Mke kama msaidizi wako

Mke kama msaidizi wako

Kwa watu wanyonge wachini vijana maskini kabisa wanaoishi chini ya 5000 kwa siku,ambao bado hawajipata ,hata watumishi wa umma wa kada za chini,kisaidiana kiuchumi ni point pia ..
japo kwa ma wakiojipata kiuchumi haiwezi ku make any sense.
kusaidiana kiuchumi mwanamke chake chake, mwanaume chake cha familia. au unamaanisha jamii gani ya ambao hawajajipata ambayo mimi siifahamu
 
mwanamke ni sehemu ya mwanaume ,kiroho ,ADAMU aliumbwa akiwa na nafsi zote ndani ya mwili mmoja yani mwanamke na mwanaume ndani ya mwili wa ADAMU.
Baadae zikawa separated mwanamke kutoka kwa mwanaume (HAWA).
Hawa wawili ni partner kila mmoja ni part ya mwenzake flesh of my flesh mifupa kutoka mfupa wangu.

na hawa wote wamekuwa mwili mmoja ,ni kitu kimoja.

unajua mwanaume na mwanamke wote wana homoni za kike na za kiume ila kwa viwango tifauti na kuna wakati anaweza kuzaliwa kiumbe chenye jinsia zote mbili hermaphroditis kama wale wanyama au mime ambayo inajizalisha yenyewe ni dume na jike hapo hapo.
japo asili ni moja katika umoja japo ni kitu kimoja ila tumetenganishwa mke na mume tofauti kwa sababu maalumu ya kusaidiana ,tunaunganishwa kuwa kitu kimoja mume na mke.
KUSHIRIKIANA na KUSAIDIANA
na UMOJA kwa sababu mume na mke ni wamoja asili wameumbwa kila mmoja kwa ajili ya mwingine na wanaposhirikina kibiolojia kiroho wanakuwa tena mwili mmoja.
WASHIRIKIANE na KUSAIDIANA kwa UMOJA wao kimwili na kiroho na kiakili.
Ungeandika maneno machache tu ila life partner ni zaidi ya msaidizi
 
basi ipeleke jukwaa la "habari na hoja mchanganyiko" huku unatuchanganywa tunachanganyikiwa
lengo langu niposti kule mchanganyiko ,vidole vimeteleza.....lakini still ina fit kukaa huku kwa context ya kusaidiana KIUCHUMI kati ya mke na mume

huwa naiangalia nembo ya taifa
ina bibi na bwana wote wanashirikiana 50 fifty..usawa wa hamsini kwa hamsini..katika shughuli za kiuuchumi..katika kuinua familia zetu jamii na taifa kwa ujumla ..mke na mume ..bibi n bwana..hata katika familia kukiwa na KUSAIDIANA kushirikina wengine wanaita PARTNERSHIP

KWA UMOJA NDIO NGUVU ..umoja na nguvu.
 
Sasa kama Taifa tu linajengwa na wanawake na wanaume ,tena wanawake wanapata zile nafasi za hamsini kwa hamsini hata raisi ni mwanamke

sasa WHY NOT kwenye kujenga familia isiwe hivyo hivyo kusaidia/kushirikina/pertnership

maana Taifa linatikana na familia imara ,familia imara zinajenga taifa imara.

KUNA LEO NA KESHO
kuna kuugua kwa mwanaume,kuna kufilisika ,kuna kunanguka kiuchumi kwa mwanaume na kuna kifo.
Mwanaume naye ni mtu kama ulivyo mwanamke ,si umeona wanawake wengine wamekuwa viongozi wetu wanaongaza wanaume na taifa kabisa.

SIAMINI katika uhafidhina wa kuwafungia wanawake ndani au kuwaondoa makazini..NAFASI YA MWANAMKE KATIKA JAMII.
naamini wanawake nao wanaweza kuchangia katika shughuli za kiuchumi za familia tena wakati mwingine kuliko hata wanaume,tuwape nafasi, tusiwafunike vupaji walivyopewa,aisee kama mdogo wangu mmoja aisee mke wake ana kicha cha biashara yani alipompa mtaji tu kafungua biashara nyingi na mtaji nanfaida zikaongezeka mara dufu na hii imesaidia kuinua kipato cha familia kwa kushirikiana partnership kuliko angemkataza na kumfungia ndani.
 
kusaidiana kiuchumi mwanamke chake chake, mwanaume chake cha familia. au unamaanisha jamii gani ya ambao hawajajipata ambayo mimi siifahamu
mwanamke chake kwa mapenzi yake amkinaweza kikawa cha familia pia ,ndio katika baadhi ya scenario na katika hali ya chini,tuwe tu wakweli kuna wanawake wanamchango significant kabisa katika familia.(hasa nyingi ya familia za hali ya chini).
 
mwanaume anaumwa maradhi sugu amelala kitandani hajiwezi kwa miezi 6 na ana mke na watoto na alikuwa ni day worker atoke ndio ale ,kama winga au dalali au afisa usafirishaji .
Mke anachukua usukani anaendesha familia ,na cha mwanamke kinakuwa cha familia ..sio cha mwanke cha mwanake cha mwanaume cha familia.

na hii inakuwa rahisi kwa mwanamke ,kama huyo mwanamke alishakuwa kwenye huo mfumo wa kushirkiana na kusaidiana na munewe kabla ya munewe kupatwa na maradhi au majanga.
POSITIVE THINKING tu...
 
just assume mke ni raisi wa nchi au waziri au mfanyabiashara mkubwa milionea na mume ana kipato kiduchu sana sana.
Halafu mke akaaanza kusaidia familia kuna ubaya gani?

na nani atakaza aseme sitaki mke wangu achangie chochote kwenye hii familia ,wala sitaki mke wangu asaidie chichote wala yeyote katika hii familia kwa sabau mimi mumewe ndio mwanaume hata kama sina uwezo ila mimi ndio mwanaume.

Kuna ubaya gani kuwawezesha wake zetu wafanikiww hata kutuzidi sisi kwa faida ya familia hata siku ikitokea bahati mbaya umekwama una back up au haupo duniani unajua nimewaacha katika mikono salama.

Kuna faida gani kumfugia mke ndani asitoke kwa sababu ya wivu ili hali huwezi kumchunga bibadamu kama mnyama.
 
Hv mkiweka 50% ya mume na mke 50% kwenye kila jambo kuna athari gani ?

Vipi ambao hawaeki hizo percent na bado inakula kwao imekaaje hapo ?

Je kwann mwanamke akumbatie Mali zake tena kwa Siri bila mume kujua Ila mwanaume ukiwa nazi wanaanza hivi ukifa ghafla,
haya mambo ya kufanya maendeleo yako pembeni kwa siri bila kumshirikisha mwenzi wako pia yana hasara zake .
Kuna mlinzi wa nyumba alikuwa analinda nyumba iliyokuwa kwenye finishing kumbe boss wake alikuwa anajenga kwa siri..mwisho wa siku kajikuta ameokota nyumba sasa huu ni mwaka wa 30 amejiokotea nyumba mana yule boss wake hakuonekana tena sijui alishakufa hatujui?wala ndugu zake hawajui na zamani hata simu hazikuwepo kwa wingi.
.kadhalika viwanja na akunti za benki..haya mambo ya kuficha ficha siku ukidobdoka ghafla utawafaidisha wengine badala ya familia yako .
Ndio umuhimu wa kushirikiana na kusaidiana partnership kama kila mmoja anafanya maendeleo yake kwa siri pembeni..kwa kumficha mwwnzake ..kuba faida gani ya kuwa pamoja kama hamna ushirika hamna umoja na hamko pamoja ..kwa nini mnaishi pamoja.
 
Nimetulia zangu nasema ngoja niingie JF kwenye jukwaa langu pendwa Biashara,uchumi na ujasiliamali nakutana na mada za ndoa doh 😣 😣 😣
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...


Cc: Mahondaw
Ndoa ni kwa ajili ya watu wenye akili,ndoa ni zaidi ya tamaa za mwili,feelings..

inabidi uingie kwenye ndoa KIAKILI sio kwa HISIA nafikiri hata maandiko yanaelekeza wanaume watumie AKILI kuishi na wake. sio hisia.

aisee usipokuwa na AKILI ya ndoa UNAKUFA KABISA ..utakutana na DELILA na wewe utakuwa SAMSONI mwisho wake ni kuteseka kwa ajili ya nyege zako na hisia zako ndio zitakazokuua ..na kupoteza mali zako zote na uhai wako ...ukikutwa na DELILA WAKO.


Nafikiri katika katu Mungu ametupa cha muhimu ni AKILI...TUMIA HIYO AKILI KATIKA KILA JAMBO... (tumia akili)

WATU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

na wanakufa kweli..kama nzi kufia kwenye kidonda..
 
well said
1.)dont fall in love but stand in love(penda kwa kutumia akili sio kwa moyo/hisia)

2.)use your mind instead of your feelings(tumia akili usipelekeshwe na nyege)

3.)oa mwanamke anayekupenda wewe kama ulivyo..uanaume wako tu wewe mwenyewe akikuona tu anashiba .

4.)usitumie NGUVU nyingi kubembelea kushikilia penzi(USILAZIMISHE KUPENDWA)
.usimsujudie mwananmke ,akuhurumie kukupenda yani kama anakusaidie ...usimsujudie usimuabudu mwanamke ili akupende

..5).oa mwanamke ambaye hayupo tayari kukupoteza anayetambua thamani yako wewe kama mwanaume uanaume wako

6.)USILILIE MAPENZI...ni aibu mwanaume kusema hawezi kuishi bila huyo...usimbembeleze ..asikupande kichwani...usionyeshe udhaifu,usikiri udhaifu...usimuabudu...akitaka kwenda MUACHE AENDE...amekupunguzia matatizo huko mbeleni....

ukiruhisu nyege hisia zitawale badala ya akili itawale ,..utakuwa mwanaume dhaifu sana ..utamlamba miguu mwanamke atakutawala ..tena..atakudharau sana.
 

Attachments

  • Screenshot_20260221-161550.jpg
    Screenshot_20260221-161550.jpg
    98.5 KB · Views: 0
  • 1_nu99ld4ANY7xBKPUfhuekw.jpg
    1_nu99ld4ANY7xBKPUfhuekw.jpg
    41.1 KB · Views: 0
JIFUNZE KUELEWA MAANA YA KUOA/KUOLEWA KABLA YA KUINGIA HUKO.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Kama wengi wetu tujuavyo, Ndoa ya kwanza ilifungishwa pale Edeni na Mungu mwenyewe. Na ilikuwa ndoa takatifu, iliyobeba msingi na dira ya ndoa nyingine zote zitakazofuata jinsi zinavyopaswa ziwe.

Katika ndoa ile ilihusisha Mtu mume mmoja (Adamu) na mtu mke mmoja (Hawa)..Kwa kupitia wazazi wetu hawa wawili ndio sisi sote tumetokea…ikiwa na maana kuwa ndoa kamili na takatifu inahusisha mume mmoja na mke mmoja…na si Zaidi. Hicho ni kigezo cha kwanza na cha muhimu.

Pia kabla ya ndoa ile kufungishwa, Maisha yalianza na Adamu kwanza, Mungu alimpa Adamu mimea, mashamba ya kulima, makazi na kila kitu, hapo kabla Hawa hajatokea…na Adamu akaanza majukumu yake ya shughuli pale Edeni kabla ya Hawa kutokea…Na Hawa alipotokea alikuwa kama msaidizi tu wa kazi ambayo tayari ilikuwa imeshaanza. Ikiwa na maana kuwa Mwanamume yoyote kabla hajadhamiria kuoa ni lazima angalau awe na mahali pa kujishikiza ili aweze kumhudumia huyo mkewe anayekuja kumwoa…

Na kumbuka Mungu hakumleta Hawa kwaajili ya tamaa za mwili za Adamu, hapana bali alimleta ili awe msaidizi kwake, kwa namna zote, kifikra, na hata katika kazi zake za kimaendeleo Adamu alizokuwa anazifanya…Ikiwa na maana kuwa lengo la kwanza la ndoa sio kukutana kimwili kama inavyochukuliwa sasa na wachache wasio na maarifa ya kutosha.

Hivyo mwanamke jukumu lake kubwa katika ndoa ni kushirikiana na mume wake, na kuyafanya majukumu yote ambayo mume wake angepaswa ayafanye, ikiwemo ya kihuduma na ya kiuchumi, Hawa hakupelekwa kwa Adamu kumtoa Adamu pesa!..bali awe msaidizi….Maana yake kitu ambacho hakijakaa sawa au hakijakamilika mikononi mwa mwanaume, mwanamke anakiweka sawa na kukimalizia.

Na jukumu kubwa Zaidi mwanamume na mwanamke walilopewa ni kujiepusha na Uovu…Na shetani huwa anawatumia wanawake wengi kuharibu ndoa kuliko wanaume..Kama Hawa mzazi wetu wa kwanza angekaa katika nafasi yake na kujiepusha na uovu, leo hii duniani kungekuwa ni paradiso, lakini kwa kuacha majukumu yake ya USAIDIZI na kwenda kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambayo Mungu hakumwagiza matokeo yake ndio yakawa yale…Na hata sasa mwanamke akiacha majukumu yake na kujikita katika ulimwengu huu, katika usengenyaji, umbea, katika kutoa siri za mume wake nje, katika kutomheshimu mume wake, kumdharau, kumdhalilisha, kumwaibisha, kuvaa kikahaba, kuwa mhuni, mlevi,mtu mwenye mizaha na kila aina ya udunia, anajiharibia mwenyewe na anaibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe..

Na Ndoa takatifu ni lazima ihusishe watu wawili wenye Imani moja..Ni kinyume na maandiko kuoa/kuolewa na mtu asiyeamini baada ya wewe kuamini, Kama umeshamwamini Yesu Kristo na uweza wake hupaswi hata kidogo kutafuta kuoa/kuolewa na mtu asiye mkristo. Na ndoa yoyote ya kikristo lazima iwasilishwe na kubarikiwa mbele ya kanisa la Kristo. Sio sahihi kabisa kufunga ndoa za kimila wala za kiserikali baada ya kumwamini Yesu Kristo.

Na ni lazima kulipa mahari kwa ndugu wa mwanamke kabla ya kumwoa, kama huo ndio utaratibu wa familia ya mwanamke, Adamu hakulipa mahari kwasababu mkewe Hawa ,chimbuko lake lilikuwa ubavuni mwake, hakuwa na wazazi wala ndugu…lakini sasa kila mwanamke anao wazazi/ndugu/walezi…Huko ndiko alikolelewa, hakulelewa ubavuni mwako,…kwahiyo ni wajibu kumtoa kwa wazazi wake kwa utaratibu huo maalumu wa kulipa mahari…

Hata Hawa alipotolewa ubavuni mwa Adamu, Bwana Mungu aliparudishia nyama pale palipotolewa ili Maisha ya Adamu yaweze kuendelea, hakuacha shimo pale wala kidonda!…Na hali kadhalika unapomtoa mwanamke kwa wazazi wake ni lazima uzibe pengo uliloliacha pale, na hilo unaliziba angalau kwa mahari, sio unamwiba na kuacha huzuni kule na malalamiko na laana na maumivu.

kama utashindwa kulipa mahari ya kiasi hicho kidogo cha fedha utawezaje kuitunza na kuihudumia familia yako inayokuja huko mbele, ambayo pengine itahitaji matunzo ya gharama nyingi kuliko hizo za mahari??…kama hutaki kutoa mahari, maana yake bado hujaelewa maana ya kuoa, hivyo unapaswa ungoje mpaka utakapoelewa vyema maana ya ndoa ndipo uoe.

Na mwisho biblia inatuambia kuwa wakati tuliobakiwa nao ni mchache sana…wale ambao wameoa na wawe kama hawajaoa…ili muda mwingi tuutumie katika kuutafuta Zaidi ufalme wake na haki yake kwasababu unyakuo upo karibuni, na mbinguni tuendako hakutakuwa na kuoa wala kuolewa, yatakuwa ni mambo mapya huko ambayo ni ya muhimu Zaidi kuliko haya.
 
SWALI: Je ulipwaji wa Mahari ina ulazima wowote?..je ni Agizo la kibiblia? Na kama ni hivyo Je! Adamu alitoa mahari kwa nani ili ampate Hawa?


JIBU: Ndoa ya kwanza ilifungishwa na Mungu mwenyewe…Na hakukuhusika mahari wala viapo…Hiyo yote ni kwasababu Hawa hakuwa na Baba wala Mama…

Lakini sasa wake zetu wanao wazazi wao..hatuwatoi ubavuni mwetu kama Adamu alivyompata Hawa..

Hatuna budi kuwatoa kutoka kwa wazazi wao… Na wazazi wao waliwalea na kuwatunza kwa gharama zao.

Hivyo sio vyema kuwaiba kutoka kwa wazazi wao na kuwafanya wetu…Hatuna budi kufuata taratibu za kuwatoa kutoka kwao na kuwaleta kwetu…Na taratibu hizo zinahusisha ulipwaji wa mahari. Ulipwaji wa mahari hakumaanishi kumnunua huyo mwanamke…hapana! Bali kumthaminisha Yule binti kwamba hajaokotwa tu.

Laiti kama tungekuwa tunawapata wake zetu kama Adamu kwamba Mungu anatuletea usingizi na kuwatoa kutoka ubavuni mwetu..hapo kungekuwa hakuna haja ya mahari wala ndoa kanisani..**hapo mahari ina ulazima wowote?..haina ulazima kwasababu wametoka kwetu(kwenye miili yetu kama Adamu)…lakini tulio nao hawajatoka kwetu wametoka kwa wengine… Hivyo ni lazima mtu upitie hatua **za kuposa, na kuposa kuna taratibu zake ikiwemo mahari,

Luka 2:4 “Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;

5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba”.

Hivyo hatua hiyo ikishavukwa kinachofuata sasa ni kwenda kanisani…Tulipowatoa! tumewatoa katika jamii..watu wote walikuwa wanajua binti Yule hajaolewa..hivyo binti kwa idhini yake sasa hana budi kwenda kukiri mbele ya umati wa jamii ya watu wake na mbele ya kanisa la Kristo na mbele ya Mungu kwamba amekubali kwa idhini yake mwenyewe kuolewa na kijana huyo..Na kijana naye vivyo hivyo anatamka kwa kukiri..kuwa ushuhuda..Na hapo ndipo Mungu anapoiridhia kuwa ni ndoa takatifu ya kikristo.

Hivyo ndoa na mahari ni mambo ya kimaandiko kabisa hata Bwana wetu Yesu Kristo aliingia gharama ili kututoa katika ulimwengu…Ilimgharimu uhai wake ili tu atupate sisi bibi-arusi wake..

Bwana akubariki.

Je umeithamini gharama Kristo aliyoingia ili akupate wewe?..Damu yake ilimwagika pale msalabani kwaajili yako na yangu..ili sisi tuwe mali yake yeye…tuondoke katika ulimwengu tukaishi naye..Kama hujaokoka unasubiri nini?..siku ile utakuwa mgeni wa nani kule au utakuwa mfano wa wale wanawali wapumbavu tunaowasoma katika kitabu cha Mathayo 25?..Uchaguzi ni wako, mlango wa rehema bado upo wazi.
 
Back
Top Bottom