TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,835
Habari za jumatano wanajamvi, bila shaka mmeamka salama kabisa.
Leo nimekuja huku kuomba ushauri maana tangu usiku sijalala kichwa kinawaka moto.Nimeoa miaka minne ilitopita, kabla ya hapo niliambiwa kabila la Mbulu sio la kuoa mie moyo ukawa umenasa hivyo na pete kanisani ikavaliwa. Nimebarikiwa mtoto mmoja wa kike.
Mwaka 2011 nilimfungulia account facebook mchumba kabla sijamuoa na nilikuwa namuamini sana.Tatizo Jana (Jumanne nikiwa kazini akaniambia account yake imesumbua halafu njia ndio mie hivyo nikiwa kazini nikalog in kwenye account yake (ikumbukwe tangu nimuunge sijawahi ingia kwenye inbox wala kugusa simu yake) baada ya kumrekebishia tatizo lake nikaona niingie inbox kwa mara ya kwanza.
Ukweli mie sinywi pombe lakini Jana nilijikuta naondoka kazini mapema na kwenda kuzimua kichwa. Nimekuta message nyingi anachat na vijana za ajabu ajabu mara mume wangu nitamuaga naenda kwa ndugu nitakuja kwako, mara mume wangu hayupo halafu nipo kitandani peke yangu baridi kali, Mara nimetoka kuoga ndio najifuta now, halafu anagawa namba yake ya simu kirahisi kwa kila anayemuomba namba. Yaani nusura nianguke ofisini maana mpaka wenzangu wamejua kuna tatizo ila sijafungua mdomo wangu.
Nimerudi nimemkuta ananichekea yani sijaongea kitu roho inaniuma vibaya, nahangaika kutoa jasho kwaajili ya kumpendezesha na mtoto wetu ila kaniona boya. Wakati naanza uhusiano nae nilikuta akiwa na elimu ya darasa la saba tu, nikamuendeleza QT na kumfundisha mpaka now ana diploma na October anaingia degree, sijui hata nifanye nini haki ya Mungu inanitesa sana.