Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,896
Tarifa kwamba mke wa kigogo mmoja wa Ikulu alichukua Tzs 2 billion za ESCROW, si vizuri kuzungukazunguka, mhusika ni mke wa Prosper Mbena ambaye alichukua pesa hizo bank ya Stanbic. Chombo mojawapo kilishamhoji huyu mama mke wa Prosper.
Prosper Mbena ajitokeze kutetea au abishe kama mkewe hakuchukua pesa hizo.
Hapa ni JF where we dare to talk openly.
Kwenu wadau.
An escrow is:
The word derives from the Old French word escroue, meaning a scrap of paper or a scroll of parchment; this indicated the deed that a third party held until a transaction was completed.
- a contractual arrangement in which a third party receives and disburses money or documents for the primary transacting parties, with the disbursement dependent on conditions agreed to by the transacting parties, or
- an account established by a broker for holding funds on behalf of the broker's principal or some other person until the consummation or termination of a transaction; or,
- a trust account held in the borrower's name to pay obligations such as property taxes and insurance premiums.
KWANINI ISSUE YA ESCROW INA TISHA?
Wakati akichangia ripoti ya PAC
Tundu lissue alitoa pendekezo kuwa majina ya watu waliochota pesa PAP kupitia StanBic Benk ni pamoja na Shabani Rajabu Gurumo ambaye ni ndugu na JK harafu ni State Controller.
Hi indo sababu pekee ambayo inampa Kiburi Maswi, Werema, na Muhongo kwa Kuwa wanajua hata State Controller amekula
Spika Anna makinda amekiri Bungeni kuwa Suala la Escrow limeleta usumbufu ambao haijawahi kutokea tangia uhuru!
Hadi naandika hapa Bunge bado halijapata ufumbuzi na huu ni ushahidi kuwa dola nayo imepasuka.
Pamoja na Tundu Lissu kusemtaja Shabani Rajabu Gurumo kuwa amekula escrow Shs800,000,000. Spika hamkumtaka alete Ushahidi lakin Bi Mshana aliposema Mbowe amechukua fedha za escrow Kenya Zungu alimtaka alete Ushahidi.
Hapa ndo tunapata Ushahidi kuwa Maafisa wa Ikulu, wamekula escrow nan do Maana kuna mizengwe ktk suala hili.
Ikulu yamtetea Prosper Mbena
VYOMBO vya habari nchini vimeaswa kuripoti matukio yaliyofanyiwa uchunguzi wa kina na yenye kufuata maadili na taaluma ya habari, badala ya kufanya kazi kwa kuongozwa na ushabiki vinapotekeleza majukumu yake.
Hayo yameelezwa katika taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ikikanusha kuhusika kwa Katibu wa Rais Jakaya Kikwete, Prosper Mbena katika kumpa mwongozo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu ili auruhusu uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyopo katika BoT.
Taarifa hiyo inasema baadhi ya vyombo vya habari (siyo HabariLeo) vimemhusisha Mbena kuingilia mchakato wa uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 306 katika akaunti hiyo iliyoibua hoja nzito nchini, kiasi cha Bunge kuingilia kati na kutaka baadhi ya mawaziri na watendaji serikalini wawajibike kwa kile kinachodaiwa kuchota fedha za umma, jambo ambalo bado halijathibitishwa rasmi. "Huu ni uongo na uzushi.
Ni jaribio jingine la kutia chumvi katika jambo ambalo limetawaliwa kwa kiasi kikubwa na mihemko ya aina yake.
Gavana Ndulu mwenyewe anathibitisha kuwa hajawahi kupokea barua yoyote kutoka kwa Katibu wa Rais kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow.
Akaunti ya Escrow ilifunguliwa baada ya kutokea kwa mgogoro wa kimaslahi baina ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL na Tanesco.
Chanzo: Habarileo