Mke amuua mume kisa wivu wa kimapenzi

Haya ya kutuchoma moto aliyeyaanzisha ni Yule Dada wa kichaga !?? Daaah sijui alijifunzia wapi!!!
 
Pole sana Dada utoto unakusumbua ukikua utaona
Nikupe pole wewe unayedhani unanijua...mimi wewe nakuzaa huku nakomenti jf mtoto upo? Mpaka kufikia umri huu nimekutana na mengi ambayo wewe wala huyajui. Nina uhakika siwezi kufanya kama aliyofanya huyu fundi mwenzangu kwa sababu ya wivu tu wa mapenzi...labda kuwe na kitu kingine

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Dawa ni moja ukirudi home kama maelewano sio mazuri unatakiwa kufanya msako wa vidumu ndani na nje bila kusahau kwenye banda ka bata na mbwa !!! Ukijiridhisha ndio ulale
 
Mwalimu wa Sekondari ya New Kiomboi mkoani Singida, Simon Roman (33) amefariki dunia baada ya kuchomwa moto na mkewe sababu ikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo lilitokea Desemba 27, 2021 jioni baada ya mume kurudi kutoka matembezi huku mkewe akitaka kujua kuhusu uhusiano wa mumewe na mmoja wa wanawake katika eneo hilo.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa Singida, Stella Mutabihirwa amemtaja mtuhumiwa mtuhumiwa wa mauaji ambaye ni fundi cherehani naye amelazwa hospitali ya mkoa wa Singida akipatia matibabu kutokana na majeraha ya moto aliyoyapata.

Mbali na mtuhumiwa, watoto wao Clara Anthony na Wisley Anthony wamelazwa hospitalini kwa majeraha ya moto huku Apolinary Simon (18) ambaye ni mdogo wa marehemu inadaiwa hali mbaya baada ya kuungua zaidi usoni.

Katika taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari, Kamanda Mutabihirwa amesema chanzo cha ugomvi ni mwanamke huyo kumtuhumu mumewe (marehemu) kwamba alikuwa na uhusiana na mwanamke mwingine jambo lililozua ugomvi kwa wawili hao.

Majibizano yalipoendelea, mwanamke alikwenda kuchukua maji ya moto yaliyochemshwa kwa ajili ya kuoga akamwagia mumewe wakiwa sebuleni na kabla hajajua la kufanya alimwagia tena mafuta ya petroli kisha akawasha moto wa kiberiti,” anasema Kamanda Mutabihirwa
Cc.millardayo.com
Unyama kabisa
 
Back
Top Bottom