Mke kuvaa nguo za mumewe ni sahihi?

Mke kuvaa nguo za mumewe ni sahihi?

mr pipa

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2021
Posts
4,287
Reaction score
9,162
Kwa muda sasa nimekuwa niki keleka pale wife anapotupia/vaa tisheti zangu

Na kuvimba nazo kitaa wakati huo nimemnunulia zake na anazo za kutosha na kila fashion ikitoka namchukulia ila ajabu havai anaweka tu kwa begi

Mara nyingi hua namuhoji majibu sipati ya kueleweka na mimi nimemvumilia nimechoka

Kuna muda Natamani hata nichome moto nguo zangu zenyewe nibaki tu na nguo ninazo vaa mwilini

Hata nikiitwa kauka ni kuvae poa tu maana unapita kitaa na tisheti unasikia kavaa la mke wake sasa mambo gani haya

Naombeni kujuzwa hili ni haki mke kuvaa nguo za mpenzi wake

Na je hiyi hali ya mke kupenda kuvaa nguo za mumewe kitaalam linaitwaje?
 
Mbona kawaida sana,sasa unalalamika za nje,za ndani je itakuwaje mkuu?Unajua dalili uliokuwa nayo ndio chanzo cha kuanza kuchokana,unaanza kumuona mkeo kama msela mwenzio wakati huyo ni mwanamke,ila yeye bado anakupenda sana ukiona hivyo, ndio maana bado anavaa hata nguo zako ili awe anakuhisi ukaribu wako...
 
Badhi ya wanaume wa JF bwana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mwingine alilalamika mkewe anamganda ganda mara hataki akumbatiwe kila saa

Mwingine hataki mkewe avae nguo zake[emoji23][emoji23]

Mwingine eti mkewe anampiga mizinga..Sasa usipompa hela ,nani ampe?[emoji23][emoji23]

Kutwa zima, wanaume wanaleta malalamiko yasiyo ya msingi kuhusu ndoa zao compared na wanawake....
 
unajua nn, kuna mahali mnakua sio tu mume na mke , bali washikaji kabisa wa damu ( ma bladifakeni)
Exactly.Na hakuna kitu kizuri kama mpenzi /mwenza wako akiwa rafiki.Inakua rahisi kuambiana pale anapokukosea without holding grudges cuz ni rafiki yako pia.

Mfano eti just kuvaliana tshirt, Mimi nasikia fahari nikivaa tshirt ya mwenzangu na ile harufu yake inakua inanipagawisha lakini since ni marafiki kama hapendi na akanieleza kwamba bby plz usivae my cloths then sitovaa na wala sitomind..

Mawasiliano nahisi ni tatizo kubwa kwenye mahusiano kwasababu wengi ni wapenzi ila siyo marafiki.
 
He!! Kumbe mwamba kamaind kweli [emoji23][emoji23].

Bro shukuru Mungu, af cha kufanya apo, nunua unisex clothes za kutosha an mvae wote.
 
Ili swala kuna siku nilivaa tshirt (jezi mnaita) ya mpenzi wangu kumbe ni sare ya timu yao mi Niko nayo tu mtaani. Wakaniona Wenye nayo. Wapo mazoezi akapigwa faini
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]daah ulitisha pepe ndio maana mi sipend avae
 
Back
Top Bottom