WomanOfSubstance
Platinum Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 975
Kwa akina kaka/baba waliooa au wanaotarajia kuoa.
Mmeoa au mnataka kuwa na mke ili iweje?
Naona baadhi ya wanaume wakidai huduma mbalimbali kuanzia kupikiwa, kufuliwa, kuoshewa vyombo, kutunziwa na kulindiwa nyumba, kuburudishwa nakadhalika. Hapo sijaongezea kuzaliwa watoto na matunzo yake, kutunza wazazi wazee au wasiojiweza, kuhudumia miradi na mifugo.
Nadhani siyo vibaya kuwa na uelewa wa pamoja katika hili.Huenda itasaidia katika management of expectations na pia kurekebisha pale ambapo hapako sawa kwa wote.
Hivi kweli mke ni kwa ajili hii? Hebu tupate mawazo kutoka kwenu. Akina dada/mama mnaweza kuchagiza.