Nna shemej angu mmoja aliwahi vunja vioo vyote vya gari ya mme wake.
Afu akajikausha kimya na yeye mwenyewe akawa anashangaa kilichotokea.
Jamaa akahisi labda majirani waswahili wamemfanyia fitna au jamaa aliekua na ugomvi nae bar siku za nyuma.
Kutokana na UCHUMI kutokua vizuri, jamaa ikabidi aipaki Kwanza gari uani.
Siku moja jamaa karud nyumban na bodaboda kasahau document ya ofisi.
Akabisha hodi hajafunguliwa, ikabid akagonge master bedroom.
Kufika dirisha, akaskia wife anaongea na sim.
Kuiskiliza kwa makin.
akaskia wife wake akimsimulia SHOGA ake jins alivyomkomesha mme wake kwa kumvunjia vioo vya gari sahv anatumia bodaboda na daladala na anawai kufika nyumban.
jamaa aliingia ndani akampiga sana mkewe.
Mkewe kipigo kilipomzidia anakimbilia ukweni.
Kikawekwa kikao Cha usuluhishi.
Mwanamke akafunguka kua,
Tangu jamaa anunue gari nyumba imekua ya Moto.
Anapakia na kufanyia mapenz kwenye gari na wanawake.
Ameshamkamata mara tatu na Kukutana condom za kutosha ndani ya gari ila haskii.
Hasimamii Tena biashara za familia, matumizi ya gari yamekua ni makubwa mno na hawaingizi chochote.
Walkua na biashara 3.
Ila ndani ya mwaka, imebaki biashara Moja. Na chanzo ni mwanaume anachukua tu pesa.
Biashara ya baa ndo ilimuuma zaidi maana jamaa kama meneja akija mwanamke mzuri lazima akiaga anaondoka ataomba ampe lifti.
Akirudi kalewa chakali Ela zote za mauzo hana na gari kaigonga, Ela nyingine inatoka gereji kunyoosha gari.
Yaan mwanaume ni kuzurura tU siku nzima viwanja vya starehe na wanawake.
Kwaiyo, akaona hii gari ikiendelea kuwepo kwenye hi familia italeta maafa zaidi.
Ndo maana akaaamua kuvunja vioo vyote maana anajua uwezo wa kuikarabati kwa Sasa hatuna.
Ukzingatia watoto wawili wamesimamishwa shule kutokana na ukosef wa ada, na jamaa alkua haoneshi kuguswa na ilo.
Aisee Kiukweli,
kwenye kikao nlkua ni mskilizaji tu maana wazee ndo walkua waamuz.
Ila kimoyomoyo nlimsapoti mwanamke kwa maana namjua vyema alivo jamaa angu akiwa na pesa.
SOMETIMES WANAWAKE WANAPITIA VIPIND VIGUM SANA. Tusiwabeze.
Sent using
Jamii Forums mobile app