Mke mtarajiwa anapoamua kuaga mchepuko ....

Mke mtarajiwa anapoamua kuaga mchepuko ....

show ya rafiki yako ya kigumu ndio maana inamvutia zaidi, huko pengine kafata pesa ama sura tu.
 
Ilikuwa ni jumatano siku ambayo nilikutana na kisa hiki ambacho leo kimetimia na kunifanya niwe mdogo kama nukta

Nilikuwa nimekwenda kumsalimia jamaa yangu ambae mwanae alikuwa amelazwa kwa kusumbuliwa na malaria na alikuwa ameshatoka hospital na nilikuwa nimekwenda kumsalimia

Mtoto wa jamaa yangu huyu ana umri wa miaka 8,jamaa anaishi peke yake na mwanae baada ya mama wa mwanae kufariki kwa ajali miaka mitatu iliyokwisha

Nilipofika nilipokelewa na jamaa yangu na tuliongea mawili matatu na ndipo aliponiambia kuwa kuna binti mmoja ambae ana mahusiano nae anakuja "kumuaga" lakini binti huyo anatarajiwa kuolewa siku ya jumamosi [leo],nilistuka na jamaa yangu aliliona hilo,ilibidi anipe kistory kifupi cha mahusiano na binti yule

Aliniambia kuwa walianza mahusiano baada ya miaka miwili kupita baada ya mkewe kufariki,alimpeda sana huyu binti na alikuwa anamipango aje azibe pengo ambalo mkewe aliliacha,lakini baada ya miezi 7 ya mahusiano yao alikuja kugundua kuwa kuna jamaa mwingine ana shea penzi kwa huyo dada,jamaa alichukia sana

Aliamua kusitisha penzi lake na huyu dada lakini binti hakuwa tayari na alikuwa anaendelea kumsihi jamaa waendelee na mahusiani,basi baada ya kujiuliza sana na kuja kugundua kuwa walikuwa wanachanganywa siku nyingi jamaa yangu aliamua kumfanya huyu dada kuwa ni "dem" wa kutulizia "mashetani" tu

Muda uliendelea hivyo na mwezi mmoja uliopita dada alikuja na kumuambia kuwa jamaa yake yule anataka kumuoa na mipango inaelekea kukamilika na baada ya mwezi mmoja [kutoka pale dada alipokuwa anatoa taarifa hii] atafunga ndoa na jamaahuyo

Jamaa yangu aliposikia hivyo hakuwa na hiyana,aliamua kukubaliana na dada huyo na kweli jamaa yangu hakumtafuta kabisaaaa,lakini baada ya wiki tatu kupita dada alimwambia jamaa kuwa angependa kumuaga kwa kukutana kimwili siku ya jumatano ijayo siku chache kabla ya ndoa[siku niliyokwenda kumsalimia jamaa yangu]

Yaliibuka mabishano kwa muda lakini jamaa yangu alijiambia kuwa kwakuwa "dem" mwenyewe kataka basi wacha ammpe kile anachohitaji,siku ya tukio ndio siku ambayo mimi nilikuwa nakwenda kumsalimia mwanae

Basi alipomaliza kunipa hiki kijistory kifupi alipokea simu kuwa dada ameshafika na anakuja,ilibidi nitoke pale nyumbani na mwanae aliyekuwa anaumwa lakini alikuwa ni kama amepona kwani alikuwa ameshachanganmka,nilitoka nae na kwenda kwenye kijiduka pale mtaani na kukaa huku akinywa juicy niliyokuwa nimekwenda nayo kumsalimia

Tulikaa pale dukani kwa muda wa saa moja na nusu na niliwaona wakitoka na walikuja hadi pale dukani na nilisalimiana na huyu dada huku nikimuangalia na nilikuwa najiuliza maswali sana

Baada ya kama dakika 3 ilikuja tax na ilimchukua na kuondoka,baada ya kuondoka ilibidi nianze kumhoji jamaa yangu ukweli wa kuolewa huyu dada na alinihakikishia na aliniambia kuwa jumamosi [leo] atanipeleka kwao na binti na nitajionea mwenyewe

Kweli leo asubuhi saa 3 nilikwenda na tulipofika niligundua kuwa jamaa yangu anafahamiana na dada wa yule "dem" wake aliemuaga kwani tulipofika alimpokea na walizungumza na kucheka sana lakini nilijua kuwa dada huyu alikuwa anajua mahusiano ya mdogo wake na jamaa yangu lakini alikuwa anajua kuwa wameshaachana

Tulikaribishwa ndani na jamaa yangu alijifanya kama vile hajaonana na bibi harusi mtarajiwa kwa muda wa mwaka,niliona pilika nyingi na hata bibi harusi nilimuona akiwa katika harakati za mwisho ili waende kanisani.baada ya hayo tuliondoka na dada mtu alitusindikiza huku akimuahidi jamaa yangu kuwa atakuwa anampa update kila baada ya saa moja

Tulipotoka niliagana na jamaa yangu na nilikuja kwenye mihangaiko yangu,jamaa yangu kanitext kuwa wanakwenda kanisani

Nimekuja hapa na maswali kibao huku nikijiuliza bila majibu

Sikuwa nimewahi kudhani kama jambo hili linaweza kuwa kweli kwani niliwahi kuambiwa matukio kama haya na sikuwa nimefikiria kuwa inaweza kuwa kweli lakini leo nimeshuhudia

Kiukweli nimekuwa mdogo kama nukta kwa kuwa huko nami nitafika,nitakuja kuoa,japokuwa hata sijajua nitakuja kumuoa nani lakini hili tukio limenifanya nisinyae kiukweli

Aisee............!!

Dunia haina huruma kiukweli!!!
 
Kivipi huoni maana ya ndoa? Kwani bwanaharusi mtarajiwa hajawai kugegeda huyo demu mpaka ushangae kwamba katolewa bikra na mshikaji wake Eiyer ...
Mhh!! Hatari sioni maana ya hiyo ndoa anayokwenda kufunga yani hata aibu hana loh!!
 
hahahaha kumbe sie tusijua kupiga shoo ka ukweli watatugegedea mademu zetu....loh basi bora niingie kwa dada poa nijiridhishe mwenyewe

jitahid mkuu yan unapigisha kwata la hatareeeeee had unakumbukwa
 
Nionavyo mm michepuko haizuiliki.Bhana tunasalitiwa sana jaman
 
hahah kuagana muhimu upate baraka uendako we hujawahi kuaga

mama yangu!!........ Kumbe unapenda na ww kuagwa. Mm sijawahi kuagwa, lakn muwe makin hizo baraka mnazozitaka znaweza kugeuka kuwa mkosi badala ya kwenda kutulia unaenda kumwagwa
 
Back
Top Bottom