Namna gani unaweza mdhalilisha mpenzio au mwenza wako bila kujua

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
1. Kutumia lugha asiyoijua
Ni hadhi mtu kutumia lugha fulani kuonyesha wewe ni msomi, mjuaji au umetembea, lakini ni mbaya kwa mpenzio ambaye hana maarifa hayo, uona kama umedharau na kumkejeli.

Tumia lugha ya kueleweka ili uonyeshe wewe na yeye ni wamoja na unakusudi zuri kwake kwa unachokizungumza.

2. Kumuomba kitu kilicho nje ya uwezo wake.
Unampomjua mwenzio hali yake, msimamo wake, familia yake, upungufu wake na imani yake, lakini unaomba kitu hicho hicho, ni kuonyesha kutomjali, kumdhalilisha, kumfukuza, kutokuwa muelewa, kumlazimisha afanye asichokusudia kwa wakati huo na kutaka kinyume na yeye na haya yapo hata faragha.

Hii ufanya mtu akuone wewe siyo muelewa, siyo mstaarabu, mwenye tamaa, pasua kichwa na mtu mwenye papara.

3. Kuacha kuongozana naye mnapotembea pamoja.
Hii uonyesha hauko tayari naye kimaisha, siyo hadhi yako, anakulazimisha kuwa naye(ni vile tu nje ya boksi), huwezi kumtetea, uamuamini, hawezi kuambia la maana na huwezi kumsifia maana kwako ni kituko.
Ajabu ni mpenzio au mwenza wako lakini mkiongozana ni kama wapita njia, wewe kule yeye huko nyuma kama mnakimbizana kumbe ni safari moja, safari moja ila kila mtu aje na usafiri wake au kwa njia yake.

4. Kushindwa kumtambulisha unapokuwa naye kwa rafikizo au nduguzo.

Uonyesha huna uhakika naye, una mtu mwingine zaidi yake, bado hujaridhika naye, unaogopa kuchekwa hivyo yeye siyo mzuri kwako, bado siyo mwenza afaaye kwako, ni wa kupita tu kwake, ndugu au rafiki hawampendi ama washamzungumzia vibaya.
Hii ni ya kuogopa sana kuwa na mtu asiyeweza kukuheshimisha.

5. Kumsifia mwingine mbele yake.
Tabia hii uonyesha yeye siyo kitu kwako, umuogopi wala kumheshimu, unaweza fanya lolote baya bila kujali yeye kwako, uonyesha una mtaka huyo mwingine na pia uonyesha hana faida kwako.

Kumlinganisha uliyenaye kwa kumuambia kwa mfano wa mtu ni tusi na kuonyesha kwako hana thamani.

Yule dada anamsambwanda atakuwa ni mtamu/ yule mwanaume ni mzuri anavutia/ningekuwa na mke/mume kama yule tungefika mbali sana. Ni dharau hii hata kama mpenzio/mwenza anakasoro tumia lugha na mifano sahihi ya kumjenga.
6. Kumpa kipaumbele mtu mwingine mahali mlipo.

Ni mbaya kuwa na mpenzi au mwenza, alafu ukamruka na kumpa nafasi mwingine, ukamuacha shida yake na kumsaidia mwingine shida zake, akaomba ukamnyima na kumpa mwingine aliyekuomba.

Anakuita unamuacha na kwenda kwa mwingine, anahitaji muda wako unamueleza uko bize alafu anakuona kwa mwingine una mpa muda wako bila shaka ya ubize usemao.
Kuwa hodari wa kulinda wengine ile yeye huwezi kumlinda.

7. Kumpa kitu chenye kumshusha hadhi au heshima yake.
Kila mtu upewa kitu na kutendewa jambo kwa nafasi yake, unaponunua zawadi isiyomfaa ni kumtusi, unapompa kitu kisicho jinsia yake ni kumtusi, unampomsifia ujinga wake kwa watu ni kumtusi, mcha Mungu unataka aende kwa ushirikina, kutenda ngono asivyopenda nk.

8. Kuwa naye tu kwenye dhiki ila kwenye raha unakula na wengine.

Kuna watu ni matajiri kwa marafiki na watu wa nje na mahusiano na ndoa zao, ila ndani ya ndoa zao na mahusiano yao ni watu wa dhiki mpaka makalioni.

Mwanamke/mwanaume ana chukua kwa mume au mke/mpenzi na kumpa mwingine.

9. Kumtusi na kumgombeza mbele za watu.
Kumfanya kama mtoto mdogo mbele ya watu, kukosa stara naye, kushindwa kuwa na subira naye pale anapokosea, kushindwa kuthibiti jazba zako, kisa ni maskini /hana kipato/ hana kazi/ unamtenda utakavyo, kumtenda kisa jinsia yake nk.

10. Kutokumjali mahitaji na hisia zake.
Kumuachisha kazi, kumtenga, kutomjali dhiki zake na afya yake, kumnyima haki ya tendo, kutompa mavazi, chakula na kutomlinda kimakazi na ndoto zake.

Kuna mahusiano watu wamepewa midomo na nguvu za vitisho na ukatili ila hata kuhudumia hawajali, ila anang'ang'ania aitwe mwenza/mpenzi.

Hivyo, ni vyema ujitazame uone ni wapi unaweza fanya na kuonyesha kumdharau uliyenaye au unayemtarajia
Imeandikwa na Mtunzi wa Ujumbe kwa Mpenzi, MMMUHUMBA.
 
Wajumbe wa Tafuta hela/mpe hela watapita kimya, but hii ni shule.
wapumbavu hawaoni.
Sana ndugu Surya, napofanya ushauri na elimu huwa nakutana na watu wanakuelezea walivyotoa mali na pesa hadi kuna wakati nasema " dah kuna watu wanapewa ndoto za watu lakini bado hawashikiki hisia zao".
Shida watu wengine wanashindwa kutambua kuwa kuna mahusiano ya aina mbili:
1. Ya hisia
2. Ya kimahitaji
 
Sana ndugu Surya, napofanya ushauri na elimu huwa nakutana na watu wanakuelezea walivyotoa mali na pesa hadi kuna wakati nasema " dah kuna watu wanapewa ndoto za watu lakini bado hawashikiki hisia zao".
Shida watu wengine wanashindwa kutambua kuwa kuna mahusiano ya aina mbili:
1. Ya hisia
2. Ya kimahitaji
Mahusiano ya kihisia na kimahitaji nielekeze hapo mkuu
 
Jee nikiamua kukaa single na kula pesa zangu ntapata tatizo gani maana mapenzi kwa hapa TZ ni mradi wa upigaji
 
ahsante sana mpendwa na ndugu katika jf, kuna vitu ukitendewa na ukajieleza kuwa unanyanyaswa na kudhalilishwa ukataja sababu zako inaonekana unatafuta ubaya mwenyewe, chochote ukitendewa ukajisikia dhalili, huo ni udhalilishaji.
 
ahsante sana mpendwa na ndugu katika jf, kuna vitu ukitendewa na ukajieleza kuwa unanyanyaswa na kudhalilishwa ukataja sababu zako inaonekana unatafuta ubaya mwenyewe, chochote ukitendewa ukajisikia dhalili, huo ni udhalilishaji.
Mahusiano ya kihisia na kimahitaji nielekeze hapo mkuu
1. Kihisia - ni kuanzisha mahusiano na kudumu nae kwa kuwa umeguswa naye kifikra kuwa naye.
2. Kimahitaji- ni kuanzisha mahusiano na kudumu nae kwasababu unakitu unakipata kwake cha kuziba pungufu lako kama kuanzisha upate fedha, mali, kusomeshwa, kula nk
 
Back
Top Bottom