wadau naomba mawazo yenu kwa hili jambo nifanyeje mimi na mke wangu kwenye ndoa yetu tuna miaka sita na tumejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume,kama ujuavyo mambo ya ndoa hamuwezi kuishi kama malaika ugomvi hutokea.ila kwa bahati mbaya siku moja kama miaka miwili tumewahi kugombana kidogo ila mke wangu alinitamkia kwamba siku moja ataniua kwa kisu au kwa sumu,wiki mbili zilizopita nilikuwa nimekuja mkoa mwingine kikazi ila alikuja ghafla usiku saa tano akakuta nimelala tukalala mpaka asubuhi,asubuhi akanambia kwamba anataalifa kwamba nina mahusiano na mwanamke mmoja na nimemfungulia duka,nikamkatalia kwamba jambo hili halina ukweli kabisa tulibishana kwa mda wa masaa sita tukiwa chumbani lodge wakati huo alikuwa kafunga mlango wa chumba na funguo kaficha,baada ya mimi kuendelea kukataa ghafla alichomoa kisu alichomeka kwenye suluali na kutaka kunichoma ikabidi tuendelee kupokonyana kile kisu bahati mbaya kikanikata mkononi naomba ushauri madau nifanyeje?