angelita
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 3,017
- 2,446
Tukio lakusikitisha limetokea mtaani kwetu asubuhi.
Huyu Baba alikuwa na mke akamuacha akaoa mwingine ambaye ndiye alikuwa anaishi naye hadi mauti yalipomkuta.
Ni mtu ambaye alikuwa na maisha mazuri, kabla hajaoa huyu bibi mdogo alikuwa amejenga tayari nyumba 3, 1 anaishi yeye na mke mdogo na 2 alipangisha.
Huyu bibi mdogo akamwambia wauze nyumba zile mbili zilizopangishwa mwanaume akauza hela kampa huyu mkewe mdogo, ikabaki wanayokaa hapo ndipo sekeseke lilipoanza mwanamke anataka na iyo iuzwe, mwanaume kuona ishakuwa shida akachukua hati akampa mwanaye mkubwa wa kiume aliyezaa na mkewe.
Mwanamke alivyoona hati haipo ugomvi, sasa leo asubuhi mumewe kakutwa kafa bafuni. Mtoto anahadithia, "nilimuona mama anaweka vitu kwenye chai ya baba, mimi nikamwambia baba usinywe iyo chai hakunisikiliza, alivyomaliza akaenda chumbani ndiyo mama akatoka nje kuwaita watu".
Mke kabebwa na polisi, maiti imeenda kufanyiwa uchunguzi.
Inasikitisha sana kweli mtaka vyote hukosa vyote kwa pupa.