Mke au mume wako anapojenga kwa siri bila wewe kujua tafsiri yake ni kwamba anajiandaa kuishi bila wewe

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,127
Habari wanandoa na wanauchumba.

Hivi unajua kuwa mwenzi wako anapoamua kujenga nyumba au kufanya jambo la kimaendeleo bila wewe kujua hapo anajiandaa kuishi bila wewe?

Hii dunia ina mambo sana. Unaweza kuona watu wakiishi pamoja wakicheka pamoja na kula pamoja ila mmoja au wote wakaingiwa na ibilisi wa ujinga, tamaa na ufedhuli.

Mtu anaamua ajenge kimyakimya. Tena wengine huwaibia wenzi wao (hujiibia wenywewe) na kwenda kujenga nyumba kwao.
Hii roho ni mbaya kuliko ile roho ya kuchepuka.

Kuna jirani yangu mmoja Mchaga hapa mjini Dar es Salaam ana viwanja 9, huku mke anakijua kimoja tu kati ya hivyo viwanja 9.
 
Mimi najaribu kufikiria mazingira wezeshi kufanya hayo bila mmoja kujua

Najua kwa namna yoyote iwe mleta ugali nyumbani ni mume, mke au wote wawili inawezekanaje kufanya jambo mwingine asijue?
Najua panaweza kuwa na pato la ziada ambalo mmoja hajui lakini ugumu utamuwia penye kufanya hilo jambo lake na mwingine akitaka mfanye la familia

Yaani kama mume anajenga kwa siri na wewe mwanamke ukikomaa mjenge ya familia hapo ndio utajua kuna kitu, atabishaje? Akibisha utambana, akikubali jambo lake litafeli

Najaribu ku-imagine mko kwenye ndoa na huwa hamzungumzii kabisa maendeleo ya familia, hapo mtu atajenga kwa siri lakini kama mna plan za pamoja mtu anajengaje?
Au tuseme labda mlishajenga mnayoishi kwahiyo hamzungumzii mambo makubwa tena hali inayompa mtu mwanya wa kujenga kwa siri? Nyie mtakuwa wafu? Hata kama mmeshajenga bado kuna plan zaidi

Maswali yote haya najaribu kuelewa inawezekanaje mmoja akajenga bila mwingine kujua
 
Ndo ivo,hakuna namna.Ila kuna uncle wangu kapata nyumba ya buree...kutokana na mjeshi kumficha mkewe Mali zake na kumthamini rafiki yake.Kafa na kende zake mke hajui kama mume alikuwa na jumba huko.
 
Habari wanandoa na wanauchumba.

Hivi unajua kuwa mwenzi wako anapoamua kujenga nyumba au kufanya jambo la kimaendeleo bila wewe kujua hapo anajiandaa kuishi bila wewe?

Hii dunia ina mambo sana. Unaweza kuona watu wakiishi pamoja wakicheka pamoja na kula pamoja ila mmoja au wote wakaingiwa na ibilisi wa ujinga, tamaa na ufedhuli.

Mtu anaamua ajenge kimyakimya. Tena wengine huwaibia wenzi wao (hujiibia wenywewe) na kwenda kujenga nyumba kwao.
Hii roho ni mbaya kuliko ile roho ya kuchepuka.

Kuna jirani yangu mmoja Mchaga hapa mjini Dar es Salaam ana viwanja 9, huku mke anakijua kimoja tu kati ya hivyo viwanja 9.
Kwa Wachaga sio jambo la ajabu. Ni criminals wanaojuana kuwa wapo kwa kuviziana. Aki disclose tu, amekwisha

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom