Mke wa mtu ananitaka nifanyaje..?

Mke wa mtu ananitaka nifanyaje..?

Joined
Jan 19, 2013
Posts
35
Reaction score
11
Mimi ni kijana mwenye umri fulani tatizo linalo nisumbua ni kwamba sehemu tunapoishi kuna jamaa ameamia yeye pamoja na mke wake. Wakati wanaamia sehemu ambayo mimi naishi mara ya kwanza huyo mwanamke nilijua anakaa na kaka yake kutokana na jamaa kuonekana kuwa mkubwa kiumri kushinda huyo mwanamke ambaye mimi nilikuwa najua kuwa ni kaka yake. Huyo jamaa amepata ajali na anatembelea machuma yale ya kusukuma halafu na yeye anasogea kumbe nivyokuwa nadhani sivyo huyo jamaa alikuwa ni mmewe. Huyo mwanamke tumezoeana sana mpaka kufikia hatua ya kuchukua namba yangu ya simu. Sasa tatizo ambalo linanisumbua ni kwamba huyo mwanamke ananitaka mimi kimapenzi na anaongea maneno mabaya juu ya mmewe. Huyo mwanamke ana pesa ameniahidi kunipa kila kitu nitakacho kihitaji tatizo mimi namwonea huruma mmewe kwa hali aliyo kuwa nayo nahisi nikimkubalia huyo mwanamke itakuwa ni dhambi kumwa ambayo sijawai kuifanya tangia nizaliwe. Kwa sasa mmewe yupo kama mlemavu kwa kuwa hatembei nishaurini jamani nifanyeje nimkubali au nimkatae...!! Pesa nahitaji tatizo namuonea huruma mmewe NIFANYAJE....?
 
Mke wa mtu sumu, mume wa mtu maziwa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kama hujatembea nae achana nae kabisa na punguza mawasiliano nae ili ushinde jaribu hilo. Pesa wewe ni mtoto wa kiume komaa kutafuta zako hata kama ni kuendesha Bodaboda, acha kuwaza shortcut always is a wrongcut.

Swali la kujiuliza siku akikupiga chini itakuwaje, pesa utapata wapi na saizi pesa za kuendeshea maisha yako unapata wapi????
 
Ulishasema ni dhambi kubwa kutembea na huyo mwanamke na pia unamwonea huruma mumewe, sasa unataka ushauri wa nini?
 
mke wa mtu ni sumu,angalia utakuja kukojoa dagaa!!!
 
Mtimizie anachotaka yatakayokukuta leta humu jamvin tukushauri tena
 
Mimi ni kijana mwenye umri fulani tatizo linalo nisumbua ni kwamba sehemu tunapoishi kuna jamaa ameamia yeye pamoja na mke wake. Wakati wanaamia sehemu ambayo mimi naishi mara ya kwanza huyo mwanamke nilijua anakaa na kaka yake kutokana na jamaa kuonekana kuwa mkubwa kiumri kushinda huyo mwanamke ambaye mimi nilikuwa najua kuwa ni kaka yake. Huyo jamaa amepata ajali na anatembelea machuma yale ya kusukuma halafu na yeye anasogea kumbe nivyokuwa nadhani sivyo huyo jamaa alikuwa ni mmewe. Huyo mwanamke tumezoeana sana mpaka kufikia hatua ya kuchukua namba yangu ya simu. Sasa tatizo ambalo linanisumbua ni kwamba huyo mwanamke ananitaka mimi kimapenzi na anaongea maneno mabaya juu ya mmewe. Huyo mwanamke ana pesa ameniahidi kunipa kila kitu nitakacho kihitaji tatizo mimi namwonea huruma mmewe kwa hali aliyo kuwa nayo nahisi nikimkubalia huyo mwanamke itakuwa ni dhambi kumwa ambayo sijawai kuifanya tangia nizaliwe. Kwa sasa mmewe yupo kama mlemavu kwa kuwa hatembei nishaurini jamani nifanyeje nimkubali au nimkatae...!! Pesa nahitaji tatizo namuonea huruma mmewe NIFANYAJE....?

Ushauri: Mtafute yule kijana wa I.fm hostel kigamboni akueleze utamu wa unachotaka kufanya:target:
 
Shauri yako bei ya Kufilishwa imeshuka Magomeni kijitu kama wewe ni Tsh.50 Elfu VAT inclusive na kutawazwa bure na unakabidhiwa Pedi ya kuanzia maisha mapya!
 
Yeye anataka mapenzi mimi nataka pesa.... sijua nifanyeje nahitaji pesa na nina shida na pesa kwa sasa
 
Back
Top Bottom