Mke wangu anadai niifukuze familia ya kaka nyumbani

Tafuta pesa afungue biashara yoyote auze vitu ajiendeleze na kusevu pesa kisha aondoke. Hapo ni pagumu haswa kama na yeye anafanya hayo yote huku una housegirl.. kiaina fulani shemeji yako ana uchokozi fulani anautenda.. labda anakupenda ila hawezi kukuambia. Mtafutie mtaji muanzishie biashara uache kuhudumia kila kitu.. yaani ameka kwako bure hata pesa ya chupi utakuwa unamnunulia wewe.. duh!!!
Umevuka mipaka na kwanini unamtoa yeye out bila kwenda na mkeo pia... unatatizo inabidi ujipange.. shemeji yako mgomvi sana anatamani maisha ya mkeo. Ni HATARI fikiria
 
Mkuu ugomvi unataka mwenyewe, kwanini usimzuie huyo Shemeji yako kufanya hayo anayofanya na umwambie mkeo ajifunze kwa mwenzake na kuanza kuwajibika kama Mke?una uwezo wa kuhudumia familia mbili zikiwa pamoja unashindwa kumpangishia Shemeji yako walau chumba tu?mbona vipo vya gharama nafuu tu lazima akubaliane na hali halisi na kukubali kwamba maisha kuna kupanda na kushuka aishi chumba utakachomudu kumlipia na ikiwezekana mtafutie hata kijibiashara kidogo hata cha mama ntilie ili aweze kupata baadhi ya mahitaji yake ili hali na wewe ukiongeza nguvu,unajua tatizo huwa tunafikiria vitu vikubwa wakati kila hali ina solution zake kulingana na uwezo.Mke wako anafanya hivyo for the sake ya ndoa yenu anaona mambo yanavyokwenda ipo siku utateleza ukamsingizia shetani. Jiongeze
 
Hujafa hujaumbika, kweli miaka mitano si mingi. Endelea kutunza familia ya kaka yako mkuu maana ndio damu yako na ukoo wako mana mwanamke ni sawa na ganda la mti mwingine kupachika kwenye mti mwingine kitu ambacho hayawezi kushikana ila wewe na kaka yako ni ganda la mti mmoja. Naamini yapo mazuri ambayo kaka yako alishawahi kukufanyia na yeye kuwa gerezani ni kipimo cha fadhila za kaka yako kwako na tambua LEO KWAKE, KESHO KWAKO. Hao watoto wa kaka yako usiwaone wadogo, kesho watapata kazi za maana tu na watawasaidia, (Nakumbuka mzee wangu alipostaafu ba'mkukwa na baadhi ya
ba'wadogo walitudharau sana tukiwa S/Msingi wakijua hatutafika popote lakini tulipambana kwa sasa tumeua University wameanza kujirudi nasi tumesamehe 7x70).

Shem kukuita MUME ni kawaida ila hizo za kufungua geti na kukupakulia chakula afanye mkeo kama hataki jipakulie mwenyewe.

NB:
Wanawake huwa hawapendani.
 
hata akimla undugu uko pale pale.....hawezi badilisha damu na vimelea vyake......awe mwanaume wa kweli.....kujisogeza kwa shemejio ni tatizo haswaa....
 
Mimi muda wote nasoma hii stori nacheka tu kwa jinsi jamaa anavyotuchuuza


Sent using Jamii Forums mobile app
Umeona eeh....anazunguuuka kumfanya mkewe aonekane mbaya kumbe tatizo lake mwenyewe. Na wa jela ana miaka mingine mitano mizima....akirudi wallah atakuta kabadilishwa jina yeye ndiyo kawa shemeji badala ya mume....
 
Yani umechukua mawazo yangu kabisa, me mwenyewe nimeshangaa, alafu cha ajabu kuna watu humu wanamlaumu huyo mke wa mleta mada eti ana roho mbaya sijui nini, tena ukute akija hapa kuhadithia mambo ambayo huyo bi dada anayafanya tutachoka. Mimi mwenyewe huwezi kuja kuishi kwangu alafu ujifanya wewe ndo mwenye nyumba hadi kwa mume wangu weee thubutuu mbona ningewapisha mtu na shem wake waliwazane vzr pumbavuuu
 
Wanawake wengi huwa hawapendi kabisa ndugu wa Mume, wanajitahidi sana kuwapenda watu wa pembeni ili waonekane wazuri.
 
This is right.
Huyo mwanamke afunguliwe biashara aishi kivyake.
Usikute ameshaanza kumgonga huyo mwanamke.
 
This is right.
Huyo mwanamke afunguliwe biashara aishi kivyake.
Usikute ameshaanza kumgonga huyo mwanamke.
 
Umeona eeh....anazunguuuka kumfanya mkewe aonekane mbaya kumbe tatizo lake mwenyewe. Na wa jela ana miaka mingine mitano mizima....akirudi wallah atakuta kabadilishwa jina yeye ndiyo kawa shemeji badala ya mume....
Hahahahah katafuta njia ya kumfukuza imeshindikana anaamua kumtafutia visa mkewe.
 
Utuambie tu ukweli kuhusu huyo shemeji yako haiwezekani akwambie hawez kujishusha kwa mkeo na we unaridhika pia unaendelea kufurahia tuu huduma zake mkataze asikuhudumie hayo matatzo unaleta mwnyewe,..na umesema una wazee kwa mini asiende kwa wazazi wenu upeleke matumizi huko?
 
Hii Ngumu kumeza,but here are some things to go thro

1. Mke wa kaka yako aende kwa ndugu zake,hapo kwako wabaki watoto tu.
Kwa maana yeye ndie chanzo cha kupoteza amani,anakufungulia geti hiyo vepe wakati mdada wa Kazi yupo? Anavaaje Nguo za kulalia halafu akupakulie chakula!!!! Mbona anaonyesha direct mambo ya kishetani??? Si ana mama wakubwa na Dada au ndugu zake?? Aende huko abakize watoto.

2. Ongea na mke wako,ugomvi wa watu lazima asiwaingize watoto,ujue watoto wanakua na wanaona kinachoendelea?? Watajenga chuki mioyoni mwao,watashindwa kusaidiana kama ambavyo wewe unamsaidia kaka yako kwa sasa.

3. Nenda kalifikishe kwa kaka yako huko gerezani kusaidie mawazo mke wake aende wapi au umeamua aende wapi kutokana na yanayoendelea.

Nb: kabishangaza sana unataka kushindana na mwenye nyumba inahusu.

Au

Make mgomo baridi,Ili akikufungulia gate mwambie usisumbuke mwache Dada wa Kazi afanye hiyo Ndio Kazi yake ukiingilia nitakuwa namlipa mshahara bure. Akikupakulia chakula kalie chumbani kwako na upotelee huko mpaka kesho yake avitoe mke wako. Akili kichwani kwako but mke wako huko right about the thoughts Ku kuhusu wewe na huyo mke wa kaka ako,mwache abiria achunge mzigo wake.
 


UNATEMBEA NAYE NA KUMPA KICHWA WEWE, USITUFANYE SISI WAJINGA KIASI HIKI ....
 
Hapo ndo alipokosea
 
Jamaa kasema hata zaman mke wake alikuwa hampi hizo huduma
Zaidi ya dada wa kazi tu
Sasa watu sijui hawaoni huo msitari!
Watu wamekazana tu anaingilia majukum sio yake akat jamaa
Amekiri dada wa kaz ndo alikuwa
Akilfanyia hayo
Ya kumfungulia geti
Mimi mpaka nimeamua kuacha na sitaki kubishana na watu humu......kuishi nyumba za watu ni kazi sana hasa ukiangalia na situation ya huyo dada
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…