wanawake.

7. Hukuwa na sababu ya kusoma hizo message.

8. Acha ujinga, kama hakufai muache.
 
Back
Top Bottom