Mke wangu ananifanyia vituko ili tuachane

Mke wangu ananifanyia vituko ili tuachane

DA,NDOA ZA MWENDOKASI


Mke wangu tuna miaka 10 toka tuoane. Kipato changu na chache hakitofautini sana, ni muda sasa tupo kwenye mgogoro wa kindoa. Kubwa ni kwamba ananifanyia vituko ili tuachane. Nimesha zikamata SMS za mapenzi za wanaume wengine kweye simu yake, nikimuuliza ananijibu alikuwa anatongozwa tu. Nimeshagombana nae sana, nimesha peleka mashtaka kwa watu wazima watusuluishe lakini habadiliki.Last week pia karudia na nimemkuta tena na sms za wanaume za kuitana honey, darling, love nimemuuliza, tumeishia kulumbana na ananijibu nimuache, nichukue 50 zangu. Nimewaita watu wazima wa karibu na familia yangu, tumeyajadili nikijua ataacha, tulipo baki wa 2 akanijibu nisimfuatilie mambo yake. Nimezaa nae watoto 2, tumeshirikiana tumejenga nyumba. Leo hii ananitaka niondoke,ninuache na watoto.Nikaanze maisha kimpango wangu.
Naambiwa kuwa anayaweza maisha bila hata ya uwepo wangu.
Nahisi kuna marafiki amewapata wana mshauri vibaya.

Naombeni ushauri.
Mwambie yy ndyo aondoke akuachie nyumba hyo
Mwanamke mjinga xn huyo
 
Mwambie yy ndyo aondoke akuachie nyumba hyo
Mwanamke mjinga xn huyo
Leo kwa kutumia upelelezi wa hali ya juu,nimeanza kuwasaka saa nane mchana,hatimaye saa 2 nimewafumania guest fulani,nimempiga sana,mwanaume amekimbia sana...
 
Brother fedheheka tu kwajili ya wanao, hicho tu ndo ikufariji wanao watafurahia uvumilivu wako in na kuona umuhimu na hekima zako pindi watakua watu wazima, najua sio rahisi lakini vumilia mungu atakupa nguvu na kumbuka miujiza hutokea kila siku,...
 
Brother fedheheka tu kwajili ya wanao, hicho tu ndo ikufariji wanao watafurahia uvumilivu wako in na kuona umuhimu na hekima zako pindi watakua watu wazima, najua sio rahisi lakini vumilia mungu atakupa nguvu na kumbuka miujiza hutokea kila siku,...
Unajua maana ya ukimwi wewe?,alafu kama kweli wewe ni dr huwezi nishauri kitu kama hicho.
Fuatilia post kuanzia mwanzo,nilikuwa tayari kusamehe,mke hakuomba radhi kwenye kikao na tulipo rudi home,akaniambia haachi kamwe,leo red handed nimemfuma guest kitandani,unataka nini tena?
 
Pole sana mkuu ila jitahidi kuperform vizuri kitandani atarudi mwenyewe,ukiona mkeo ameanza kuchepuka ujue mechi zako ni za dana dana.
 
Pole, kaza moyo tu mkuu! Anza kumpuuza usimfwatilie kuwa busy na mambo yako ya kujiongezea kipato na rafiki zako pia jitahidi kukaa mbali nae kiufupi anza kumtenga maana ndivyo anavyotaka! Kama anakupenda ataanza kupata wivu kama hakupendi itakua ni suluhu ya kuepusha migogoro, muache yeye awe wa kwanza kudai talaka kama ni vikao aitishe yeye tena mwambie kabisaa kama unataka talaka itisha kikao udai talaka yako ili baadae asipate sababu ya kukushushia lawama kuwa wewe ulimfukuza na kumtelekeza na kwenye kikao kwa kuwa yeye ndo anahitaji kujitoa kwenye agano ng'ang'ana ubaki na wanao maana weka wazi tu huna uhakika na ubora wa maisha watakayoenda kuishi wanao chini ya mwanaume mwingine so ni bora upambane tu kuwalea watoto wajue mama yao ndio kawakimbia sio wewe ndio umewakimbia maana sumu ya maneno ya mama ni Kali sana kwenye saikolojia ya watoto, KUNA WANAWAKE Wana roho mbaya sana hasa wakipata bwana wa nje kama uyo wako yuko tayari kuvunja familia kwa ajili ya mjinga mmoja huko nje ila time will tell atakuja kukupigia kagoti ipo siku

Mkuu maneno yako yamenipa hekima ahsante sana. Ndugu mtoa mada fata huu ushauri wa huyu mheshimiwa utakua na hekima sana
 
Shida kwa upande wangu ni watoto, kwa sababu ndio kizazi chako halafu..sina uhakika na maisha baada ya kuachana upande wako tena mmejenga, kwa hatua ambayo umefikia kimaisha ningependa kuona ukikabili tatizo na kupata suluhu sio kukimbia tatizo.
 
Daah huyo bora umeachana nae kaka angekusumbua na kukutia aibu, mungu atakusaidia utampata mwingine mkuu.
 
Hapo kwenye kufukuzia mbali ndo pagumu.
Nyumba ambayo wewe ulimwaga trip 10 za mawe uka safiri kutafuta pesa,kurudi ukakuta kajichanga kaongeza trip tano na yuko busy ku process mkopo bank aendeleze,unaanzaje kumfukuza mtu na anaanzaje kuondoka?
Wanawake siku hizi sijui wamekumbwa na nn.
Nina rafiki yangu alichanganywa mpaka akaamua kubadili mpaka dini na kuoa upya...
Hati ya kiwanja na nyumba ni ya nani? Usikubali kua mnyonge hivyo
 
Back
Top Bottom