Mkataba wa IGA Ulitengenezwa Kuwa na Vipengele Hasi kwa Tanzania, na Viongozi Wetu Walijua na Kushiriki Uhujumu Huo

Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
7,660
8,807
Sote tuanelewa kwamba nchi yetu Rais ni kila kitu kwetu, hahojiwi na mbaya zaidi huwezi kumshtaki mahakama yoyote nchini, akiwa madarakani au baada ya kuachia madaraka.

Wananchi wa nchi hii wamezoea, kwamba hawawezi kumwajibisha kiongozi huyo kwa njia yoyote ile; na Bunge ambalo sheria inaruhusu kumwajibisha jinsi wawakilishi wa Bunge hilo wanavyopatikana kwa fadhira za mtu huyo huyo mmoja (Rais), halina uwezo wa kumwajibisha mtu huyu.

Bila shaka yoyote, Rais wetu Samia yote haya aliyajua, na hasa baada ya kuona ni namna gani mtangulizi wake alivyokanyaga kila kitu kutimiza matakwa yake.
Kwa hiyo Samia hakuwa na hana hofu yoyote juu ya kufanya aliyonuia kuyafanya siku nyingi, kama angepata fursa hiyo ya kuyafanya

Kwa bahati nzuri kwake, na mbaya kwetu wengine fursa hiyo ikamwangukia bila ya mategemeo yoyote

Sasa anatimiza alichonuia toka siku nyingi.
Hapa nataka kuonyesha mambo yaliyofanyika, kwa maksudi, tokea mwanzo alipochukua uongozi wa nchi ili kufanikisha lengo lake la kuiumiza nchi yetu. Nitaorodhesha mambo aliyoyafanya au kutoyafanya ili kufanikisha IGA hii iliyoletwa kwetu ifanikiwe. Kumbuka wakati wote, yeye anajua hakuna lolote wananchi wanaloweza kufanya kumzuia au kumuwajibisha sasa au baadae.

1. Uteuzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika eneo husika, na kuwaondoa viongozi ambao hawakukidhi mahitaji yake. Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara, Wakurugenzi TPA na kwingineko. Sitataja majina, kwani wanafahamika.
Hawa ni watu maalum walioteuliwa kuhakikisha lengo la IGA (mbovu) linafanikiwa.

2. Kufanya viini macho ili kupoteza lengo.
Paliwahi kuwepo mjadala wa kufufua mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, na yeye Rais aliwahi kueleza kuwa kuna timu ya majadiliano na waChina. Hili halikufika mbali, kabla ya kugeukia kwenye ujenzi wa hatua za mwanzo sisi wenyewe.

Wakati haya yakiendelea, imebainika sasa kwamba DPWorld tayari walikuwa kwenye kibarua cha kutengeneza IGA na wataalam wetu hapa ambao haijulikani walipatikana kwa mpango upi kushughulikia kazi hiyo. Bila shaka ni sahihi pia kusema kuwa ni watu walioaminiwa kutengeneza kitu alichokitaka mteuzi wao kwenye nafasi hiyo.

3. TICTS - abaki/asibaki? moja ya viini macho kuzuga watu, bila shaka hata wao TICTS hawakujua hatma yao itakuwa vipi. Wakati wote huu wa sintofahamu, DP World na wataalam wetu wapo kazini wakisuka IGA ya kutukomesha sisi.
4. Mara BUUUUU! DP World anaingia kwa kishindo kikubwa. Sasa ndipo watu wanaanza kuunganisha doti
Bendera yetu na picha ya Rais wetu juu ya jengo refu kabisa duniani; mara fununu za viongozi kwenda kwenye EXPO Dubai kimya kimya na Rais kukaa huko kwa siri kubwa, kumbe anatia saini mkataba wa kutuuza!

5. Mkataba unavujishwa? Juhudi kubwa zinaanza kufukia mahandaki. Hapana, huo siyo Mkataba, hayo ni "Makubaliano tu, ikiambatana na upotoshaji mwingi mwingine, toka kwa waziri na mtu mwingine aliyeaminiwa sana kusimamia kujua kilichomo ndani ya Mkataba/Makubaliano" hayo. Mtaalam wa sheria mbobezi (tunaambiwa), Hamza Johari ndiye mkuu wa timu. Watu wanajiuliza, na Mwanasheria mkuu wa Serikali alishiriki vipi hadi kufika kwenye hatua hii?
Mwanasheria Mkuu wa Serikali hasemi kitu, bali kukanusha tu kwamba "Bandari haijauzwa". Hakuna anayejua kiwango cha ushiriki wake kwenye mkataba huo, na kama yeye, kwa nafasi yake anakubaliana na yaliyomo kwenye mkataba. Sijasikia akisema lolote juu ya hayo.

6. Taratibu na Hatua sahihi za kuingia mikataba kama huu (IGA) - Je, sisi kama taifa tunao utaratibu wowote tuliojiwekea wa kuingia kwenye mikataba kama hii? Huu siyo mkataba wa kwanza Tanzania iliouingia, je hiyo mingine kulifanyika mambo gani ambayo yamezoeleka kufanywa, lakini safari hii ikawa ni tofauti?

Hili ni swali lililo wazi, kama kuna utaratibu maalum, je ulifuatwa, hata kwa kiasi fulani tu?
jambo la kwanza linaloniingia akilini ni "Vikao vya Baraza la Mawaziri". Kwa mtizamo wangu, jambo kubwa kama hili haliwezi kufanyika bila ya uwepo wa angalao kikao cha Mawaziri kulijadili..
Vikao hivi vya Baraza la Mawaziri siku hizi vimekuwa kama ni siri kubwa sana, hata kule kutaja tu kulikuwepo na kikao siku hizi ni nadra sana, hata bila ya kutaja yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho.
Kwa hiyo hili ni swali tu kuuliza kama kulikuwa na kikao cha kujadili, au kujulishwa tu kwamba kuna mpango wa ujio wa DP World na hatua zilizokuwa zikifanyika kuwakaribisha hapa.
Kama Mawaziri nao hawakuwa na habari, hilo litakuwa jambo la kushangaza sana linaloongeza uzito katika hoja za andiko hili.
7. Ushirikishwaji wa Bunge katika "kuridhia Mkataba" Bila shaka yoyote palikuwepo na mpango kabambe wa kulishirikisha Bunge katika kufanya hujuma hizi, siyo kwa nia njema bali kwa nia ovu..
a) Kundi la wabunge lililopelekwa Dubai, ni utaratibu upi uliotumika kuwachagua hao waliokwenda? Wanazo sifa maalum ambazo zingewawezesha kutambua mambo ambayo hayana manufaa kwetu?
b) Waliandaliwa na kupewa semina wajiandae kuhusu maswala nyeti katika kazi wanayokwenda kuifanya huko walikokwenda? Walipewa Mkataba wausome wajue yaliyomo kabla hawajaondoka hapa?
Hawa wabunge ni akina nani hasa?

Kama maswali yote haya hayana majibu, maana yake ni kwamba hii ilikuwa ni mbinu tu, iliyotegeshwa kuhalalisha maovu juu ya nchi yetu, maovu waliyoyajua walioandaa mkataba huo na washirika wao wote.
c) Bungeni wakati wa kikao cha Bunge, ni wabunge wapi waliopewa nafasi ya kujadili yaliyomo kwenye mkataba, na ni nani aliyetoa nafasi hiyo kwa wabunge hao maalum? Hawa wabunge walijua kilichokuwemo kwenye huo Mkataba? Mbona hta mmoja wao hakujitokeza na anagalao kutaja tu hata kifungu kimoja alichokuwa nacho mashaka? Hawa wote waliandaliwa kwa maksudi kwa ushirikiano na uongozi wa Bunge?
d) Ushirikiwa wananchi, wanapewa masaa 24 kuleta maoni yao. Maana ya hili ni kwamba hapakutakiwa kuwepo na mchango wa wananchi ili lengo la kuhujumu nchi litekelezwe.

DPWorld wanao uzoefu mkubwa sana katika maswala haya ya Mikataba, kwa sababu kila sehemu walikokwenda wamekutana na chngamoto chungu nzima zilizowakabili.
Wamekuja hapa kwetu, wakamkuta mkuu wetu aliye tayari kabisa kuwapokea kwa masharti waliyoyapenda wao. Mkuu wetu hana uzoefu wowote, na isitoshe hana uchungu mkubwa kuhusu nchi anayoiongoza yeye, ila anayo madaraka ya kufanya lolote analotaka bila kuwajibishwa na yeyote.

Hapa ndipo tulipofikia sasa hivi.

Ingekuwa ni nchi nyingine, Mkataba huu usingemwacha huyu mkuu abaki salama, tena akiendelea kwenye madaraka yake kana kwamba hakuna lolote lililofanyika.
Lakini hii ni Tanzania. Yeye kishasema "Ameziba masikio", wenye kupiga kelele wapige kelele hadi wachoke wenyewe; lakini DP World hakuna wa kumzuia kuja hapa.

SAWA.
Sasa tumebaki na moja tu tunaloweza kulitegemea kuondokana na hujuma hii juu ya nchi yetu.
Je, tunaweza kumpata kichaa mwingine (bila ya baadhi ya mambo ya aliyetangulia mbele ya safari) atuondolee uchafu huu ndani ya nchi yetu? (Bila kujali hasara tutakayoingia kwa kuvunja mkataba (kwani kuendelea na mkataba wa aina hii ni hasara kubwa zaidi ya kulipa hiyo fidia tutakayodaiwa).
Na kwa kuwa ni 'kichaa', bila shaka baadhi ya hawa wahujumu watachukuliwa hatua bila ya kuwaonea aibu.

IGA baina ya Tanzania na Dubai ni hujuma iliyo andaliwa maksudi kuihujumu Tanzania.

N.B. Sikutegemea na wala siyo kawaida yangu kuandika gazeti, lakini leo acha iwe hivyo, kwani hakuna namna.

Samahani kwa makosa ya kiuandishi kama yamo kwenye andiko hili..
 
Itafikia kipindi hawa viongozi wakistaafu wataanza kutafutwa mmoja mmoja mitaani na wananchi wenye hasira za kuibiwa maliasili zao.
 
Chongolo amesema DPW lazima wapewe bandari akasisitiza ukiona mpinzani wako anakusifia basi achana na ilo jambo na ukiona mpinzani anakupinga basi kanyagia hapo hapo usonge mbele kwa kasi.

Hasa mtu mwenye vyeti vya kuungaunga vya open university anajua hata mikataba ni nini? Yeye anajua kunyoa vipara tu na kuvaa mashati yake ya kijani basi
 
Mimi nins jibu kufuatama hiyo heading , kwamba viongozi walisaini na vifungu Hadi Kwa sababu huko ndiko wanapojihakikishia mlo wao . Ili mshindwe kuvuja nkataba .
 
Samia ndie architect wa ule uovu, ametusaliti watanganyika, na kwa kuonesha nia yake ovu kwetu, na dhamira yake, anasema bila aibu ametuzibia masikio, kwamba licha ya ubaya aliotufanyia, hataki kusikiliza malalamiko yetu kwake.

Huyu ndie kiongozi wetu, kiongozi anayesikiliza ndugu zake wa uarabuni zaidi yetu, anayewajali ndugu zake uarabuni zaidi yetu, anayetumia rasilimali za taifa ketu bila aibu kwa manufaa ya ndugu zake wa uarabuni.

Halafu licha ya huu unyama wake wa dhahiri dhidi yetu, bado kuna wajinga wanamtetea, wajinga wanaoamini wakitumia kigezo cha dini, basi watatufunga wengine mdomo, wamefeli, na wataendelea kufeli mpaka mwisho, Samia ni shetani msaliti asiye na aibu.
 
DPWorld Wamekuja hapa kwetu, wakamkuta mkuu wetu aliye tayari kabisa kuwapokea kwa masharti waliyoyapenda wao.
Ni kweli Mama kafungua nchi kuwapokea wawejezaji ila masharti tunaweka sisi!, hivyo sio sahihi kusema masherti wanaweka wao!. Ile IGA ni barua tuu ya posa, tumeipeleka kwenye kikao cha familia (Bungeni), ili kufanya ushirikishaji wa familia nzima kuridhia tuipokee barua hiyo ya posa!. Bunge letu kuridhia ni kuridhia posa ipokelewe, na sasa ndio tunapanga mahari (HGA), anayepanga mahari ni mwenye binti!. Mahari tunapanga sisi, tunawapa, tuna negotiates, tukifikia maelewano, tunawaruhusu kuleta mahari, HGA, ikipokelewa, tunawakabidhi binti!. Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA?
Mkuu wetu hana uzoefu wowote,
Hii sio kweli!, Mama ana uzoefu wote ila yeye sio mwanasheria, hivyo anawategemea wasaidizi wake wa kisheria, ambao it has happened, baadhi yao ni vilaza na stupid kabisa kama alivyosema mwenyewe. Hili hata sisi tumelisema IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria vilaza wa Ajabu. Je, Bunge letu na Serikali navyo ni vya Ajabu?
na isitoshe hana uchungu mkubwa kuhusu nchi anayoiongoza yeye,
Hapa sasa ni kumuonea bure, ameisha onyesha kwa dhamira, kauli na matendo, ana uchungu mkubwa na mapenzi ya dhati kwa nchi yake. Yeye ndiye mzalendo numero uno!.
Mifano hai ni hii
ila anayo madaraka ya kufanya lolote analotaka bila kuwajibishwa na yeyote.
Yes, hili ni kweli na madaraka hayo hakujipa yeye, ameyakuta yapo kwenye katiba yetu, hivyo aliyempa madaraka na mamlaka hayo ni katiba, na wenye katiba ni sisi wananchi, hivyo madaraka na mamlaka hayo tumempa sisi wenyewe, sasa tunalalamika nini?!.

Kwenye hili la DPW na Bandari zetu, nimewahi kuuliza DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?

Nikashauri Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

Naendelea kusisitiza wito wangu huu Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

P
 
Ni kweli Mama kafungua nchi kuwapokea wawejezaji ila masharti tunaweka sisi!, hivyo sio sahihi kusema masherti wanaweka wao!.

P
Ndugu Paskali Mayalla , elimu yako ya sheria haijakusaidia hata kujua kupitia wording ya Mkataba wa Bandari kwa mkataba huo haujaandaliwa na Tanzania bali Dubai?!!

Halafu uliona wapi Mpangaji ( Tenant) ndiye uandaa Mkataba ( Lease) na Mwenye Nyumba ( Landlord) yeye ni kuanguka sahihi tu!

Kwa hili la Mkataba wa Bandari Mama na Brokers wenzake walijitoa ufahamu kabisa na hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuwaelewa kabisa!

Tundu Lissu yuko sawa 100% dhidi ya Mama na Brokers Wenzake!

Tusubiri Judgement from the High Court on 7/8.
Uzuri ni kwamba Judges on disposing that case, the have to write into details na kwa Legal Brains tutajua tu kwamba hii ni pumba au mchele!
Let's wait and see!
 
Mkuu Fuma, Fumadilu Kalimanzila , naomba kukiri udhaifu, ni kweli LL.B yangu haijanisaidia kwenye hili la kujua ile IGA imeandaliwa na nani, kwenye mikataba ya wenzetu ni lazima uone majina ya whoever alie draft.

maadam mwanzo nimekiri udhaifu, naomba kukiri udhaifu

Huku sasa ni kuwatukana Watanzania matusi ya reja reja!. Serikali yote ya Tanzania wanamwelewa, ina maana hawana akili timamu?.
Bunge letu Tukufu la JMT limemwelewa, limeunga mkono, limeridhia!, ina maana Bunge letu lote hawana akili timamu?.

Chama tawala CCM, kimemwelewa na kinamuunga mkono!, ina maana CCM hawana akili timamu?.

Wananchi wa kawaida wa JMT, mamia kwa ma elfu, and probably mamilioni, wanamwelewa!, ina maana hawana akili timamu?.

Duh...!

Naunga mkono hoja, let's wait and see!.

Nashukuru umenielewa japo umefanya comouflage fulani hivi!

Unasema wewe umezoe kuona aliye draft mkataba anaandika Jina lake!!!

Hayo ndo madhara ya Elimu ya kuunga unga Paskali Mayalla!

For the best legal brains, we don't define things but we interprete things!

Wewe ni mwanasheria wa definitions! na pengine If I'm not mistaken hujawahi kushinda kesi yoyote High Court!

Naweza kukutumia mojawapo ya case zangu nilizoshinda High Court na High Court Judge anasema ," As Mr. Fumadilu Kalimanzila argued correctly.......".
 
Kwenye mikataba yote kuna eneo la drown by...
Hayo ndo madhara ya Elimu ya kuunga unga Paskali Mayalla!
Kwenye hili la elimu ya kuunga unga ni kweli, mimi ni wale wa zamani 60s, enzi zetu LL.B inatolewa UDSM pekee!, chuo kilikuwa kina enrols only 60 students top creams, darasa letu Ilboru, tukachukua nafasi 10 tukiwa ndio top in Tanzania, mimi sikufanikiwa kupenya ndio nikaenda journalism, nikaunga unga mpaka nikapata LL.B
For the best legal brains, we don't define things but we interprete things!
Sithubutu kujiita the best legal brain, kwasababu sijaonyesha popote u best wangu ila....
Wewe ni mwanasheria wa definitions! na pengine If I'm not mistaken hujawahi kushinda kesi yoyote High Court!
No sio sijawahi kushinda kesi yoyote high court, bali sijawahi kupanda Mahakama kwa kesi yoyote kwasababu I don't practice!
Naweza kukutumia mojawapo ya case zangu nilizoshinda High Court na High Court Judge anasema ," As Mr. Fumadilu Kalimanzila argued correctly.......".
Asante sana for info, na leo ndio nimejua kumbe Fuma ni verified name na ni wakili!.
Nice to know you.
P
 
Mimi nins jibu kufuatama hiyo heading , kwamba viongozi walisaini na vifungu Hadi Kwa sababu huko ndiko wanapojihakikishia mlo wao . Ili mshindwe kuvuja nkataba .
Huu mkataba jinsi ulivyo, sioni ni jinsi gani utashindwa kuvunjwa. Ni heri ya kuingia gharama kubwa, hata ya watu kupoteza maisha, lakini wengine wawe huru.
Mkataba huu siyo wa kurekebisha vifungu, ni wa kuvunja moja kwa moja.
 
Sote tuanelewa kwamba nchi yetu Rais ni kila kitu kwetu, hahojiwi na mbaya zaidi huwezi kumshtaki mahakama yoyote nchini, akiwa madarakani au baada ya kuachia madaraka.

Wananchi wa nchi hii wamezoea, kwamba hawawezi kumwajibisha kiongozi huyo kwa njia yoyote ile; na Bunge ambalo sheria inaruhusu kumwajibisha jinsi wawakilishi wa Bunge hilo wanavyopatikana kwa fadhira za mtu huyo huyo mmoja (Rais), halina uwezo wa kumwajibisha mtu huyu.

Bila shaka yoyote, Rais wetu Samia yote haya aliyajua, na hasa baada ya kuona ni namna gani mtangulizi wake alivyokanyaga kila kitu kutimiza matakwa yake.
Kwa hiyo Samia hakuwa na hana hofu yoyote juu ya kufanya aliyonuia kuyafanya siku nyingi, kama angepata fursa hiyo ya kuyafanya

Kwa bahati nzuri kwake, na mbaya kwetu wengine fursa hiyo ikamwangukia bila ya mategemeo yoyote

Sasa anatimiza alichonuia toka siku nyingi.
Hapa nataka kuonyesha mambo yaliyofanyika, kwa maksudi, tokea mwanzo alipochukua uongozi wa nchi ili kufanikisha lengo lake la kuiumiza nchi yetu. Nitaorodhesha mambo aliyoyafanya au kutoyafanya ili kufanikisha IGA hii iliyoletwa kwetu ifanikiwe. Kumbuka wakati wote, yeye anajua hakuna lolote wananchi wanaloweza kufanya kumzuia au kumuwajibisha sasa au baadae.

1. Uteuzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika eneo husika, na kuwaondoa viongozi ambao hawakukidhi mahitaji yake. Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara, Wakurugenzi TPA na kwingineko. Sitataja majina, kwani wanafahamika.
Hawa ni watu maalum walioteuliwa kuhakikisha lengo la IGA (mbovu) linafanikiwa.

2. Kufanya viini macho ili kupoteza lengo.
Paliwahi kuwepo mjadala wa kufufua mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, na yeye Rais aliwahi kueleza kuwa kuna timu ya majadiliano na waChina. Hili halikufika mbali, kabla ya kugeukia kwenye ujenzi wa hatua za mwanzo sisi wenyewe.

Wakati haya yakiendelea, imebainika sasa kwamba DPWorld tayari walikuwa kwenye kibarua cha kutengeneza IGA na wataalam wetu hapa ambao haijulikani walipatikana kwa mpango upi kushughulikia kazi hiyo. Bila shaka ni sahihi pia kusema kuwa ni watu walioaminiwa kutengeneza kitu alichokitaka mteuzi wao kwenye nafasi hiyo.

3. TICTS - abaki/asibaki? moja ya viini macho kuzuga watu, bila shaka hata wao TICTS hawakujua hatma yao itakuwa vipi. Wakati wote huu wa sintofahamu, DP World na wataalam wetu wapo kazini wakisuka IGA ya kutukomesha sisi.
4. Mara BUUUUU! DP World anaingia kwa kishindo kikubwa. Sasa ndipo watu wanaanza kuunganisha doti
Bendera yetu na picha ya Rais wetu juu ya jengo refu kabisa duniani; mara fununu za viongozi kwenda kwenye EXPO Dubai kimya kimya na Rais kukaa huko kwa siri kubwa, kumbe anatia saini mkataba wa kutuuza!

5. Mkataba unavujishwa? Juhudi kubwa zinaanza kufukia mahandaki. Hapana, huo siyo Mkataba, hayo ni "Makubaliano tu, ikiambatana na upotoshaji mwingi mwingine, toka kwa waziri na mtu mwingine aliyeaminiwa sana kusimamia kujua kilichomo ndani ya Mkataba/Makubaliano" hayo. Mtaalam wa sheria mbobezi (tunaambiwa), Hamza Johari ndiye mkuu wa timu. Watu wanajiuliza, na Mwanasheria mkuu wa Serikali alishiriki vipi hadi kufika kwenye hatua hii?
Mwanasheria Mkuu wa Serikali hasemi kitu, bali kukanusha tu kwamba "Bandari haijauzwa". Hakuna anayejua kiwango cha ushiriki wake kwenye mkataba huo, na kama yeye, kwa nafasi yake anakubaliana na yaliyomo kwenye mkataba. Sijasikia akisema lolote juu ya hayo.

6. Taratibu na Hatua sahihi za kuingia mikataba kama huu (IGA) - Je, sisi kama taifa tunao utaratibu wowote tuliojiwekea wa kuingia kwenye mikataba kama hii? Huu siyo mkataba wa kwanza Tanzania iliouingia, je hiyo mingine kulifanyika mambo gani ambayo yamezoeleka kufanywa, lakini safari hii ikawa ni tofauti?

Hili ni swali lililo wazi, kama kuna utaratibu maalum, je ulifuatwa, hata kwa kiasi fulani tu?
jambo la kwanza linaloniingia akilini ni "Vikao vya Baraza la Mawaziri". Kwa mtizamo wangu, jambo kubwa kama hili haliwezi kufanyika bila ya uwepo wa angalao kikao cha Mawaziri kulijadili..
Vikao hivi vya Baraza la Mawaziri siku hizi vimekuwa kama ni siri kubwa sana, hata kule kutaja tu kulikuwepo na kikao siku hizi ni nadra sana, hata bila ya kutaja yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho.
Kwa hiyo hili ni swali tu kuuliza kama kulikuwa na kikao cha kujadili, au kujulishwa tu kwamba kuna mpango wa ujio wa DP World na hatua zilizokuwa zikifanyika kuwakaribisha hapa.
Kama Mawaziri nao hawakuwa na habari, hilo litakuwa jambo la kushangaza sana linaloongeza uzito katika hoja za andiko hili.
7. Ushirikishwaji wa Bunge katika "kuridhia Mkataba" Bila shaka yoyote palikuwepo na mpango kabambe wa kulishirikisha Bunge katika kufanya hujuma hizi, siyo kwa nia njema bali kwa nia ovu..
a) Kundi la wabunge lililopelekwa Dubai, ni utaratibu upi uliotumika kuwachagua hao waliokwenda? Wanazo sifa maalum ambazo zingewawezesha kutambua mambo ambayo hayana manufaa kwetu?
b) Waliandaliwa na kupewa semina wajiandae kuhusu maswala nyeti katika kazi wanayokwenda kuifanya huko walikokwenda? Walipewa Mkataba wausome wajue yaliyomo kabla hawajaondoka hapa?
Hawa wabunge ni akina nani hasa?

Kama maswali yote haya hayana majibu, maana yake ni kwamba hii ilikuwa ni mbinu tu, iliyotegeshwa kuhalalisha maovu juu ya nchi yetu, maovu waliyoyajua walioandaa mkataba huo na washirika wao wote.
c) Bungeni wakati wa kikao cha Bunge, ni wabunge wapi waliopewa nafasi ya kujadili yaliyomo kwenye mkataba, na ni nani aliyetoa nafasi hiyo kwa wabunge hao maalum? Hawa wabunge walijua kilichokuwemo kwenye huo Mkataba? Mbona hta mmoja wao hakujitokeza na anagalao kutaja tu hata kifungu kimoja alichokuwa nacho mashaka? Hawa wote waliandaliwa kwa maksudi kwa ushirikiano na uongozi wa Bunge?
d) Ushirikiwa wananchi, wanapewa masaa 24 kuleta maoni yao. Maana ya hili ni kwamba hapakutakiwa kuwepo na mchango wa wananchi ili lengo la kuhujumu nchi litekelezwe.

DPWorld wanao uzoefu mkubwa sana katika maswala haya ya Mikataba, kwa sababu kila sehemu walikokwenda wamekutana na chngamoto chungu nzima zilizowakabili.
Wamekuja hapa kwetu, wakamkuta mkuu wetu aliye tayari kabisa kuwapokea kwa masharti waliyoyapenda wao. Mkuu wetu hana uzoefu wowote, na isitoshe hana uchungu mkubwa kuhusu nchi anayoiongoza yeye, ila anayo madaraka ya kufanya lolote analotaka bila kuwajibishwa na yeyote.

Hapa ndipo tulipofikia sasa hivi.

Ingekuwa ni nchi nyingine, Mkataba huu usingemwacha huyu mkuu abaki salama, tena akiendelea kwenye madaraka yake kana kwamba hakuna lolote lililofanyika.
Lakini hii ni Tanzania. Yeye kishasema "Ameziba masikio", wenye kupiga kelele wapige kelele hadi wachoke wenyewe; lakini DP World hakuna wa kumzuia kuja hapa.

SAWA.
Sasa tumebaki na moja tu tunaloweza kulitegemea kuondokana na hujuma hii juu ya nchi yetu.
Je, tunaweza kumpata kichaa mwingine (bila ya baadhi ya mambo ya aliyetangulia mbele ya safari) atuondolee uchafu huu ndani ya nchi yetu? (Bila kujali hasara tutakayoingia kwa kuvunja mkataba (kwani kuendelea na mkataba wa aina hii ni hasara kubwa zaidi ya kulipa hiyo fidia tutakayodaiwa).
Na kwa kuwa ni 'kichaa', bila shaka baadhi ya hawa wahujumu watachukuliwa hatua bila ya kuwaonea aibu.

IGA baina ya Tanzania na Dubai ni hujuma iliyo andaliwa maksudi kuihujumu Tanzania.

N.B. Sikutegemea na wala siyo kawaida yangu kuandika gazeti, lakini leo acha iwe hivyo, kwani hakuna namna.

Samahani kwa makosa ya kiuandishi kama yamo kwenye andiko hili..
Basi kama ni hivyo jeshi limweke pembeni kama kilichotokea hapo niger juzi na wamwonye aache kuchezea rasilimali za nchi
 
Kuandaa kipindi kile na yule mwanasheria mkenya haikutosha.

Kumuita mbunge yule wa Arusha katika kipindi chako maalum na kuisambaza ile clip haikutosha.

Kutengeneza fake news nyingi na yenyewe kwako haijatosha.

Unapoteza muda na kutumia nguvu nyingi bure tu. Hatua itakayofuata ni kuandaliwa mikataba ya Consession na Lease kwa faida za wafanyabiashara.

Haliwezi taifa likatekwa na wasaliti wachache kama huyu Kalamu halafu wao hawana msaada wowote baada ya kuwa bandari yetu imekimbiwa na wateja!.

Kina Kalamu watakuwa wa kwanza kuicheka serikali hii hii kwamba imeshindwa kusimamia sekta ya bandari baada ya kuwa tumeshapoteza wateja wakubwa wenye kuipa mzigo reli ya SGR.

Dawa yao ni kukanyaga mafuta tu, kuitafutia maendeleo Tanzania.
 
Back
Top Bottom