Habari wanajf. Mimi nimeoa na tuna watoto wawili ila mke wangu ni mkorofi sana mpaka nafikia hali ya kuwaza ameingiwa na nini. Yaani yeye anataka awe ndio muamuzi wa kila jambo ndani ya nyumba na ukiweka idea yako anaona eti una mdharau mnataka kwenda out basi time yake ndio ifuatwe na sio yako. Na Ikitokea mabishano ya hoja na kuona anashindwa basi atavunja kila kitu km TV, pasi, deck au hata simu anairusha ukutani na kuvunjika kwa hasira. Baada ya siku anasema tununue vitu vilivyoharibika. Sasa mm naona kama ni ukichaa huu, jamani wenye mawazo au maoni naombeni kwani nafikilia mambo mengi sana ya hii ndoa