Nimefurahishwa sana na hitimisho lako kuhusu huduma hizo nilizozitaja kuwa ni expression of love!
Inakuwaje basi mtu anaposhindwa ku express love kwa namna.mtindo huu wakati mwingine inamgharimu maisha? Tumesoma/kusikia mwanaume akimpiga na wakati mwingine kumuua mwenzi wake kisa ati alichelewa kupika, hakufaya jambo fulani etc.
binadamu ni kiumbe wa ajabu sana, wakati mwingine hufanya kitu bila kujua sababu ya kukifanya na moja ya mambo yanayofanywa maranyingi bila wahusika kujua sababu ya kuya fanya ni kuoa nakuolewa.... kimsingi kila mtu ana sababu zake na si lazima zifananne na sababu za wengine ama sababu zinazokubalika katika jamii. matendo ya kupika, kufua nk. katika ndoa wakatimwingine ndio mapenzi yenyewe na ni halisi kama mapenzi na sio mara zote ni "just"
expression of love bali wakati mwingine ni neutral duties zisizoweza kuathiri mapenzi yao kwa namna yoyote ile.
kuna watu wanaoa kwa ajli ya kufanyiwa kazi hizo tu basi, kuna baadhi unakuta kama watoto anao tayari, kama ni accompany hana upweke wa kiwango chochote na kama ni msaada wa maisha hana uhitaji huo kwa kiwango chochte ila anahitaji mtu wa kushughulika na mambo hayo ya kupika usafi , kutunza mazingira, mifugo nk na ambaye atamwamini hadi chumbani kwake na atakayeweza kumhudumia namna yoyote takayotakiwa mfano wakati wa ugonjwa bila kupata vikwazo vya mipaka ya kijamii (social distance). ndoa nyingi za mitala huwa zina maudhui kama haya. na ukichunguza utakuta maeneo ya vijijini amabako "wage labor" haijazoeleka (hasa siku za nyuma kidogo) mitala ilikuwa suluhisho, na kuna wakati hata mke mkubwa humlazimisha mumewe aoe mke au wake wengine ili yeye apumzike hizo "kazi" hasa baada ya umri kuanza kumtupa mkono....
magomvi yanayolipuka atika ndoa kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu hayo yaliyotajwa ni "matokeo" tu ya ugomvi ambao tayari unayala mapenzi yao na si "ugomvi" wenyewe ndio maana utasikia mara nyingi abla ya kipigo kuwa mfano "... we mwanamke siku nyingi nakuona unaanza kiburi, sasa leo nitakuonyesha..." hii inaonyesha kuwa nyumba ilikuwa na utulivu tu wa utambo na sasa hali imetibuka...
nimeona maishani mwangu ndoa zenye sababu tofauti nyingi tu.. kwa mfano,
1.ndoa zinazotaka watoto tu
2. zinazolenga kuthibitisha kuwa wahusika wamekuwa wakubwa
3. zinazolenga kusaidia wanafamilia wengine kwa kuwapa mahari kupunguza umasikini wa familia
4. kusawazisha tofauti za kijamii hasa pale ambapo mfano agemates wote wamo ndani ya ndoa na waahusika wanataka kuingia ili walingane na agemates
5. kupunguza kero toka kwa jamii kuwa "utaoa lini?"
6. uthibitisho wa kutokuwa na nuksi maishani (hasa kwa wasichana)
7. kudhibiti tamaa za mwili
8.nk
so mjadala ni mpana na mrefu, sababu ni multidimensional......