mke wangu alitaka nichoma kisu

mke wangu alitaka nichoma kisu

Sasa hapo ndo tujiulize, ilikuwaje 'kiama' kikatangazwa na mhusika asichukulie serious...alijua makosa yake

Baada ya kuona mtuhumiwa haelewi somo, ilibidi bimkubwa aje amuonyeshe kuwa alikuwa serious..nadhani mume hakuzingatia terms za kwenye namba moja

Nadhani mtuhumiwa hakujua namna ya kupooza hali ya hewa, na ukute ndio alizidi kuichafua


Bado nakataa kama ni mpango mahsusi, kwa sababu hata thread inavyojieleza inaonekana ni hasira za bibie tu
Mkuu hebu msome huyu jamaa kwa makini hapa chini.....

wadau naomba mawazo yenu kwa hili jambo nifanyeje mimi na mke wangu kwenye ndoa yetu tuna miaka sita na tumejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume,kama ujuavyo mambo ya ndoa hamuwezi kuishi kama malaika ugomvi hutokea.ila kwa bahati mbaya siku moja kama miaka miwili tumewahi kugombana kidogo ila mke wangu alinitamkia kwamba siku moja ataniua kwa kisu au kwa sumu,

wiki mbili zilizopita nilikuwa nimekuja mkoa mwingine kikazi ila alikuja ghafla usiku saa tano akakuta nimelala tukalala mpaka asubuhi,

asubuhi akanambia kwamba anataalifa kwamba nina mahusiano na mwanamke mmoja na nimemfungulia duka,nikamkatalia kwamba jambo hili halina ukweli kabisa

tulibishana kwa mda wa masaa sita tukiwa chumbani lodge wakati huo alikuwa kafunga mlango wa chumba na funguo kaficha,baada ya mimi kuendelea kukataa ghafla alichomoa kisu alichomeka kwenye suluali na kutaka kunichoma ikabidi tuendelee kupokonyana kile kisu bahati mbaya kikanikata mkononi naomba ushauri madau nifanyeje?

Ukisoma kwa makini utatambua kuwa huyu mwanamke ana matatizo.
1. Wana miaka sita ya ndoa, mara ya mwisho kugombana imeshapita miaka miwili!!
2. Anamtuhumu jamaa ana mwanamke mwingine na kamfungulia duka (ANAMTUHUMU KWA KUWA HANA UHAKIKA... Hajathibitisha pasopo shaka)
3.Amefanya ziara ya ghafla akitegemea angemkuta mmewe ana kimada ndani, ili labda awaue wote lakini kamkuta mmewe yuko peke yake na wakalala mpaka asubuhi
4. Kafunga mlango na funguo kaficha ili jamaa asipate mwanya wa kutoroka..... Oh Gosh!
5. Kachomoa bisu mfukoni tayari kumshindilia mmewe....

Hata kama ni hasira za namna gani, kwa mtiririko wa matukio haya, isingempasa kufikia hatua ya kutaka kumuua mmewe.

Ndio maana namtahadharisha jamaa, akae mbali na huyu kichaa. Atajamuua kweli si masihara!
 
...Ndio maana namtahadharisha jamaa, akae mbali na huyu kichaa. Atajamuua kweli si masihara!
Hhahahahah..babu huyu mwanamke sio KICHAA bwana..nashukuru kwa analysis yako..Hebu ngoja na mimi nikuonyeshe kuwa bibie sio insane..Ila analinda Penzi lake linalotaka kumponyoka...Ngoja nichambue post yake:

wadau naomba mawazo yenu kwa hili jambo nifanyeje mimi na mke wangu kwenye ndoa yetu tuna miaka sita na tumejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume,kama ujuavyo mambo ya ndoa hamuwezi kuishi kama malaika ugomvi hutokea.ila kwa bahati mbaya siku moja kama miaka miwili tumewahi kugombana kidogo
Hapa babu utaona Jamaa anakiri kuwa wana UGOMVI..na most likely wamegombana just recently..kwa hiyo matatizo yapo

ila mke wangu alinitamkia kwamba siku moja ataniua kwa kisu au kwa sumu
Hapa utaona mwanamke anatoa adhabu endapo atabaini ukweli wa tatizo..bahati mbaya jamaa naye kwa sababu anajua anachokifanya hastuki

,wiki mbili zilizopita nilikuwa nimekuja mkoa mwingine kikazi ila alikuja ghafla usiku saa tano akakuta nimelala tukalala mpaka asubuhi,asubuhi
Angalia hapa wamelala hadi asubuhi, muuaji gani asikuue usiku wakati unakoroma aje akuue asubuhi ukiwa macho

akanambia kwamba anataalifa kwamba nina mahusiano na mwanamke mmoja na nimemfungulia duka,nikamkatalia kwamba jambo hili halina ukweli kabisa tulibishana kwa mda wa masaa sita tukiwa chumbani lodge wakati huo alikuwa kafunga mlango wa chumba na funguo kaficha,baada ya mimi kuendelea kukataa ghafla alichomoa kisu alichomeka kwenye suluali na kutaka kunichoma ikabidi tuendelee kupokonyana kile kisu bahati mbaya kikanikata mkononi naomba ushauri madau nifanyeje?
Hapa kinachoonekana na majibizano ambayo huenda mleta uzi alishindwa kufunguka na ndipo bibie akaamua kumtishia, jiulize alipataje ufunguo wa mlango?...Bibie sio MUUAJI ila alitaka kuweka sawa mambo yake babu
 
Iwe ni kweli una nyumba ndogo au lah! Suala la kukuchoma kisu ni kitu tofauti, wote wenye nyumba ndogo wangechoma visu nani angeishi?, jaribu kuulizia huko kwao wanamhusiano gani na visu ama kuua watu, tusijekukuzika ndg.
 
Asprin juzi alisema mtoto wake akiliwa (shoga) anaweza kumuua.

Mke wa jamaa alimwambia akimsaliti atamuua

Wauwaji hawasemi bwana; mleta mada kuna vitu vingi ameamua kuficha. Wameamka asubuhi wakagombana for 6 hrs. Mkewe akavaa suruali na kuweka kisu kwenye suruali ndipo alipokichomoa.

Whatever it is, "amuache huyo mwanamke muuaji!"
 
Last edited by a moderator:
Hhahahahah..babu huyu mwanamke sio KICHAA bwana..nashukuru kwa analysis yako..Hebu ngoja na mimi nikuonyeshe kuwa bibie sio insane..Ila analinda Penzi lake linalotaka kumponyoka...Ngoja nichambue post yake:


Hapa babu utaona Jamaa anakiri kuwa wana UGOMVI..na most likely wamegombana just recently..kwa hiyo matatizo yapo


Hapa utaona mwanamke anatoa adhabu endapo atabaini ukweli wa tatizo..bahati mbaya jamaa naye kwa sababu anajua anachokifanya hastuki


Angalia hapa wamelala hadi asubuhi, muuaji gani asikuue usiku wakati unakoroma aje akuue asubuhi ukiwa macho


Hapa kinachoonekana na majibizano ambayo huenda mleta uzi alishindwa kufunguka na ndipo bibie akaamua kumtishia, jiulize alipataje ufunguo wa mlango?...Bibie sio MUUAJI ila alitaka kuweka sawa mambo yake babu

Hahaha mkuu SnowBall usiniambie huwa tunalinda penzi kwa kudhuru au kuua tumpendaye....! Yaani unataka kumpeleka mtu akafanye mapenzi na funza chini ya dongo la tani saba ndo useme ulikuwa unalinda penzi? Aaa... c'mon boy!!

Mkuu msome vizuri, mara ya mwisho kugombana miaka miwili ilishapita.... "Recently" kwangu mie naichukulia kama juzi labda. Ugomvi ushapita miaka miwili mkuu! Siyo ugomvi tena huu, hiki ni kisasi. Kwamba hakusamehe na adhabu aliyoipanga ni kuua! Muuaji huyu mwanamke nakuapia.

Hahahaha! Mkuu unaweza kumtishia mtu kwa kufunga mlango na kumsokomezea mbisu? Kama si jamaa kukinga na kuumiza mkono wake saa hizi si angesha RIP? Alipopata ufunguo? HAPO NDIO UJIULIZE SASA. kama hakuwa na dhamirio la kuua aliutafutaje ufunguo mpaka akaupata na kuuficha? Alitaka amchinjilie mbali halafu apotee zake. na ndio maana alikuja kimyakimya bila kutoa taarifa ya ujio wake ili kupoteza ushahidi. Stuka! Wauwaji ni wajanja sana.....:A S angry::A S angry:
 
Last edited by a moderator:
Asprin juzi alisema mtoto wake akiliwa (shoga) anaweza kumuua.

Mke wa jamaa alimwambia akimsaliti atamuua

Wauwaji hawasemi bwana; mleta mada kuna vitu vingi ameamua kuficha. Wameamka asubuhi wakagombana for 6 hrs. Mkewe akavaa suruali na kuweka kisu kwenye suruali ndipo alipokichomoa.

Whatever it is, "amuache huyo mwanamke muuaji!"
Ewaaaaa! Unless kuna kitu kaficha mtoa mada. Lakini kama itabakia kama ilivyo, na hivyo ndivyo ilivyokuwa, then huyu mwanamke ni muuaje. Na aachwe akapumulie mbali kuleeee!!

Nimefurahi ulivyoonyesha tofauti yangu na huyu mwanamke...
Asprini kasema......."anaweza" kuua
Mwanamke kasema...... Atamuua....

Lugha ya dhamirio huwa haijifichi.
 
Haya babu Asprin nimekusoma, ila kama jamaa atamsue mkewe ntamuomba loya [MENTION]Rutashobolwa[/MENTION] tukamtee huyu binti..bado naiona 'conscience' yake iko very clear na demeanor yake was not entitled to murder somebody................
 
Last edited by a moderator:
Mkeo kuna kitu anachosiku nyingi ndani ya moyo,alisema atakuuwa..ni kwamba lazima atakuuwa,umekwisha jaribu kama usingeng'ang'ana na hicho kisu nini kingetokea baada ya hapo?ashukuriwe mungu kimekuumiza mkono.

Naweza kusema kuwa katika lile neno kuwa atakuuwa tayari katika ulimwengu wa roho limekwisha umbika ajalishi mtakaa kwenye ndoa miaka mingapi hipo siku tu lazima atakuuwa..litatokea katika ulimwingu halisi..

muite mkeo na watu wazima,washuri wenu wa mambo ya ndoa ndugu zako na ndugu zake..sema kila kitu na yeye aseme kila kitu,msameane mbele ya watu wengine kama mashaidi na atubu lile neno kuwa atakuuwa kwa kisu,na kuanza safari upya ya maisha ya ndoa.

Naomba usichukulie rahisi kama unavyofikiri mwenzio yuko serious kuna nguvu ya shetani nyuma yake ndiyo maana amefunga safari akiwa na kisu kukufuatilia.

MORE USHAURI UNAWEZA KUNI INBOX
 
mahango kweni mkeo kabila gani?? kwani kuna makabila wanawake huua waume zao so ka ni miongoni mwa hayo makabila (yanajijua) chapa lapa aiseee , atakurestisha in peace......
 
Last edited by a moderator:
Bibie Kaunga heri ya siku ya ngumi.

Babu yangu aliwahi niambia kuwa mtu akikuambia atakudhuru kwa namna fulani (awe amelewa au hajalewa), na kweli siku moja akataka kufanya kama alivyokuambia. Kaa mbali na huyo mtu kama utafanikiwa kutoka salama kwa kuwa hakika ni lazima atatimiza lengo lake.

Kwangu mie babu yangu ni kama nabii, kwahiyo napenda kuishi maneno yake.

Jirani yangu siku moja alikuwa anajinyonga bahati nzuri mkewe akawahi akakata kamba..... Akamwambia "umenichelewesha tu, lazima nitajiua" Watu walimkalisha chini, wachungaji wakamwombe ikaonekana kimeshaeleweka......Maweeeeee Haukupita muda akakutwa kajining'iniza kwenye mwembe na mauti yashamkumba!!

Hawa watu wanaozungumzia mambo ya kudhuru au kujidhuru na wakaatempt kweli....... waogope mbaya!! Ni vichaa hawa!!
Ni kweli Asprin, ogopa sana mtu anaekwambia atakuua manake anakuwa amevaa liroho la shetani na kweli kuna siku atakuua, wewe alikwambia babu yako, mie mama angu mzazi amewahi kunambia ukisikia mtu anakwambia atakuua kaa nae mbali manake ni kweli kuna siku atakuua. Alinisimlia kisa cha kweli kilitokea huko kijijini kwao kuwa kulikuwa na mke na mume kila wakigombana yule mwanaume anamwambia mkewe ntakuua, ntakuua.

Basi siku moja wakagombana haswa, yule mwanaume akachukua panga akamkata mkewe, mke akadondoka faham zimepotea, mume akakimbia nadhani alijua keshaua, wakaja majirani wakampeleka hospital, akapatiwa matibabu akapona then akarudi kwao, amekaa kwao karibia mwaka mzima, baadae yule mume akajirudi akaomba msamaha, wazazi wa pande zote mbili wakaita vikao, wazee wa ukoo nao hawakuachwa nyuma, mume akajiapiza siku hiyo kuwa hatakaa arudie tena kumpiga wala kumtisha mkewe!

Mama angu ananambia mume akaleta na mbuzi, sijui wakanyweshwa damu na kadhalika. Watu wakala wakanywa na kufurahi. Jioni ya sa moja mke na mume wakaondoka kwenda kuanza maisha yao upya!

Hivi unajua kilichotokea? Huezi amini usiku ule ule yule mwanaume alimchinja mkewe kama kuku na akatoweka wala hakujulikana alipoenda mpaka leo!

Hivi vitu vipo na kiukweli mie sitaki kuamini hata kama mwenzio kakukera namna gani suluhisho ni kumuua, bora kuachana kwa amani ya bwana!



We mleta mada huyo mkeo hakufai, mwogope kama ukoma, amekukosa majuzi kuna siku atakupata, amekukosa kwa kisu atakupata kwa kukuwekea sumu kwenye chochote, kimbia ndugu! Ndoa ishakuwa ndoano hiyo, fanya maamuzi magumu asee! Haya maisha ni matamu sana mpendwa.
 
Last edited by a moderator:
hapo huna mke bali una ASHA Ngedere.POLE.
 
Mkuu unaonekana wewe ni kicheche.Nimeshaona situation ya namna iyo.Cha kufanya badili tabia.Kama ulikuwa mlevi stop,rudi nyumbani mapema,kuwa karibu sana na wife wako,mshirikishe kwenye mambo yako ya kimaendeleo pia toka nae out yeye na familia.Hakika atabadilika.Ni wivu unamsumbua halafu wewe unaonekana hujali hisia zake.Ukileta masikhara atakuua kweli.Change..!
 
Akikuua usikubali mpaka na wewe umlipizie, haya ni maneno tuliyokuwa tukiambiana wakati wa utoto lakini kwasasa ktk hali ya utu uzima huu tunaelewa kua ukifa hauwezi kufanya kingine chochote. Ndugu yangu kuwa makini uhai wako ni mali kuliko huyo mke wako hivyo jipange mkuu katika hali ya kuepuka hicho kifo.
 
Asprin msome tena taratibu; that his story hatujui ya mkewe. Na kumbuka kila mtu ana kauendawazimu kinachohitajika ni stumuls tu, sasa kiwango au intensity ya stimulus hutofautiana.

Mdada hadi kufikia hatua hiyo ujue kuna maudhi, maumivu yaliyokomaa na kuzaa hasira. Mkaka ingawa hatoi story au ukweli wote anafeel guilty in a way kwani anajua amesababisha mengi. Ukitumia kipimo cha wewe unvyoishi na mkeo na jinsi gani humuoni mkeo akifikia hatua ya kutoa kisu au kukumwagia moto hutaelewa. Tumia kipimo cha story za usaliti wa kupitiliza, utelekezaji wa familia na mengine ndipo unaweza pata picha.

Hapa ndipo tunaposhangazana, kwani mumeo/mpenzio akikuudhi unapaswa kuchukua hatua za kumdhuru? Kwa nini usisepe kivyako kuepuka hayo maudhi na maumivu kutoka kwake.

Hakuna mwenye hati miliki na maisha ya mwingine (iwe mumeo/mpenzi, mzazi, ndugu au mwana). Kila mtu awajibike kwa yanayompasa kuwajibika kwao bila kutishia kumdhuru au kuondoa uhai wa mwingine.

Simwamini hata siku moja mtu ninayekutana nae ukubwani akiniambia ananipenda, wote waongo, wake kwa waume.
 
Mwanangu jibu unalo. Ukiuawa iwe ni kwa kisu au sumu usimlaumu mkeo bali wewe mwenyewe. Unataka akwambie mara ngapi? Unataka Mungu akusaidie vipi na mara ngapi? Unataka tukupe msaada upi wakati kila kitu kiko wazi? Kama umeamua kujitoa kafara kwa ujuha wako endelea vinginevyo jibu unalo sema hutaki kulikubali. Hivi unataka mkeo atumie lugha na ishara gani umuelewe kuwa amedhamiria? Kweli la kufa hali ubani! Amka kumekucha utauawa kipuuzi tokana na ujuha wako. Kick the ass instead of licking it. Kama baba yako nikupendaye nimelazimika kutumia maneno makali ili lau uelewe. Yakikukuta usilaumu kuwa hatukuonya na kuadibu.
wadau naomba mawazo yenu kwa hili jambo nifanyeje mimi na mke wangu kwenye ndoa yetu tuna miaka sita na tumejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume,kama ujuavyo mambo ya ndoa hamuwezi kuishi kama malaika ugomvi hutokea.ila kwa bahati mbaya siku moja kama miaka miwili tumewahi kugombana kidogo ila mke wangu alinitamkia kwamba siku moja ataniua kwa kisu au kwa sumu,wiki mbili zilizopita nilikuwa nimekuja mkoa mwingine kikazi ila alikuja ghafla usiku saa tano akakuta nimelala tukalala mpaka asubuhi,asubuhi akanambia kwamba anataalifa kwamba nina mahusiano na mwanamke mmoja na nimemfungulia duka,nikamkatalia kwamba jambo hili halina ukweli kabisa tulibishana kwa mda wa masaa sita tukiwa chumbani lodge wakati huo alikuwa kafunga mlango wa chumba na funguo kaficha,baada ya mimi kuendelea kukataa ghafla alichomoa kisu alichomeka kwenye suluali na kutaka kunichoma ikabidi tuendelee kupokonyana kile kisu bahati mbaya kikanikata mkononi naomba ushauri madau nifanyeje?
 
wadau naomba mawazo yenu kwa hili jambo nifanyeje mimi na mke wangu kwenye ndoa yetu tuna miaka sita na tumejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume,kama ujuavyo mambo ya ndoa hamuwezi kuishi kama malaika ugomvi hutokea.ila kwa bahati mbaya siku moja kama miaka miwili tumewahi kugombana kidogo ila mke wangu alinitamkia kwamba siku moja ataniua kwa kisu au kwa sumu,wiki mbili zilizopita nilikuwa nimekuja mkoa mwingine kikazi ila alikuja ghafla usiku saa tano akakuta nimelala tukalala mpaka asubuhi,asubuhi akanambia kwamba anataalifa kwamba nina mahusiano na mwanamke mmoja na nimemfungulia duka,nikamkatalia kwamba jambo hili halina ukweli kabisa tulibishana kwa mda wa masaa sita tukiwa chumbani lodge wakati huo alikuwa kafunga mlango wa chumba na funguo kaficha,baada ya mimi kuendelea kukataa ghafla alichomoa kisu alichomeka kwenye suluali na kutaka kunichoma ikabidi tuendelee kupokonyana kile kisu bahati mbaya kikanikata mkononi naomba ushauri madau nifanyeje?

Pole na pia nakupa hongera ya kupendwa kupindukia na mkeo. Unajuwa hakuna penzi lisilo na wivu kwani penzi bila wivu hilo si penzi. Hata wewe jiulize, kama unapata taarifa kuwa mkeo anapigwa miti huko mkoani alikokwenda utajihisije? Kama humpendi na kutomjali utaona ni sawa na kusema bora ato.mbwe na mwingine ili nipate kisingizio cha kumwacha, sivyo? Ila ukitokwa na povu na mishipa ya shingo kukutuna basi ujuwe hayo ni mapenzi kwani hutaki kushare mkeo na mimi ama jamaa mwingine kwa sababu unampenda, si ndiyo? Sasa kwanini mkeo asikutishie kukuua kama anatetea haki yake? Kumbuka, siku hizi wanawake wengi ni matapeli haswa akijuwa kuwa una mtu wako (mkeo). Utalishwa mavitu ya kienyeji mpaka utasahau ulikotoka na kuisusa kabisa familia yako kipenzi juu ya Malaya wa muda. Hapa bongo kuna usemi kina dada wanaambiana kwamba hapendwi mtu, pochi mbele. Mademu wengi sana hapa Bongo ni feki na wanaishi maisha ya tamaa wasiyoyaweza na ndiyo maana hujidhalilisha kwa kuwapanga wanaume foleni ili waishi maisha wayatakayo. Hivyo ndugu yangu jichunge na kina Wema Sepetu. Tena nakupa hongera ya kutishiwa kuuwawa na mkeo, maana angelikata dushelele lako kwa hasira sijuwi ungefanyeje. Hongera tena kwa kupendwa na kulindwa na mkeo. Tuko wengi kumbe tupendwao, inatia raha sana kusikia hii.
 
Mkimbie muuaji huyo amekukosakosa mara ya kwanza mara ya pili atafanya kweli anaweza kuja hata na "Bistola" ili akudedishe. Fanya maamuzi haraka kabla hawajakulia ubwabwa.
 
Yani kaka wewe nimpole kiasi gani? huyo mkeo ndio kawa mume au unampenda sanaa mpaka kupitiliza?
ebu jikaze kidogo ajue kama wewe ndio mwanamme ..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom