Pole ndugu, ila nliwahi shauriwa kuwa kama huna kifua kaa mbali na simu ya mwenza wako, mi nakuomba fanya yafuatayo, toka naye out siku moja jua wewe na yeye, ikiwezekana hata chukua weekend moja hotelini, wakati mnainjoi embu jaribu kupeleleza kama kuna kitu ana miss kwako, nini anatamani uongeze katika mapenzi yenu, kama vipo hivyo vitu then in a polite way jaribu kumuuliza kama ndo vinafanya anachat ujinga fb, kama havipo jaribu kumuuliza politely why anafanya anayoyafanya?
Ongea naye tatua in a polite way mpe another chance, niliwahi salitiwa na mpenzi wangu niliumwa hadi kulazwa, alikuja akitubu na msamaha analia hadi alizimia ila sikuwa tayari, baadae nilijiuliza hivi ningekuwa ni mimi nimefanya hilo kosa si ningetaka kusamehewa? I believe ingehappen kwako ungetaka na wewe kusamehewa na mwenzako akupe fursa ya kujieleza why ulianguka, kama yeye amechangia au lah, na upewe a chance to make things fresh.
Victor j (MC mtumishi)
Inspirational and motivational speaker/master of ceremony