Mke wa mtu ananitaka nifanyaje..?

Mke wa mtu ananitaka nifanyaje..?

Nasoma nipo chuo pia nafanya graphics and design sio kama sina kazi ya kufanya pesa napata bt yeye ameniahidi vitu vingi pamoja na pesa.

amekuahidi ee! Angalia unachoshauriwa hapa. Na je jiweke wewe katika nafasi ya mumewe kisha mkewe akutendee huo uchafu utafurahi eee! Fikiria unachotaka kukitenda je upo radhi utendewe! Sikuambia umkatalie wala umkubalie, kama una akili maelezo yote yaliyotolewa hapa yanatosha kukuongoza kufanya maamuzi unayoona ni myema.
 
unataka tukushauri nini wakati ni mke wa mtu achana naye tafuta wakwako au unahitaji uanze ile kazi anayosisitiza waziri mkuu wa uingereza cameroon kweli vijana wa siku hizi wahapendi kufanya kazi wanahitaji mijimama ya kuwalea kama huyu toa upuuzi wako hapa eti yeye anahitaji mapenzi wewe unahitaji pesa ambayo hujaitolea jasho uwe makini na wake za watu kijana kitakachokupata uje uombe tena ushauri.
 
Back
Top Bottom