Mke wangu ananifanyia vituko ili tuachane

ndoa ni msalaba cha muhimu ni kuvumiliana na kumtegemea Mungu sana, fanya biashara zako jiongezee kipato mbona atarudi mwenyew alafu usimuulize chochote wala usiguse simu yake we fanya tu yanayokuhusu ila msiachane atanyooka tuuu mkuu, msiachane watakaoumia ni watoto hasa wataumia kisaikolojia
UNAXEMA ASIMUACHE AKIMLETEA UKIMWI JE?
 
Kuoa wanawake wenye kipato au wafanyazi ni nadra sana kudumu kwenye ndoa wana changamoto xna. Mimi mwenyewe nashuhudia jamaa zangu wengi walio oa wafanyakazi wanavyolalamika juu ya maisha yenye v8sa na vituko vingi kutoka kwa wenza wao. Yaani kwa kifupi wana shida kubwa sana na wanajilaumu kwa kuingia kwenye ndoa hizo afadhali wangeoa magolikipa km sisi wengine
 
Sitisha kushirikiana nae kimwili ili kuepuka magonjwa kwa wakati huohuo ishi maisha ya kawaida hapo nyumbani ila anza kuwekeza pembeni ikiwemo kununua kiwanja nk.

Mkitengana hiyo iwe nyumba ya watoto na akitaka kuolewa aiache nyumba ya watoto akaanze upya au muiuze mgawane.

Akili kumkichwa ukilemaa umeachwa feri.
 
Kiufupi kuna wanawake huzuzuka na mijamaa mingine yumkini huyo nimmoja wao! Ninakushauri jaribu kukaa kimya na usihangaike na mambo yake, kama ni simu yake achana nayo hata ukiona sms za ajabu achana nazo wewe kuwa mpole na mkimya ila usikubali akupande kichwani! Kama una house gal, shughulika nahuyo zaidi kwa mawasiliano ya ndani ila si mawasiliano ya kimapenzi hapa namaanisha kama unahitaji kutoa hela za matumizi ya nyumbani mpe house gal kama nikwa ajili ya watoto house gal afanye kazi hizo na mkeo mwache na maisha yake japo mtakuwa ndani ya Nyumba moja.

Tena, kama ukiwa mvumilivu basi itakusaidia sana kiongozi, ipo siku hao wanaompandisha bichwa watamwona yeye mpuuzi tu na waajabu. Unajua hakuna mtu anayehitaji maendeleo ya familia nyingine usikute kuna mtu anawaone wivu jinsio mnavyoishi na yeye kwa akili zake za kimende akaingia kichwa kichwa pasipo kutafakari.
 
Mtu akisema amekuchoka anamaanisha kuanzia leo usimuulize chochote, usishike cm yake na kuhusu kuondoka mwambie aondoke yeye akuache na watto ye si ndo kakuchoka be a man bhana.
 
Hiyo nyumba mlio ijenga pamoja, haina thamani kama uhai wako ama afya yako.
Alafu......
Wewe ni mwanaume mpumbavu kupita kiwangu cha kawaida.
Yaani kwa hayo yote umeyakuta kwa mke alafu bado unaomba kushauriwa
Aina ya wanaume kama wewe ndio nawaita wanaume yogoyogo, na endelea kutafuta suluhu ili huyo mwanamke aje akuletee na maradhi kabisa.
Wenzio tulio pitia mambo kama hayo, tuliamua kujiindoa kwenye nyumba tulizo jenga tukiwa pamoja na kisha tuka waacha wafurahie maisha ya uhuru kama watakavyo. Maadam mmezaa watoto, basi usihofu kuhusu nyumba, ifanye kama ni mali ya watoto wenu na msimamizi ni mama yao.
 
ndoa ni msalaba cha muhimu ni kuvumiliana na kumtegemea Mungu sana, fanya biashara zako jiongezee kipato mbona atarudi mwenyew alafu usimuulize chochote wala usiguse simu yake we fanya tu yanayokuhusu ila msiachane atanyooka tuuu mkuu, msiachane watakaoumia ni watoto hasa wataumia kisaikolojia
Hivi.....
Kweli mwanamke ana kanyagwa, alafu nimuvumilie
Mhhhhhh......
Hili nalo litakua ni moja ya maajabu matakatifu kuwahi kutokea chini ya jua
 
hiyo ndiyo maana ya kile kiapo kuwa atakuwa naye siku zote kwa shida na raha
 
Nenda tu boss... Hawa watu wanaweza kukufanya lolote wakati wowote bila sababu yoyote
 
Mimi naisi africa kweli iq zetu ni ndo yaani mtu amekuchoka waziwazi ila we bado upo tu kwani uyo ni mama yako?
Akya shetani mimi icho kitu akitokaa kitokee kwangu
Maisha yenyewe ndo mafupi namna ii alafu nivumilie mtu? We jamaa sizani kama ni mzima
 
Mmmh!!! Pole sana, maisha haya yanachangamoto sana jaman, kwanza kabisa muombe Mungu ili upate amani ya Moyo wako, harafu ongea na mkeo kwa upole sana na hisia zote jinc gani? Hautamani hata siku moja itokee uachana naye mwambia jinc gani ana umuhimu katika maisha yako pamoja na watoto wenu, kama akiigiza haelewi mwambie akuache wewe hapo nyumbani, harafu yeye ndio aende anapokutaka lakini wewe huwezi kumuacha, Naamini inaweza kusaidia kuokoa ndoa yenu, kwa uwezo wa Mungu yote yatapita.
 
Kwanza kapime kucheki afya yako, halaf akitaka chakula cha usiku tumia mpira, ili wakati unajipanga au kujiandaa kumwachia maisha yake uwe unachunga na afya yako, Kiufupi acha kumfatilia na kama mmechokana mwambie aondoke yeye kwako na sio wewe, Labda kama hiyo nyumba ndio mmejenga wote na kuepusha kuwatesa wanao, mwache yeye abaki na watoto ila kuanzia sasa anza plan nyengine yakutafuta kwako, yani nunua eneo kwa jina lako anza maisha yako taratibu ukiwa na Amani, iko siku atarudi tu au atakutafuta, ASILIMIA KUBWA YA WANAUME WANAOCHUKUA WAKE ZA WATU, HUWACHUKUA KWA MATAMANIO TU NA SIO KAMA WANAFUTURE NAO, Kama huamini mwache halafu usikie ameolewa, utasikia kamwaga na atarudi kwa magoti, na hata akiolewa hadumu huko...pole sana
 
Back
Top Bottom