Hapa mke wangu kanidanganya

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,578
3,148
Wakuu habari za uzima?

Leo jumamosi imeambatana mvua kubwa sana kwa maeneo ya dar es salaam.

Mke wangu aliamka saa11 alfajiri kutengeneza maadazi, sasa kipindi anatengeneza akaanza stori zake kwenye biblia.

Yeye: unajua mme wangu miongoni mwa stori nzuri za kwenye biblia ni kisa cha yesu alipovuka nga’mbo na kwenda kwenye mji wa wagerasi

Mimi: uzuri wake ni upi kisa hicho mgerasi?

Yeye: akacheka.... yesu alipofika katika mji wa wagerasi ambao sifa yake kubwa ulikuwa ni ufugaji wa nguruwe alikutana na mtu aliyepagawa na mapepo aliyeishi mapangoni, mtu yule alipomuona akamkaribia akasema, eheee mwana wa mungu tumekukosea nini? Yesu akamuuliza unaitwa nani? Akajibu LEGIONi ikiwa na maana ya jeshi. yale mapepo yakasema bwana ukitutotoa usituridishe shimoni bali turuhusu tuingie nguruwe wale. Naye yesu akawamuru watoke na wakaliingia kundi lile kubwa la nguruwe.

Mimi: sasa mgerasi kilichokufurahisha ni nini hapo?
Yeye: unajua shetani huwa anajiona yeye ni mjanja, lakini yesu alikuwa mjanja zaidi yake,

Mimi: kivipi?
Yeye: kwanza shetani alifahamu mji ule unathamini nguruwe kuliko mtu yule ambaye aliishi mapangoni akiwa na mapepo, mbili alijua nguruwe hawawezi kuogelea hivyo pindi watakapowaingia kundi lile la nguruwe lililokuwa karibu na bonde la maji watakufa wote....

Mimi: kwahyo yesu alifanya makubaliano na shetani ili aharibu uchumi wa mji ule?

Yeye: Shetani huvamia(attack) kitu ambacho unakithamini alijua kwa kufanya vile watu wa mji ule wangekasirika na na kumfukuza na ndicho kilichotokea, lakini pia shetani hakufahamu kwamba hata yeye angeangamia na kundi hilo la nguruwe lililozama.

Mimi: kwani yesu alishindwa kuwatoa pasi na kuharibu mali za mji ule?
Yeye:mume wangu katika kusoma kwangu sikuwahi kuona ukombozi ambao haujambatana na gharama, ukombozi lazima uwe na gharama.

Mimi: kwahyo shetani aliangamia na nguruwe wale kwenye maji?
Yeye: kabisa... na hilo ndio lililoleta ukombozi kwa mtu yule aliyeteseka.

Nikamwambia wewe kilichobaki ni kwenda kwa mwamposa tu embu endelea kutengeneza maandazi.

Ndugu zangu wana JF wakazi wa dar es salaam hali ya mvua sehemu unapoishi ipoje hapo?
Hapa mtaani ninapoishi nyumba mbili fensi zimeanguka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom