Mke wangu hana hobby ya kitu chochote

Mke wangu hana hobby ya kitu chochote

Mkeo hobby anazo nyingi ila haziendani na zako.
 
Ebu nipe namba yake ili niongee nae!!!
Pengine we unamnyanyapaa!!!!!
 
daaaahh....wewe kaka hebu shukuru mungu wakooo kwa mke aliyekuatia.. au kama vipi mpe talaka mim nimuunganishie na kaka yangu aliyebambikiwa watoto wawili ndani ya ndoa na mwisho akamfumania na houseboy wake na kuachana kwa matusi na kejeli..hope akimpata mkeo akili ake itatulia.. pia kuna mtu kapigwa na shoka la kichwa na mkewe ili afe mke arithi mali baada ya kudanganywa na wenzake kwenye vikao vyao vya umbea...NARUDIA TENA SHUKURU MUNGUUUUUU...
 
Mmmh hii kali, mtu wa aina hii ni tabu kuishi nae mpaka uzeeni. Maana utakuwa umekufa longtime bado kuzikwa. mwambie abadilike....kidogo.
 
Kwanza niwatakie lunch njema. Kabla hatujaoana aliniorodheshea hobbies zake kama kusafiri, kuangalia tamthilia, movies, usafi wa ndani na mazingira ya nje, outing. Tumeingia kwenye ndoa mwaka wa 5 sasa hayuko interested na kitu chochote. Jumatatu hadi ijumaa yuko busy kazini. Jumamosi anaenda sokoni kufanya shopping. Jumapili kwenye ibada.

Nikimuliza ni wimbo gani anaupenda uwe wa dini au kidunia hajui manake hapendi kuangalia hata TV, hata taarifa ya habari huwa namlazimisha.

Hajui kujiremba anavaa kawaida sana. Nikimwambia outing anasema bora hiyo hela tununue chakula tupike hapa nyumba. Hata usafi wa nyumba sio wa kiviile saana.

Yeye akiona watoto wameoga wameshiba ndo starehe yake basi, hata kuwatembelea marafiki huwa namlazimisha.

Nimejaribu kumuliza hana jibu anaona kama namuonea na siyo kwamba anachoka sana iwe ndo sababu kwani msichana wa kazi tunae. Na sio kwamba tuna umri mdogo hapana, tulioana tukiwa na umri wa kuitwa mama na baba.

NISHAURINI NIMESHINDWA KUMWELEWA HUYU MKE WANGU

Kumbe unapenda awe anasafiri sana, atake outing sana, ajirembe sana, apende nguo za gharama? Wenzio wenye wake wenye tabia hizo wanalia kila kukicha. Sehemu haina kidonda unapaka dawa, sijui kidonda kikitokea utapaka nini!
 
Wenzie tunataman tusafiri dunia nzima kujionea mambo,ila ni vizuri mbonaaa mke mtulivu furahiaaa wenzio wanaumwa kichwaa mke kila siku yupo kwenye taarabu,harusi,vigodoro ohooooooio
 
Mi ningekuwa na mke kama huyo ningefurahi sana.

Mke asiye na usumbufu wa vi"obby" safi sana. Ogopa kuwa na mke mwenye "obby" ya kulala misibani, kugegedwa mchana, kuiba vijiko bar, au mpenzi wa ngumi na kareti.
Asprin
Umenchekeshaaaaa loh
 
Last edited by a moderator:
haya we ng'ang'ania kutaka kuijua hobby yake siku ukiijua na talaka juu usisite kuja kutujuza.
acha chokochoko hizo akikata kamba kijasho kitakutoka.
 
Shukuru Mungu kwa huyo mkeo,wa kwangu ana hobi ya kioo, hadi mboga jikoni inaungua yeye emeshika penseli anajichora "zebra"kwenye kope!
 
Back
Top Bottom