Mke wangu ananiumiza kichwa

Mke wangu ananiumiza kichwa

Mmmhh.chanzo cha hayo yote ni wewe mwenyewe! Baada ya hasira kuisha jitafakari,ongea na mkeo then delete hiyo account problem solved! Mke wa mtu unatoa wapi muda wa kuanza kuchati na vivulana loh! Huyo naye jipu ka majipu mengine tu! Mpe kerebu moja kwanza ajifunze huenda unamlea ka yai! Mwanamke hatakiwi kupewa uhuru kiivyo loh!
 
Evelyn kinachoniuma ni kwamba before sijakutana nae nilikuwa Malaya mbwa ila nlipokutana nae nikajua roho mtakatifu kanigusa na nikabadilika kabisa, nikiwaza hapa atakuwa ameshanisaliti mara ngapi mpaka hivi leo? Kazi yangu yenyewe ni mikoani mara kwa mara naweza kaa mkoani hadi miezi mitatu kama project ni ndefu kiaina...hapo Kati atakuwa ameshakung'utwa vya kutosha, kama Facebook anajirahisi kiasi hichi vipi vijana wa hapa mtaani? Naweza kuwa nasalimiana na vijana wenzangu mtaani kumbe wananicheka wanavyonimegea mke wangu, sijui naanzia wapi kuongea nae, Nina hasira za karibu na sijawahi mpiga hata siku moja, nahisi Naweza fanya kitu cha ajabu....kichwa kinaniuma vibaya hapa
Ha ha ha ha ha haaa, nacheka kama mazuri. It's pay back time beibe, mara nyingi unayemtumikia ndo anakupa ujira hivyo usitegemee kumtumikia shetani halafu asikupe mwanamke wa kambi yake we nani.
hakuna unachobadilisha kwa kupaniki kama ameliwa ameliwa tu ila uzuri wamekubakishia hawajaondoka nacho.
Mwambie umeona hayo mawasiliano uone anasemaje, anaweza kuwa anachati nao tu
 
duh.... mkubwa pole sana. mie hapa sisemi chochote,,,, nashauri tuu usiguse simu ya mkeo wala asiguse yako..... kuna mahali umesema ulikuwa malaya mbwa -----ndege wafananao..............
 
Habari za jumatano wanajamvi, bila shaka mmeamka salama kabisa.

Leo nimekuja huku kuomba ushauri maana tangu usiku sijalala kichwa kinawaka moto.Nimeoa miaka minne ilitopita, kabla ya hapo niliambiwa kabila la Mbulu sio la kuoa mie moyo ukawa umenasa hivyo na pete kanisani ikavaliwa. Nimebarikiwa mtoto mmoja wa kike.

Mwaka 2011 nilimfungulia account facebook mchumba kabla sijamuoa na nilikuwa namuamini sana.Tatizo Jana (Jumanne nikiwa kazini akaniambia account yake imesumbua halafu njia ndio mie hivyo nikiwa kazini nikalog in kwenye account yake (ikumbukwe tangu nimuunge sijawahi ingia kwenye inbox wala kugusa simu yake) baada ya kumrekebishia tatizo lake nikaona niingie inbox kwa mara ya kwanza.

Ukweli mie sinywi pombe lakini Jana nilijikuta naondoka kazini mapema na kwenda kuzimua kichwa. Nimekuta message nyingi anachat na vijana za ajabu ajabu mara mume wangu nitamuaga naenda kwa ndugu nitakuja kwako, mara mume wangu hayupo halafu nipo kitandani peke yangu baridi kali, Mara nimetoka kuoga ndio najifuta now, halafu anagawa namba yake ya simu kirahisi kwa kila anayemuomba namba. Yaani nusura nianguke ofisini maana mpaka wenzangu wamejua kuna tatizo ila sijafungua mdomo wangu.

Nimerudi nimemkuta ananichekea yani sijaongea kitu roho inaniuma vibaya, nahangaika kutoa jasho kwaajili ya kumpendezesha na mtoto wetu ila kaniona boya. Wakati naanza uhusiano nae nilikuta akiwa na elimu ya darasa la saba tu, nikamuendeleza QT na kumfundisha mpaka now ana diploma na October anaingia degree, sijui hata nifanye nini haki ya Mungu inanitesa sana.
wakulaumiwa ni we mwenyewe,,,umemfundisha panya kula pamba,wakati godoro lako ni la sufi.
 
Pole ndugu, ila nliwahi shauriwa kuwa kama huna kifua kaa mbali na simu ya mwenza wako, mi nakuomba fanya yafuatayo, toka naye out siku moja jua wewe na yeye, ikiwezekana hata chukua weekend moja hotelini, wakati mnainjoi embu jaribu kupeleleza kama kuna kitu ana miss kwako, nini anatamani uongeze katika mapenzi yenu, kama vipo hivyo vitu then in a polite way jaribu kumuuliza kama ndo vinafanya anachat ujinga fb, kama havipo jaribu kumuuliza politely why anafanya anayoyafanya?

Ongea naye tatua in a polite way mpe another chance, niliwahi salitiwa na mpenzi wangu niliumwa hadi kulazwa, alikuja akitubu na msamaha analia hadi alizimia ila sikuwa tayari, baadae nilijiuliza hivi ningekuwa ni mimi nimefanya hilo kosa si ningetaka kusamehewa? I believe ingehappen kwako ungetaka na wewe kusamehewa na mwenzako akupe fursa ya kujieleza why ulianguka, kama yeye amechangia au lah, na upewe a chance to make things fresh.

Victor j (MC mtumishi)
Inspirational and motivational speaker/master of ceremony
hapo ni sawa na kumbembeleza,kama ana ushahidi wa kutosha kama tunda lake linaliwa,ni kumtema tu,dunia imeoza hii,msije kuvaa nepi bure!
 
Mmmhh.chanzo cha hayo yote ni wewe mwenyewe! Baada ya hasira kuisha jitafakari,ongea na mkeo then delete hiyo account problem solved! Mke wa mtu unatoa wapi muda wa kuanza kuchati na vivulana loh! Huyo naye jipu ka majipu mengine tu! Mpe kerebu moja kwanza ajifunze huenda unamlea ka yai! Mwanamke hatakiwi kupewa uhuru kiivyo loh!
shangazi umeongea kapoint kwa mbaaali,kwanini mke wa mtu akeshe mitandaoni?lakini kufuta akaunti sio dawa,atafungua nyingine kwa siri,na kama ni tabia yake ataendelea tuuuuuuu.
 
Hii dunia tunatakiwa tusifuatiliane. Waaminifu ni wachache. Acha kumfuatilia mkeo uishi kwa amani, vinginevyo unachotafuta utakipata. Wanawake hawana lebo kama ameolewa au bado. Ndio maana wengi siku hizi hawakatai, ukiongeza na ulimbukeni wa mitandao ya kijamii, wengi wanataka kuwaonesha wanaochat nao kuwa wako single. Hapo ndipo shida inapoanzia.
Usimchunguze sana kuku kwani huwezi kuendelea kumla!
 
Haya mambo yanatokana na upbringing, msiwalaumu sana wanaume wa kiafrika kwa kukosa caring, walivyokuwa wadogo hawakuona baba na mama zao wakiambiana "nakupenda" au "nisamehe mke wangu".

Mambo mengine watu hushindwa kuji tune ukubwani, laiti kama wangeyaona utotoni, wangejifunza na kuyatumia ukubwani. Mfano mimi na kukua kwangu sikuwahi kumuona baba hata kumchumu mama shavuni, hata mara moja, hivyo ni ngumu sana kufanya hivyo mbele ya watoto saivi.
Hio siyo excuse mkuu. Unaweza kumwambia mkeo hata kama wazee hujawahi kuona wakifanyiana hayo. Tatizo la wanandoa wengi ni kuwa wavivu na kutegeana mke anaona mzee hajishughulishi naa yeye anaona poa tu. Baada ya hapo hakuna anayehangaika kumfurahisha mwenzake mnaanza kuishi kama roommtes akitokea mchepuko mtu anahamia hukohuko.
 
Pole ya kawaida hayo, ongea nae delete hiyo account Facebook, jipe muda maumivu yapungue msamehe maisha yaendelee.....
Nataka kufuta account facebook lakin nashindwa nimejaribu mara kadhaa lmeishia kudiactivate kwa muda still notification Zinakuja kama kawaida
Nitumie mbinu gani niifute permanet mkuu naomba mbinu
 
Pole sana bro, ila haki ya nane tena Wambulu wengi wao ni warahisi sana,
 
Back
Top Bottom