Mke wangu hana hobby ya kitu chochote

Mke wangu hana hobby ya kitu chochote

. Nimerudi

Umepata nyumba ndogo mpaka leo unamuona mkeo yupo tofauti?

Si bure

Mwezi uliopita ulimnunulia urembo gani mkeo? Nguo? Ulimpeleka saluni

Maana kama unaona hana interest umpeleke hadi azoee

Akishazoea usirudi hapa kulalamika jinsi ya kumwachisha
 
Kwanza niwatakie lunch njema. Kabla hatujaoana aliniorodheshea hobbies zake kama kusafiri, kuangalia tamthilia, movies, usafi wa ndani na mazingira ya nje, outing. Tumeingia kwenye ndoa mwaka wa 5 sasa hayuko interested na kitu chochote. Jumatatu hadi ijumaa yuko busy kazini. Jumamosi anaenda sokoni kufanya shopping. Jumapili kwenye ibada. Nikimuliza ni wimbo gani anaupenda uwe wa dini au kidunia hajui manake hapendi kuangalia hata tv, hata taarifa ya habari huwa namlazimisha. Hajui kujiremba anavaa kawaida sana. Nikimwambia outing anasema bora hiyo hela tununue chakula tupike hapa nyumba. Hata usafi wa nyumba sio wa kiviile saana. Yeye akiona watoto wameoga wameshiba ndo starehe yake basi, hata kuwatembelea marafiki huwa namlazimisha. Nimejaribu kumuliza hana jibu...anaona kama namuonea na siyo kwamba anachoka sana iwe ndo sababu kwani msichana wa kazi tunae. Na sio kwamba tuna umri mdogo hapana, tulioana tukiwa na umri wa kuitwa mama na baba. NISHAURINI NIMESHINDWA KUMWELEWA HUYU MKE WANGU
Anayo hobby...wewe ndo hujaijua tu....
Do ur homework broo....
 
1. Ni HOBBY sio obby!
2. Nani alikudanganya kuwa wewe ndie uko sahihi???
Kwamba wewe hobby zako ndizo nzuri na zafaa kuwa mfano wa kuigwa na mke wako. Nina mashaka na uelewa wako wa: a)ndoa b) maisha ya ndoa c)mwanamke mwema

Ninaona unafiki wako katika bandiko hili - hujasema yote yanayokukera!
a)Hana bashasha kwenye tendo la mahaba!
b) Haongei na wewe muda unaotaka
c) halalamiki ukifanya nae mapenzi
d) ana marafiki wa ajabu ajabu ambao labda sio dot com kama ambavyo wewe ungetaka
e) Yuko basic sana kwenye maongezi na unaona kama anakutia aibu unapokuwa na marafiki zako.

*I believe that you are the one who is supposed to change and find a common line where you can draw a line and make a decision to start together.
I also think kwamba wewe ulikaa kijijini muda mrefu na labda unatamani kuifuta historia yako ya huko nyuma - lakini kufanya hivyo sio lazima mke wako awe hivyo unavyotaka (maana unavyotaka wewe sio maisha ya ukweli (it isn't real!)

* Kwanza umechelewa kuamuakwamba ungetaka mwanamke wa aina gani - umeingia kwenye ndoa na huna msimamo wa kuwa unataka mke au ndoa ya aina gani au mke wa aina gani.

Unabuni misimamo kwenye maisha kadri unavyokwenda mbele - huna picha yako ya maisha kuwa unataka nini, huna unachosimamia. As a result unadhani tatizo sio wewe - unaamini tatizo ni mke wako ( Utaishia kuwa na maisha ya huzuni na kukosa furaha kwa kuwa unaamini furaha yako anayo mke wako au mtu mwingine!
utanielewa tuu!!!!
 
Kaka mshukuru Mungu kwa kukupa mke asiye na makuu kama huyo. Ungepata mke mcharuko ungeumiza kichwa. Kumbuka hobbies nyingi zinaendana na gharama ambazo ukiwa wa kiume ni shurti uzitimize. Na kibaya zaidi hobbies nyingine haziendani na maadili yetu ya ki-Afrika. Kumbuka hobbies nyingi ni za kuiga kutoka magharibi. Haina maana zote ni mbaya, la hasha. Kuna zilizo nzuri lakini ukweli ni kuwa zipo nyingi ambazo hazistahili kwa mazingira yetu. Na kwa bahati mbaya wa-Swahili tukiiga tunaiga mzima mzima bila kupembenua lipi linafaa na lipi halifai. Imefika hatua hakuna tofauti kati ya aliyeoa/olewa na asiye-oa/olewa kwani wote wanafanya yale yale tu tena bila kuficha. Wazungumzaji wa ki-ingereza wanaita "Identity Crisis".
 
Oya nlivyoona "obby" kwenye title ya thread nikawa nna hamu kujui ni nini?
Kumbe "hobby"! Dah

unamkumbuka yule 'obby' wa kwenye gazeti la sani? mi ndo nilidhani mwenyewe
 
Pole.mpendane tu mpaka kifo kitapowatenganisha.
 
Kwanza niwatakie lunch njema. Kabla hatujaoana aliniorodheshea hobbies zake kama kusafiri, kuangalia tamthilia, movies, usafi wa ndani na mazingira ya nje, outing. Tumeingia kwenye ndoa mwaka wa 5 sasa hayuko interested na kitu chochote. Jumatatu hadi ijumaa yuko busy kazini. Jumamosi anaenda sokoni kufanya shopping. Jumapili kwenye ibada. Nikimuliza ni wimbo gani anaupenda uwe wa dini au kidunia hajui manake hapendi kuangalia hata tv, hata taarifa ya habari huwa namlazimisha. Hajui kujiremba anavaa kawaida sana. Nikimwambia outing anasema bora hiyo hela tununue chakula tupike hapa nyumba. Hata usafi wa nyumba sio wa kiviile saana. Yeye akiona watoto wameoga wameshiba ndo starehe yake basi, hata kuwatembelea marafiki huwa namlazimisha. Nimejaribu kumuliza hana jibu...anaona kama namuonea na siyo kwamba anachoka sana iwe ndo sababu kwani msichana wa kazi tunae. Na sio kwamba tuna umri mdogo hapana, tulioana tukiwa na umri wa kuitwa mama na baba. NISHAURINI NIMESHINDWA KUMWELEWA HUYU MKE WANGU

Mkuu hapo kwenye bold: Unadhai ni kitu kidogo hicho? Kumbuka kuwa mke wako
1. amekuzalia watoto (bila watooto msingeishi kwa jinsi ninavyokuona)
2. anakutunzia watoto, anakulelea watoto
3. anakupikia chakula
4. anakupikia
5. anakufulia nguo mpaka c.h.u.p.i yako
6.anafanya kzi ofisini
7. anakusaidia budget ya matumizi nyumbani, n.k nk nk list ni ndefu.
Leo umesahau yote hayo, unadiriki kuleta issue public hapa unamsema vibaya mke wako, kisa pengine alikuambia kuwa anapenda kucheza karata lakini sasa hachezi!

Hii midude mingine mipumbafu Mungu ameijalia wake lakini hata haina shukrani. Ukiendelea hivi utakuja kupata shida sana katika maisha yako. Roho mbaya sana kupita kiasi hii!
 
papuchi si unapewa?hebu tosheka na ushukuru mungu
 
Habari za ndoa huwa zanipa raha! Haya walimwengu mso na shukrani, lalamikeniiiiiiiiii mpaka, ukija shtuka wenzio wa nje , walishazisoma hobbies na mke wamebeba!
 
Hakuna cha wife material, huyo ni anti social tu, nyie ndio mnaooa mazezeta ili wawasikilize kila mnachowaambia...
hebu nitake radhi, aliyekwambia mimi ninaoa ni nani? akili yako inakwambia kila aliyeko humu ni mwanaume?
 
hiv kuwa na hobby nako kuna kuza mapenzi?
 
Back
Top Bottom