Mke wangu hana hobby ya kitu chochote

Mke wangu hana hobby ya kitu chochote

>wengine mnajaaliwa wake wazuri lakini wenyewe ni vicheche.. Ungekuwa hujamzalisha ningekuomba nimuoe mimi!
 
Najua kwa michango yote hii umeelewa wapi ulikosea, na kipi cha kufanya.

Tena usicheze na hii mambo ya Hobby kabisa, cheza mbali. Kuna hobby kama za ngoma, kupenda zawadi (shopping ya nguo nguo), kupenda kukaa na mashost wanapiga umbea, wee!

Unless uliingia kwenye ndoa ukiwa hujamaliza ujana, utamlalamikia huyu, otherwise mshukuru Mungu aisee.
 
Ama kweli kwenye miti hakuna wajenzi!!!!!!!!!!!!

Ningekutana na mwanamke huyu ningejihesabu mwenye bahati kubwa!!!!!
hivi ndoa si zaidi ya kazi?? sio sisi tunawashauri watu kila leo wawatoe out wapenzi wao??
 
Umepata mwanamke bora kabisa ktk hii dunia, mwenye hobi ya kumkumbuka mungu na sio mambo ya kidunia au tubadilishane na hili gumegume langu nini?
 
aisee una wakati mgumu pole ila utazoea tu kila binadamu ana mapumgufu yake ndoa ni kusaidiana na kubebeana mizigo basi beba mzigo huo wa mkeo you never know hata wewe kuna vitu unamkera na ni kweli kama unamlazimisha ina maana una muuzi ila anakuvumilia kama mume wake
 
Kwanza niwatakie lunch njema. Kabla hatujaoana aliniorodheshea hobbies zake kama kusafiri, kuangalia tamthilia, movies, usafi wa ndani na mazingira ya nje, outing. Tumeingia kwenye ndoa mwaka wa 5 sasa hayuko interested na kitu chochote. Jumatatu hadi ijumaa yuko busy kazini. Jumamosi anaenda sokoni kufanya shopping. Jumapili kwenye ibada. Nikimuliza ni wimbo gani anaupenda uwe wa dini au kidunia hajui manake hapendi kuangalia hata tv, hata taarifa ya habari huwa namlazimisha. Hajui kujiremba anavaa kawaida sana. Nikimwambia outing anasema bora hiyo hela tununue chakula tupike hapa nyumba. Hata usafi wa nyumba sio wa kiviile saana. Yeye akiona watoto wameoga wameshiba ndo starehe yake basi, hata kuwatembelea marafiki huwa namlazimisha. Nimejaribu kumuliza hana jibu...anaona kama namuonea na siyo kwamba anachoka sana iwe ndo sababu kwani msichana wa kazi tunae. Na sio kwamba tuna umri mdogo hapana, tulioana tukiwa na umri wa kuitwa mama na baba. NISHAURINI NIMESHINDWA KUMWELEWA HUYU MKE WANGU

Wewe na watoto ndio hobby zake.........big up kwake......ogopa kuwa na mke kama hawa wenye "hobbies" za ajabu!

IMG_5472.jpg
 
Wewe shukuru mungu kwa kupata mke mwema, wenzio wanalia wanaibiwa pesa na wake zao wanaenda kustarehe, jaman watu wengine kwel iiii kabsaaa hizo nazo ni shida za kulalamikia au unatuchoraaa tuuuuu.
 
Sometimes huwa nashindwa kuwabebea mbeleko gani baadhi ya wanaume jamani
 
kua mbunifu na fanya tafiti ujue kipi kinachompa furaha na kifanye kisiwe kwa kawaida ila fanya kwa Muonekano tofauti.....kuwa nae muda mwingi pia kumbuka kipindi cha nyuma ulivyokua unamtokea alikua anapendelea nini hapo utaelewa nini cha kumfanyia...
 
Usipende unavyohisi au unavyotaka nae awe hivyo watu tunatofautiana. Huyo ni bonge la mke we mpe yale mambo yetu vizuri mpk adevelop hobby.
 
Back
Top Bottom