Mugishagwe
JF-Expert Member
- Apr 28, 2006
- 300
- 58
Je JK alishauriwa vyema na kualingalia swala la Zimbabwe kwa undani kabla hajaanza kumwa sifa na support kwa Mugambe badala ya wananchi wa Zimbabwe ? Je katika hotuba yake aliwaacha wapi wananchi wa Zimbabwe ambao wanateseka hadi wanatamani mkoloni kuwepo tena ??
2006-04-29 10:26:00
Na Maura Mwingira, Bulawayo
Rais Jakaya Kikwete amesisitiza kuwa uhuru wa kisiasa unakuwa na maana tu pale nchi inapokuwa na uwezo wa kujiamulia mambo yake bila ya kusukumwa au kuingiliwa na mataifa ya nje.
Alisema kama nchi haina uwezo wa kufanya hivyo basi maisha na watu waliojitolea mhanga kwa ajili ya uhuru wa nchi yao kama vile walivyojitolea wapigania uhuru wa Zimbabwe hayatakuwa na maana yoyote.
Alikuwa akizungumza wakati wa chakula cha usiku alichoandaliwa na mwenyeji wake, Rais Robert Mugabe, katika Ikulu ya Bulawayo.
Rais Kikwete alikuwa nchini hapa kwa ziara ya siku mbili ya kikazi.
Tunakuhakikishia kuwa, tutaendelea kupigia debe falsafa hii kwamba uhuru wa kisiasa utakuwa na maana kama tutaweza kujiamulia hatima yetu bila ya kusukumwa au kuingiliwa na mataifa ya nje, alisema Rais na kushangiliwa na wageni waliohudhuria dhifa hiyo.
Rais ambaye mara baada ya kukanyaga ardhi ya Zimbabwe alipokewa na mwenyeji wake kwa kupigiwa mizinga 21, alisema Tanzania inatambua kipindi kigumu na ambacho wananchi wa nchi hiyo wanakipitia na kuongeza Tanzania inaunga mkono juhudi za nchi hiyo na kulijenga upya taifa lao na kuondokana na udhalimu wa kikoloni.
Nakupongeza kwa moyo wangu wote komrade Rais kwa kukataa kukubali mahangaiko na machungu mliyoyapata wakati wa vita vya kupigania uhuru wenu yaonekane kuwa hayana maana yoyote.
Changamoto yetu sote ni kuhakikisha kuwa matumaini waliyonayo wananchi hasa wale waliopoteza maisha yao wakipigania uhuru yanatekelezwa kikamilifu.
Alimhakikishia Rais Mugabe kuwa serikali yake imedhamiria kuendeleza na kudumisha uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Nina uthamini na kuuendeleza uhusiano huu wa kidugu ambao Watanzania wameendelea kuuenzi tangu siku ile walipoona umuhimu wa kuungana mkono na kaka na dada zao wa Zimbabwe katika harakati za Chimurenga, alisema Rais, kauli iliyoshangiliwa na wenyeji wake.
Alisema kuwa leo Waafrika wanatembea kifua mbele na wanazungumzia hatma ya bara lao kwa kujiamini kwa sababu wananchi wa Zimbabwe wamethubutu kuzungumza na kutenda katika maana ile inayotafsiri kuwa dhahama na udhalimu wa kikoloni ulikuwa na mwanzo wake kwa hiyo lazima utakuwa na mwisho wake.
Leo hii Komrade Rais, tunaweza kutangaza kwa ufahari na imani kubwa kuwa wale wote waliotoa mhanga maisha yao katika Chimurenga na harakati za ukombozi, hawakujitoa bure, alisema.
Alisisitiza komrade Rais, na kaka mpendwa nataka nikusisitize tena kwamba kukuunga kwetu mkono katika juhudi za kuleta mageuzi katika Zimbabwe, hauna mjadala wala masharti kama ambavyo imekuwa siku zote.
Rais Kikwete ambaye pia akiwa nchini hapa alifungua rasmi maonyesho ya biashara ya kimataifa, alisema kuwa ziara yake hiyo licha ya kujitambulisha kuwa yeye ndiye rais mpya wa Tanzania, lakini ilikuwa pia ni ya kujifunza namna ambayo nchi hiyo imeweza kupita hatua kubwa kiuchumi.
Kwa upande wake Rais Robert Mugabe alisema kuwa Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo imeendelea kuiunga mkono serikali yake kwa hatua yake ya kuwapatia wazawa ardhi na akashukuru kwa hatua hiyo.
Tanzania mmeendelea kuwa nasi katika harakati zetu za kuwapatia watu wetu ardhi. Mmekuwa nasi hata pale mataifa makubwa walipotuwekea vikwazo kwa uamuzi wetu, tunawashukuru sana kwa upendo wenu, alisema.
SOURCE: Nipashe