Mke wangu tuna miaka 10 toka tuoane. Kipato changu na chache hakitofautini sana, ni muda sasa tupo kwenye mgogoro wa kindoa. Kubwa ni kwamba ananifanyia vituko ili tuachane. Nimesha zikamata SMS za mapenzi za wanaume wengine kweye simu yake, nikimuuliza ananijibu alikuwa anatongozwa tu. Nimeshagombana nae sana, nimesha peleka mashtaka kwa watu wazima watusuluishe lakini habadiliki.
Last week pia karudia na nimemkuta tena na sms za wanaume za kuitana honey, darling, love nimemuuliza, tumeishia kulumbana na ananijibu nimuache, nichukue 50 zangu. Nimewaita watu wazima wa karibu na familia yangu, tumeyajadili nikijua ataacha, tulipo baki wa 2 akanijibu nisimfuatilie mambo yake. Nimezaa nae watoto 2, tumeshirikiana tumejenga nyumba. Leo hii ananitaka niondoke, nikaanze maisha kimpango wangu.
Naombeni ushauri.