Mke wangu ana tatizo kubwa msaada please

Mke wangu ana tatizo kubwa msaada please

Mpende sana mke wako kwani anahitaji upendo, mfanyie vile anavyopenda na pia kuwa rafiki yake akufuate wewe tu pindi anapokuwa na shida. Kiufupi unatakiwa uwe kioo pindi akutazamapo ajione katika kioo hicho.
 
hayo ulitakiwa kuyajua kabla ya kumuoa
 

Pole sana!maadam umegundua kosa ni hili basi jitahidi kutomgombeza na kumkemea!najua itakuwa vigumu kwako lakini jitahidi for the sake of ur marriage.

Pia jitahidi kumpeleka maeneo tofauti todauti ya kuvutia kubadilisha mazingira itamsaidia pia.Anza utamaduni mpya kumsifiasifia na kumpelekea zawadi kama maua mbalimbali.maua ni dawa pia .

Ukiweza mpeleke kwa prof Japhet mbobezi wa matatizo ya akili na mshauri mzuri sana wa mahusiano wewe kamuone kwanza mweleze hali halisi halafu siku mkienda jifanye kwa mkeo wewe ndo unatatizo unamuudhiushi mkeo unahitaji ushauri sasa mkifika pale atawahoji kila mmoja wenu kirefu hadi historia ya kila mmoja wenu then tatizo na ufumbuzi.

Mtapata kwa pamoja!nina uhakika utarudi hapa kukiri mabadiliko.session zake ni three hours per couple!na sio ghali kabisa yuko BOCHI hospital Mbezi kwa Msuguri alikuwa nje kwa zaidi ya miaka ishirini ndo amerudi last year.nakushauri kutokana na kupona binamu yangumy best friend too tatizo kama la mkeo na amesota miaka kumi ndoani.
 
POA, Fanya Hv, Muache Usimkosoe Kama Miez 2 Hv. Hata Akikosea Mbele Za Watu Uchune, Kua Mpole, Muoneshe Mapenz, Na U2nze Kumbukumbu Ya Makosa Yake, Toa Cku Moja Akikosea, Mwite Chumban Muhoj, Mweleze Mwanzo Wa Makosa Yake, Then Mtandike Mpaka Alainike, Baada Ya Kichapo, Mwambie Sitak Hik Na Hik Kuanzia Leo Ama Ntakurudisha Home, Majeraha Yake Usimpe Pole Wala Kumpleka Hosp, Hatagundua Kama Umechukia, Mchunie Hata Cku 2,onesha Kutomjar, Huku Ukirud Mapema Home Na Mahtaj Kama Kawaida, Ila Usimguse, Atakuomba Samahan Mwenyewe Na HATARUDIA TENA, Sote Tulikua Hvo

Huu sio ushauri bora kwanini mpige kwani hakuna njia nyingine yakueleweshana mpka umpige huyu ni mtu mzima mwenzio na sio mtoto kusema utamfundisha kwa kumchapa kuna njia bora nyingi na sio kumpiga :angry:
 
Huu sio ushauri bora kwanini mpige kwani hakuna njia nyingine yakueleweshana mpka umpige huyu ni mtu mzima mwenzio na sio mtoto kusema utamfundisha kwa kumchapa kuna njia bora nyingi na sio kumpiga :angry:

Si Wote Wanaeleweshwa Kwa Upole. Ukiwa Mpole Anakupandia, Na S Wote Wanaeleweshwa Kwa Ukari, Una Angalia Upepo Wake Ndo Mana Akikosolewa Anaongea Naneno Mia. Huyo Anahtaj Awe Mkal Kdogo
 
Mzee Mugishagwe,

Hashima yako mkuu, naona hapo unachanganya mambo mawili mazito wazungu hawampigii kelele Mugabe kwa sababu ya wananchi kuwa na shida kwani si hata bongo wapo wananchi kwa mamillioni ambao wangependa mkoloni arudi! kwani tofauti yetu na Zimbabwe ni nini?

The issue hapa ni ardhi! Mugabe baada ya miaka mingi katika power alikuja kugundua kuwa asilimia 95% ya wananchi wake hawana ardhi au wanamiliki only 5% ya ardhi ya Zimbabwe nchi yao, wakati wazungu ambao ni asilimia 5% ya zimbabwe wana own 95% tu ardhi ya zimbabwe, kabla hajaanza pokonya pokonya ya ardhi hiyo aliwaomba wazungu yaani the West wamsaidie kulitatua tatizo hilo la Aedhi ya zimbabwe inlcuding The Commonwealth, wota wakaanza kujiuma uma, akamuomba Mbeki na Madiba, waote hawana jawabu, ndipo akaamua kuanza kuchukua ardhi hiyo na sio kwa faida yake bali kuwapa wananchi wa Zimbabwe, sio kama kina fulani hapa bongo ambao wamezichukua na kujenga majumba ya kupanga, sasa wewe mzee Mugishagwe hapa ni kipi usichoelewa? Hamna sababu ya kuwa Intellectual au professor, au genius kuelewa kuwa some where au somehow something had to be done! Na hata hawa wazungu wa Zimbabwe ni wapumbavu wakubwa kwani hata wao walipaswa kuelewa
kuwa it was coming kwa hiyo wangeanza mapema kutafuta njia za ku-reconcile au kutafuta njia za kubalance hii issue!

Mbeki, Madiba, na the whole OAU katika hili wako na Mugabe, kwani aliwauliza wote wamsaidie kumpa maarifa ya kuweza kuchukua hiyo ardhi bila kutumia nguvu none had an answerr for him, Mwalimu alimwambia achukue ardhi hiyo pale tu walipopata uhuru yeye akaamua kuheshimu makubaliona ya Lacanster, ambayo yalitengenezwa na wazungu kwa ujanja wa kujua kuwa ardhi yote ya Zimbabwe imo mikononi mwa wazungu, jamani tuache kusikiliza hawa the West waongo wakubwa na wanafiki wakubwa hawa, ndio wanatupa misaada lakini uhusiano uishie kwenye misaada tu sio mpaka waingilie siasa zetu,

Wewe mkuu Mugishagwe na the West mlitaka mugabe afanye nini?

Kamwe katika maisha yangu sitanyanyua mkono wangu kumpiga mwanamke,na Mungu anisaidie.Pia kumpiga mtu mzima ni kukosa akili.
Anachopaswa kukifanya mleta mada ni kuwa karibu zaidi na mkewe,kumfanya amuone yeye ndiyo kimbilio lake, matatizo ya Kisaikolojia kamwe hayatatuliwi kwa ngumi!
Ni vyema kuanza kwenda naye out mara kwa mara, na outings hizo km ni mkristo zihusishe sehemu zenye concert za nyimbo za injili,lkn pia na kwenye maombi.
Anahitaji Amani ya Moyo, na ili aipate lazima Asamehe.Only good moments will make her realise that.
Yapo mengi ya kufanya,ila kubwa ni kuwa rafiki yake anayemwelewa matatizo yake na kuyatafutia suluhisho lisilo na negative impact!
Kuna siku atafunguka na Kuachia yote yaliyo moyoni!
 
Kamwe katika maisha yangu sitanyanyua mkono wangu kumpiga mwanamke,na Mungu anisaidie.Pia kumpiga mtu mzima ni kukosa akili.
Anachopaswa kukifanya mleta mada ni kuwa karibu zaidi na mkewe,kumfanya amuone yeye ndiyo kimbilio lake, matatizo ya Kisaikolojia kamwe hayatatuliwi kwa ngumi!
Ni vyema kuanza kwenda naye out mara kwa mara, na outings hizo km ni mkristo zihusishe sehemu zenye concert za nyimbo za injili,lkn pia na kwenye maombi.
Anahitaji Amani ya Moyo, na ili aipate lazima Asamehe.Only good moments will make her realise that.
Yapo mengi ya kufanya,ila kubwa ni kuwa rafiki yake anayemwelewa matatizo yake na kuyatafutia suluhisho lisilo na negative impact!
Kuna siku atafunguka na Kuachia yote yaliyo moyoni!

Mnh huyo uliyemquote umeitoa wapi mkuu?
 
Pole sana mkuu, Sema tupo TZ kwa wenzetu mkeo ana matatizo ya kisaikolojia. Mimi nashauri muwaone wataalamu husika kwani wahenga walisema "mficha uchi maradhi humuumbua". Kila la kheri.
 
Kama ni stori ya kweli..niPM nikupe contacts za Psychologist amsaidie. She needs a professional help!
Niko pamoja na wewe katika hili chief wangu. Ni msaada wa mtaalamu wa saikolojia pekee ndo utakaomsaidia mke wa jamaa.
 
Niko pamoja na wewe katika hili chief wangu. Ni msaada wa mtaalamu wa saikolojia pekee ndo utakaomsaidia mke wa jamaa.

Mnataka kumlia tu hela huyu mkaka,tatizo la mkewe sio kubwa kihiivyo lol azidishe upendo,ampe compliments za mara kwa mara,amshirikishe kwenye mambo yake then ataona signifficant change 💃💃💃💃💃💃💃💃
 

Pole sana kwa hayo majanga. Kwakuwa umelijua tatizo la mkeo ni kuwa anajiona hathaminiki la kufanya ni kucheza na akili yake,toa time yako nyingi kuwa nae, mtoke out, muangalie movie pamoja za mapenzi za kuchekesha.

Ili kuleta bond kati yenu Pia itasaidia kuwa na story ya kupiga nae mara unapo kuwa nae. Vijizawadi ni muhimu ili kuamsha tabasamu lake na furaha yake, si lazima iwe ya gharama kubwa sometimes hata kitu cha 5000 kinatosha kumchangamsha mwanamke.

Punguza kumfokea, tafuta njia tofauti ya kumuelezea makosa yake, unaweza kuwa unafikisha ujumbe huo kwa utani.
Just mpe furaha na upendo, kwa kifupi atakuwa sawa.
 
Kijana Kwanza pole kwa changamoto inayokukabili, fanya yafuatayo kurekebisha, muache akosee mara 2,3 alafu msubiri akiwa Kwenye mood mchape bakora kali hakikisha anaifurahia akishatosheka mwisho kabisa msomee mashtaka yake kwa upole alaf mwambie alipokosea, then mnyuke tena bakora ya mwisho, atakaa tu mstarini huyo.
 
Mshukuru Mungu kwa kukuwezesha japo kufuatilia na kuamua kutafuta suluhu ya hili tatizo. Kama ungeanza kuwaza kua na mwanamke mwingine ndio ingekua mwanzo wa ndoa yako kuharibika. Kama kweli nia yako ni kutafuta suluhisho la tatizo la mkeo, nna imani kwa kiasi kikubwa kwamba utafanikiwa.

Jambo la kwanza ni lazima umweleze kwa upole kwamba unampenda kwa dhati lakini haufurahishwi na hiyo tabia yake ya kutokupenda kukosolewa. Mweleze jinsi inavyokuweka katika wakati mgumu na ajue kwamba haumchukii yeye bali ni hiyo tabia.

Pili ni lazima awasamehe na aachilie hao waliomtendea ukatili, bila kufanya hivyo hilo jambo litaendelea kumsumbua sana. Atakua anaishi maisha ya kuigiza tu, anasumbuka au kuogopa kitu kisichokuwepo ki uhalisia, kipo kwa kufikirika tu. Kwa mfano hapo anaona unamnyanyasa wakati ki ukweli wewe unahangaika kutafuta suluhu.

Utakosea sana kama utaamua kumuacha anapokosea bila kumkosoa kisa unaogopa atajisikia vibaya, utatengeneza maisha ya kisanii yasiyo na uhalisia.

Mwisho wa yote UPENDO huvumilia yote na hauhesabu mabaya, mpende mkeo mkuu!
 
Nimefurahi kuwa hujamkatia tamaa mkeo ingawa ushamkon'gota vya kutosha. Kwa kuwa ushajua tatizo suluhisho kubwa hapo ni moja tu:

Mkeo kuwasamehe ndugu zake hasa yule aliyemlea toka utotoni maana ndiye aliyepanda mbegu ya kutokujiamini kwake. Akisamehe anaweza kuanza kuamini kuna kupendwa maana watu wa aina hii wakipendwa wanakasirika.

Akili zao zinataka manyanyaso. Ukimsifia anafikiri unamkejeli, ukimkosoa anaona unakuwa kama shangazi yake, ukimpa zawadi anaona humaanishi anaona unajipendekeza baada ya kumuonea.

Njia ya kuwasamehe watesi wake ni rahisi kuliko ya kwenda kwenye sessions za wanasaikolojia ambao hawana muda wa kutosha, na wengine hujifanya wanajua sana kumbe wamekariri tu, na bado utatakiwa kulipa. Akikubali ana tatizo na akaweka nia ya kupona akatangaza msamaha toka moyoni atashangaa namna atakavyobadilika.
 
Dawa !! Mkuu nitonye kwa dawa na tiba ya haraka zaidi ni bora muende Vacation, mutoke nje kwa matembezi !! mtarudi na mawazo mengine ya kimaisha!!
 
Last edited by a moderator:
Matatizo ya kiakili yana ugumu sana kutatua, ni kitu kilijengeka kwa mda mrefu, sio rahisi kukiondoa kwa siku moja au mwezi mmoja.

Kama alivyosema Riwa, tafuta wataalamu wa maswala hayo, wala usiogope, mueleweshe tu kuwa anahitaji wataalamu wa maswala ya saikolojia ili kumrudishia hali yake ya kawaida.

Lakini pia, kuwa mpenzi na rafiki yake...ongeza upendo!!
 
Last edited by a moderator:
Tatizo lako dogo sana.

Haumridhishi, Haumfikishi.

Jitahidi.
 
Back
Top Bottom