Mke hataki ndugu wa mume:Msaada please. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke hataki ndugu wa mume:Msaada please.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ChiefmTz, Feb 7, 2011.

 1. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Kuna jamaa yangu kaniomba ushauri juu ya tatizo linalomkabili. Yeye kaoa mke. Baada ya kufiwa na mdogo wake wa kike, ndugu waligawana watoto wa marehemu na yeye(jamaa) akapewa mtoto m1 ili amtunze na hasa ikizingatiwa kuwa hakuwa na baba. Matatizo ya mke ndo yakaanza. Mara simtaki huyo mtoto kwa kuwa hukunishirikisha. Mara mtoto huyo ameshndikana huko alikotoka kwa kuwa ni mtundu. Mke ameendelea kusistiza kuwa hamtaki huyo mtoto licha ya kupita miaka 3 sasa. Kutokana na presha ya mke wake, jamaa aliamua kutafuta shule ya boarding ya watoto yatima lakini bila ya mafanikio. Pia aliwahi kumchukua ndugu yake mmoja ili amsaidie kwenye biashara zake lakini kelele za kumkataa zikasikika na hatimaye yule kijana akaondoka. Jamaa wiki iliyopita aliombwa na ndugu wa mke ampokee kijana wake akae kwake ili ajiandae kure-sit mtihani wa fm4 mwaka huu. Jamaa hakuwa na hiana akamkubalia bila ya kumshikisha mke wake huku akihofia kelele za mke wake kwa kutomshirikisha. Kijana kafika na hakuna kelele.
   
 2. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Ila kelele ndo zimezidi za kumkataa yule mtoto yatima. Jamaa anauliza afanyeje? Je naye amtimue ndugu wa mke? Msaada wenu wanajf
   
 3. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Du jamani hakuna wa kunipa point za kumshauri huyu jamaa yangu? Au watu wako bize na Dowans. Jamani naombeni maoni yenu.
   
 4. H

  Haika JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ngoja nikupe ushauri, mimi kama dada wa kichaga.
  Kwa kuwa upependa kutaja kabila la mke bila kutaja kabila la mume unadhani huo ukabila wa mke ni muhimu katika ushauri unaotegemea?

  Basi ni hivi,
  1. Mwambie amuache huyo mwanamke atafute wa kabila lake au lako wewe.
  2. Awape funzo ndugu zake wote wasijeoa wachaga kwani watawakataa ndugu zao na hao wanawake wataleta ndugu zao nyumbani.

  Iwe onyo na fundisho kwao.
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Una hasira tuliza munkari sister sio wachagga wote wenye tabia hizo mie nadhani kuepuka kuvuruga ndoa jamaa kama kweli alimpenda na anampenda mke wake awe anajaribu kumshirikisha kwa kila jambo sio kujichukulia maamuzi matatizo kama hayo yanatokea kwa familia nyingi sana kuhusu kabila ni tatizo mimi ni mhehe ila nakataa kabisa kwamba sio wachaga wote wenye tabia hizo kwasababu nina mifano mingi tu kwamba kuna ndugu zangu wameoa wachaga na mbona wake zao wanapokea wageni kila siku na wanaishi nao vizuri na kuna ndugu zangu pia wameolewa na wachaga lakini naona life inakwenda fresh tu tatizo hapo hata mume anachangia kwasababu hamshirikishi mkewe kwa kila jambo na anachukulia kama kila kitu ni rahisi tu sasa wewe mshauri jamaa kama anaweza huyo mtoto ampeleke tu shule za boarding na baadae akae na mke wake waongee juu ya hilo pia hata hawa watoto wa kufikia kuna wengine unakuta ni kweli watukutu na wakorofi sana unamkatalia hili anafanya lile ukimkataza hili anafanya hili mke lazima achukie kama kila siku TV na redio vinaunguzwa au mtoto tuchukulie anakunywa pombe na nyumba hairuhusiwi kunywa pombe kwa hiyo always nyumba hujengwa na wananyumba ndio maana huwa wanasema unapotaka kuoa jitahidi uwe makini sana katika kuchunguza kwanza unaweza kuchunguza hata miaka 3 au 4 na sio kujichukulia tu mke au mume matatizo kama haya huwa yanaweza kabisa kuepukika mapema!!!
   
 6. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160


  Dada Haika, that is too harsh!
  Sidhani kama mleta hoja anahusisha matatizo ya yule mke na kabila. Mimi binafsi nimeona matatizo kama hayo kwa watu wa makabila mbali mbali. Kwa ujumla, wanawake wengi huwa hawawapendi sana ndugu wa kiume, wapo baadhi ya wanawake hutumia busara tu ili kuonyesha uvumilivu kuwa wanawajali ndugu wote. Hii haijalishi kabila.

  Mimi nakushauri mtoa hoja, Mume ajaribu kushirikisha ndugu wa mke wake, hasa wazazi, ili kuweza kubadili mtazamo wa huyo mke. Hata viongozi wa dini mara nyingine husaidia.
   
 7. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wakae chn wazungumze
  awe anamshirikisha kwenye mipango yote
  awaite wazee waongee na mke wake ju ya kuwakubali watoto /ndg zako
   
 8. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  Jamani msimlaumu Dada haika,
  jamaa anayetaka ushauri amekosea kutaja kabila la huyo mwanamke, ina maana alikuwa anataka ushauri ambao utashirikisha kabila, Kwamba Uchagga wa huyo my wife wake ndio tatizo
  pili inaonekana huyo ndugu yake anapewa lawama nyingi sana kwa kuoa mchaga, yaani matatizo yote yanasababishwa na Uchagga
  ilikuwa haina sababu kabisa ya Kutaja kabila la huyo mama, Mi si Mchagga lakini inaboa kudiscuss Tabia ama Uamuzi wa mtu kwa kigezo cha kabial lake
   
 9. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160


  OK, Thanks. Msg delivered:
  Nafikiri tunapo-post tuwe makini ili kutoumiza feelings za watu. Mtoa hoja nafikiri ange-edit kidogo ili isiwe kama ilivyo.
   
 10. H

  Haika JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Baada ya msg kuwa delivered,
  ushauri wangu wa ukweli ni kuwa:
  1. mnapoingia kwenye ndoa muwe makini na kuangalia streghts za personalities zenu, na muwe tayari kuishi nazo. Mie sipendi kuona mtu anaishi na mkewe au mumewe huku anaogopa kuleta baadhi ya hoja mezani. Hio si ndoa ni ndoano, na lazima mmoja huyo atakuwa mnyonge na atatia huruma sana hata kwa ndugu na jamaa zake. ajitahidi kumatch up na arguments (hoja) za mkewe, aje na hoja mezani.
  Ndoa za kiafrika wote tunaelewa ni za kiukoo zaidi kuliko mtu mmoja mmoja.
  2. Kwa huyo jamaa yako bila kuwa wazi baba na mama, lazima kuna mambo mengi sana yametokea hapo nyuma, sie wanawake mara nyingi huwa tunaunganisha matukio mengi madogo madogo na kuyatafakari kwa ujumla wake, kuna habari hatuwezi kuijua hapa.
  2. Ajiweke kwa ajili ya mke wake, bila kujidharaulisha, na abainishe wazi majukumu ya kulea ndugu,
  KWA KIFUPI ATAMBUE MAANA YA KUITWA BABA, si sifa wa la cheo ni MAJUKUMU. Awe tayari kwanza kuwa BABA WA NYUMBA YAKE ndio ataweza kuwa msaada wa watu wengine.

  hili ni tatizo kubwa sana kuliko tunavyodhania.
  Personalities za wanaume kwa miaka ya karibuni mimi huwa naona kama wanaanza kukubali kuwaachia wanawake kuprovide security ya familia, hii itatucost, wote wanawake na wanaume.
  Kuna mwalimu wangu alikuwa anasisitiza sana wanafunzi wa kiume wasome sana, wasikubali kupitwa na wasichana, alikuwa naogopa sana kuwa watakuja kudharauliwa baadae, mie kil amara huwa nakumbuka na kuzidi kuona ukweli wa maneno yake mengi kama haya:
  - we mtoto wa kuime usikubali kudharauliwa,
  - usiache familia yako isikutegemee, hakikisha unawatunza
  - mwanaume anatakiwa awe radhi hata kukesha ili kulinda familia yake
  - mtoto wa kiume halii mbele ya mtoto wa kike
  - mwanaume anatakiwe awe jasiri wakati wote
  - jibebeshe jukumu la kutunza familia yako kwa heshima
  - usikubali mwanamke akulishe atakudharau au utajidharau
  - mwanaume huwezi kusamehewa kwa kukosa uelekeo na msimamo wa maisha yako
  nk nk
   
 11. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  ndugu mtoa mada,ungeweza kuomba ushauri bila kutaja kabila coz it has nothing to do with the situation,,,back to the point huyo mume amewahi kukaa na kuongea na mkewe khs hiyo tabia?
   
 12. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  na nyie mmezidi kuoa mijanamke yenye tabia za ajabu ajabu......wanawake wote hawa duniani hapa we unaenda kuoa watu walio na akili za ajabu ajabu.
   
 13. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  solution hapo ni either aendelee kumsikiliza mke wake, kwa sababu ndio aliyemchagua.....vinginenvyo ampe talaka arudi kwao
   
 14. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ajaribu kushauliana na mke kwa kila jambo kabla hajaamua .
  Kwani hapa inaonyesha kuwa mwanamke hajashirikishwa katika uletaji wa hawa ndugu

  Hawa wanaume huwa wanakuwa na dharau, wanaona wao ndio wanahaki zaidi wakati wapo na wake zao.
  Ustaarabu ndio unaomcost, huyu dada hana kosa anaona amedharauliwa kama mke ndani ya nyumaba
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Duh Haika lah!

  Tribaphobia! - right?
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Aachane nae na atafute atakae weza kufata matakwa yake mme.....
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Soma alicho kiandika mleta mada sijui kama ulikiona
  Bado mimi naendelea amtimue tu
   
 18. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimekiona sana kunasentensi ina sema simtaki huyo mtoto kwa kuwa hukunishirikisha sasa kama yeye anajifanya kidume hajadili kwanza na mklewe analeta tu watu anategemea nini?
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mbona mnakuza mambo, Issue ni mke hataki ndugu za mme na limejionyesha wazi wazi baada ya ndugu yake kuja na hakuongea chochote..
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwa ndugu yake mbona hakujadili na bado hakuongea chochote....kifupi jamaa anatakiwa asimamie maamzi yake kama kicho cha familia na akileta msimamo wake wa kuto wataka ndugu za mme amtimue....
   
Loading...