Mke kufurahia anguko la Mume

establishment

JF-Expert Member
Jun 27, 2015
1,630
2,378
Katika maisha ya ndoa niliwahi kushuhudia mke wangu wakati fulani anafurahia magumu ninayopitia kazini (demotion na suspension). Tukigombana kidogo tu anabwatuka na utafukuzwa hiyo kazi. Lakini nashukuru Mungu leo hii nafuu kubwa Sana (nilipata kazi nyingine na mshahara mkubwa Zaidi).

Wakati fulani nawaza akili za hawa wanawake wa kichaga siwaelewi). Anyway, pamoja na yote bado tupo pamoja kwa miaka 21 sasa, toka 8 Januari 2000.

La ajabu siku nimepata kazi nzuri zaidi ndo wa kwanza kujibaraguza eti Hongera!

FUNZO:
Mume (hasa vijana) chase ur dream achana na maneno ya mke (akiwemo Mama Mkwe).
 

Attachments

  • kijitonyama_lutheran_church_20210208_212149_0.mp4
    7.4 MB
Kama mlikuwa mnaishi paka na panya ndani ya ndoa yenu mkuu lazima tu uambiwe hivyo

Ila kama mnaishi ndoa yenye masikilizano na kuheshimiana hukuti kabisa hizo mambo tena mke anakuwa mfariji wako mkuu kwa chochote kile
 
Inategemea na matumizi ya hayo mafanikio ya mume.

Sisi wanaume wengine tukipata pesa/mafanikio ndo kwanza, michepuko, pombe vinashika hatamu.

Unakolea kwa michepuko na pombe, dharau sana kwa mkeo mpk unaitelekeza familia nzima.

Wengine wanahamishia makaz kabisa kwa mchepuko.

Zikiisha unarudi mikono nyuma,kichwa chini kwa mama watoto myajenge upya.

Sasa,
Kwa Hali Kama iyo Ni mwanamke wa Aina gani atafurahia mafanikio yako Kama ukizipata unakua ivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nna shemej angu mmoja aliwahi vunja vioo vyote vya gari ya mme wake.

Afu akajikausha kimya na yeye mwenyewe akawa anashangaa kilichotokea.

Jamaa akahisi labda majirani waswahili wamemfanyia fitna au jamaa aliekua na ugomvi nae bar siku za nyuma.

Kutokana na UCHUMI kutokua vizuri, jamaa ikabidi aipaki Kwanza gari uani.

Siku moja jamaa karud nyumban na bodaboda kasahau document ya ofisi.

Akabisha hodi hajafunguliwa, ikabid akagonge master bedroom.

Kufika dirisha, akaskia wife anaongea na sim.

Kuiskiliza kwa makin.
akaskia wife wake akimsimulia SHOGA ake jins alivyomkomesha mme wake kwa kumvunjia vioo vya gari sahv anatumia bodaboda na daladala na anawai kufika nyumban.

jamaa aliingia ndani akampiga sana mkewe.

Mkewe kipigo kilipomzidia anakimbilia ukweni.

Kikawekwa kikao Cha usuluhishi.

Mwanamke akafunguka kua,
Tangu jamaa anunue gari nyumba imekua ya Moto.

Anapakia na kufanyia mapenz kwenye gari na wanawake.

Ameshamkamata mara tatu na Kukutana condom za kutosha ndani ya gari ila haskii.

Hasimamii Tena biashara za familia, matumizi ya gari yamekua ni makubwa mno na hawaingizi chochote.

Walkua na biashara 3.

Ila ndani ya mwaka, imebaki biashara Moja. Na chanzo ni mwanaume anachukua tu pesa.

Biashara ya baa ndo ilimuuma zaidi maana jamaa kama meneja akija mwanamke mzuri lazima akiaga anaondoka ataomba ampe lifti.

Akirudi kalewa chakali Ela zote za mauzo hana na gari kaigonga, Ela nyingine inatoka gereji kunyoosha gari.

Yaan mwanaume ni kuzurura tU siku nzima viwanja vya starehe na wanawake.

Kwaiyo, akaona hii gari ikiendelea kuwepo kwenye hi familia italeta maafa zaidi.

Ndo maana akaaamua kuvunja vioo vyote maana anajua uwezo wa kuikarabati kwa Sasa hatuna.

Ukzingatia watoto wawili wamesimamishwa shule kutokana na ukosef wa ada, na jamaa alkua haoneshi kuguswa na ilo.

Aisee Kiukweli,
kwenye kikao nlkua ni mskilizaji tu maana wazee ndo walkua waamuz.
Ila kimoyomoyo nlimsapoti mwanamke kwa maana namjua vyema alivo jamaa angu akiwa na pesa.

SOMETIMES WANAWAKE WANAPITIA VIPIND VIGUM SANA. Tusiwabeze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom