Mke anataka watoto zaidi

Elia

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
3,425
567
Ana watoto wa tatu mmoja std 3 wapili std1 watatu kindergarten. Anataka watoto zaidi kwani anadai haoni sababu ya kuwa na watoto wachache. Jamaa anasema mwanzoni alidhani ni utani lakini sasa hivi hii topic imekuwa too much. Kaniomba msaada ili ndoa yao iendelee kuwa na amani, kwani ana mpenda sana mke wake. Mimi nilipongea naye kiundani sana, lakini Nimeileta huku ili mnipe mawazo yenu.
 
Zaeni muongezeke ndo anachotekeleza huyo mama je maisha anayamudu??

Wana uwezo kawaida kwani bwana ni mfanyakazi selikarini na mama anasimamia miradi yao! watoto wote wanasoma st. mary's
 
Basi wazae tu hao 13 hadi kizazi kiishe uwezo si upo bana shida iko wapi?
 
Kama wana uwezo wa kuwalea vizuri kwa kuwapa upendo na mahitaji muhimu aongeze,lakini pia huyo baba nae awe ameridhia kutoka moyoni ili isiwe tuamekubali kumridhisha mke wake.
 
kusoma st marys si tatizo,hao watatu wenyewe mnapata muda mzuri wa kuwa nao,kujua matatizo yao au mnajaza dunia tu :rain:
 
Thanks, shosti; hata mimi nadhani watoto wanahitaji ukaribu na wazazi wao sio uwepo wa mahitaji yao tu.
 
Naombeni faida na hasara za huyu jamaa kukubali au kukataa kuwa na watoto wengi, swala la uchumi tuliondoe kwani sio tatizo
 
Ana watoto wa tatu mmoja std 3 wapili std1 watatu kindergarten.
Kwanza ninaweza sema huyo jamaa nanafanya kazi gan? Na je wanaumri gan? Alafu mbona hawa watoto watatu ni weng sana kulingana na hal ya maisha ya sasa hv alafu ukiangalia watoto bado wadogo. Na bado wanasoma tena std na kindagaten mbona mwambie akiongeza watoto mwambie hato weza kuwalea kutokana na maisha ya sasa cnamaana atashndwa la hasha ila cjajua kipato cha kwake na mkewe. Alafu vp huyo mkewe ni kabila gan? Na kasoma kwel? Sawa je anafanya kaz gan? Kama hal ya maisha ni nzuri kwao waendelee kuzaa hata watoto 30
 
Ana watoto wa tatu mmoja std 3 wapili std1 watatu kindergarten. Anataka watoto zaidi kwani anadai haoni sababu ya kuwa na watoto wachache. Jamaa anasema mwanzoni alidhani ni utani lakini sasa hivi hii topic imekuwa too much. Kaniomba msaada ili ndoa yao iendelee kuwa na amani, kwani ana mpenda sana mke wake. Mimi nilipongea naye kiundani sana, lakini Nimeileta huku ili mnipe mawazo yenu.
ndugu umeleta sredi nzuri kwani hata mimi ninasuguana na mchumba wangu kwa hili.
Mimi nataman mungu atupe watoto wanne au watano,jamaa anasema anataka wawili tu baada ya kumvuta sana akakubali watutu na siyo zaidi.Balaa ni pale mume anapotaka idadi kubwa kuliko mkewe.
 
Kwanza ninaweza sema huyo jamaa nanafanya kazi gan? Na je wanaumri gan? Alafu mbona hawa watoto watatu ni weng sana kulingana na hal ya maisha ya sasa hv alafu ukiangalia watoto bado wadogo. Na bado wanasoma tena std na kindagaten mbona mwambie akiongeza watoto mwambie hato weza kuwalea kutokana na maisha ya sasa cnamaana atashndwa la hasha ila cjajua kipato cha kwake na mkewe. Alafu vp huyo mkewe ni kabila gan? Na kasoma kwel? Sawa je anafanya kaz gan? Kama hal ya maisha ni nzuri kwao waendelee kuzaa hata watoto 30
Ahsante Murefu Hapo kwenye bluu, Ni 'masanja', amesoma, accountant also managing family business
 
ndugu umeleta sredi nzuri kwani hata mimi ninasuguana na mchumba wangu kwa hili.
Mimi nataman mungu atupe watoto wanne au watano,jamaa anasema anataka wawili tu baada ya kumvuta sana akakubali watutu na siyo zaidi.Balaa ni pale mume anapotaka idadi kubwa kuliko mkewe.

Hapo amri ubabe/amri hutumika
 
sana tu na kama ukikataa atakwambia subiri miaka miwili ntamtambulisha mtoto hapa home na nakuomba umleee kama wakwako.

So kwasababu huwezi lea wa mwenzio itakubidi ukubali au sio?
 
Ushauri wa watu wa nje unaweza kuwasaidia lakini baada ya yote wao ndio wahusika wakuu. La kufanya ni kwa wao wawili kujadiliana mpaka kufikia uamuzi.
 
mmmhhh si kila asemalo mke ukubaliane hata kama unampenda sana....maisha yana surprises zake,mmoja aweza shindwa kwa sababu tofauti kuendelea ku-manage familia au wakati mwingine wote wawili....nafikiri kwa hali ilivyo sasa,watoto watatu wanaweza!
 
asante michelle, maisha yana suprises zake, tatizo letu upendo tunautafsiri kwa maana tofauti!
 
Aisee mi nna wawili, na huyu mama akilogwa akanambia tutafute watatu anaweza chezea talaka.

Hao wawili tu kijasho kinanitoka seuze watatu?
 
kama mbegu bado zipo waambie waongeze mbona kwetu tumezaliwa 11 na mama mmoja sembuse hao watatu anaogopa! mwambie apige mashine afetue watoto kama tofali bila kusimama
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom