Mke wangu amepata zero kwenye interview, ananilaumu

Mke wangu amepata zero kwenye interview, ananilaumu

wewe nae ni kilaza mwenzie!! we kama unamfahau mkeo ni mbululu ulitakiwa umpe desa alimeze akifika kwenye interview akateme tuu,,,, ona sasa unanyimwa utamu shaur yakoj
 
cyo vzurI kuletA mambO ya familia humU jukwaanI maanA naonA mmemchanA hadI marks zake alizopatA
 
Hata wakifanya marudio ya interview watu watafeli kama kawaida
 
Duh, ushaoa kiazi. Na uombe Mungu watoto warithi akili zako. Wakirithi kwa mama yao (mkeo) umeliwa. Uandae hela ya kusomesha tuition na shule za private... Na hela ya bumu uandae wakifika chuo...
 
aisee msicheke hii elimu imeharibika, kuna mdada kahitimu chuo maarufu huko kati mwez uliopita nilipata job sehem nikamwomba sivii yake, nilitamani kulia cv ina jina lake, la ukoo, shule alizospma, na amwani kamaliza...
tuache ushabiki wa kuharibu elimu kuna vyuo vinazalisha matap tap
 
kapata zero kakununia na wewe unababaika....kweli nawe walewale
 
Haya tazama uozo huu.

Kwa watu kama hawa wanaogawana nafasi za kazi mnategemea kuwa na maendeleo Tanzania hii?
 
Mbona haukumpa mtihani nyumbani kabla ya siku yenyewe?
Watu wanafanya hivyo kwa vilaza... (hii niisikia mahali..huwa wanawapa watu watakaofanya interview maswali)
 
Kama haelewi mwambie boss wako amwite akamwonyeshe marks zake huko huko ofisini.
Kwani na wewe unapokaa naye hukujuwa kuwa humo kichwani hamna kitu?
 
Ni kosa kubwa kuingiza personal interest ktk kazi za umma, haishangazi tumefika hapa kama Taifa.
 
nadhani si busara kumchukulia mke wako kama hana akili, yawezekana amefanya makusudi kupata sifuri ili akuone utafanya nini au utatumia busara gani kuongea nae, tafuta kwanza njia mbadala kama mume, ya kuongea nae ili kuweza kuikabili hisia yake maana ni wewe pekee ndo unafahamu uzur na mapungufu yake
 
wewe nawe ulikuwa hutaki kufanya naye kazi ofis moja, ungekuwa na nia ungempa maswali kabla ya intavyuu
 
Wakuu amani iwe kwenu,

Mimi ni afisa utumishi kwenye kampuni moja hivi hapa Dar es salaam. Hivi karibuni bodi ilitengeneza nafasi 12 mpya za kazi na kuzitangaza.Viongozi waligawana nafasi nafasi tatu kila mmoja na mimi kuniachia 3.

Huwa inakua hivyo kila tunapoajiri, katika hizo nafasi tatu nilizopewa nilipanga moja nimpe wife ambae amemaliza chuo mwaka Jana, nyingine ni mshikaji wangu ambae aliniandalia pesa na ya mwisho nimpe rafiki wa wife ambae wife
mwenyewe aliniomba. Mimi na wife tulioana akiwa na elimu ya form six hakuweza kuendelea kuna matatizo yalijitokeza, hivyo baada ya kumuoa ndipo nikampeleka chuo baada ya kukaa miaka 3 nyumbani.

Mwaka jana ndio amemaliza, so hivi juzi tukamwita kwa mtihani pamoja na wenzie kama 100 hivi tuliowachuja matokeo yalipotoka akawa amepata 2 ya 50 mi naita sifuri maana nilimuongezea mimi hizo mbili wakati nasahihisha.Bosi wangu akasema niamue nwenywe kama namchukua na matokeo hayo siku wakija auditors jumba bovu litaniangukia ni vyema nikasubiri nafasi zingine. Hivyo wale wengine 11 akiwemo na Rafiki yake wakaitwa kwa kazi

Sasa ndani kuna ugomvi kati yangu na mke wangu anasema ningemchykua hivyo hivyo hata kama kafeli. Nimemwelewesha hataki kuelewa kaninunia wiki sasa, hatuongeleshani tunaamka kama mabubu.Usiku saa ya kulala anavaa suruali za tight mbili na jeans juu na mkanda ndo analala tena kwenye kona ya kitanda.Nikimgusa ni ugomvi anasema ninatembea na rafiki yake niliempa kazi, nikimwelewesha kuwa yule alifaulu mtihani anadai tunamsaliti nyumba haina amani sasa.

Wadau najiuliza maswali kadhaa;
(1) Inakuaje graduate akapata 2 ya 50 kwa maswali ambayo wote tuliyasoma sekondari?
Mengine ya primary school?

(2) Inakuaje mtu anashindwa hesabu za ratio, kuandaa balance sheet, statement of ACC wakati chuo amepita mitihani na Ku graduate au ndo zile degree za chupi? Nalazimika kuwaza hivyo maana hainiingii akilini

Nikijaribu kumuuliza haya maswali anakua mkali anasema hataki maongezi. Kwa kweli nimechoka juzi nilikua naongea na rafiki yake kuhusu huu mgogoro kwa kweli alinifariji vizuri hadi nikafikria kuwa ni bora niwepo nae tu ukichukulia kuwa kwa sasa sipati conjugal rights .

Naomba mwongozo wenu

NB:
Tuna watoto wawili
Hizi ndo hadithi za kwenye kahawa ambazo mimi huwa sizitakagi.
Wajumbe wa UKAWA hivi ni wapi siku hizi mumeona watu wanaitwa kufanya tu usaili wa mtihanin wa kuandika tu halafu anaitwa kazini, bila hata ya kufanya usaili wa mahojiano (Oral)

Wewe umesema ni afisa utumishi, je hukuuona huo mtihani kabla? ili umpe mkeo majibu ya huo mitihani?
Nani alitunga huo mithani, na kama alitunga mtu mwingine kwanini wewe ulipewa usahihishe?
Je hujui uwezo wa mkeo kichwani hasa kwenye masuala ya darasani?

Binafsi naona naona umekuja na hadithi ya kwenye kahawa ili kufurahisha kijiwe tu! Haya watu wamecheka, furahi basi!
 
Back
Top Bottom